Zero 65,000.. Maghembe unatupeleka wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zero 65,000.. Maghembe unatupeleka wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Einstein, Feb 8, 2010.

 1. Einstein

  Einstein Senior Member

  #1
  Feb 8, 2010
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimesikitishwa sana na matokeo ya kidato cha nne. Katika matokeo hayo zaidi ya 82% ya wanafunzi waliofanya mtihani, wamepata division zero au four!!!!!! Tunaenda wapi??? Ni lazima tujiulize credibility ya hawa wanaojiita mawaziri wanafanya nini ofisini??

  Nilipata kusoma shule moja ya pale Kilimanjaro(Shule ya ufundi). Nilikuwa nasoma ufundi wa umeme (O'level). Kwa kweli nilikuwa nashangazwa sana na utaratibu wa shule hiyo, katika swala zima la ufundi na baadhi ya masomo mengine. Zamani mtu alikuwa akimaliza shule ya sekondari ya ufundi alikuwa anaweza kujiajiri mwenyewe.. Lakini katika kipindi hicho ufundi huo niliosoma mimi swala la masomo kwa vitendo lilikuwa halitiliwi maanani.. Walim walikuwa wakijisifu kwa matokeo mazuri(Theoretically) ambapo wanafunzi hawa katika real life hawana chochote. Wengi waliosoma shule hizo wanaweza kuwa mashahidi kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya wanafunzi wanaomaliza shule za ufundi ni empty kabisa, hawana chochote.

  Baada ya hapo nilipata kusoma shule moja, wanayoiita ya vipaji. Kiukweli sielewi maana ya huu msemo. Ila huenda wanamanisha shule ni ya vipaji kwa maana zinachukua wanafunzi waliofaulu sana. Walimu wengi katika shule hizo hawana uwezo, mpango-mkakati wa kumjenga mwanafunzi kuwa CREATIVE. Hawana utaalamu wa kisaikolojia wa kumjenga mwanafunzi ili nae aweze ku-reason mambo.. HAKUNA!!

  Wanafunzi wengi wanaofanya vizuri, wanaotoka shule za serikali, wengi wao hujihangaikia wenyewe na kwa kusoma vitabu vya kutosha na twisheni ili waweze kuelewa mambo mbalimbali.. Kuna wakati mpaka wanafunzi wanaelewa mambo mpaka wanamzidi hadi mwalimu anaewafundisha ( Maana walimu wengi hawana vipaji vya kufundisha).

  Tanzania ni moja ya nchi isiyojali wasomi kwa kuwaacha wakijihangaikia wenyewe bila angalau ya kuwapa sapoti ya aina yoyote. Kwa mtoto wa maskini, hawezi hata kununua vitabu vizuri wala ya kulipa twisheni, ili aweze kujisomea ili afikie malengo yake.. Na wala haina taim nao, kwa maana, serikali inaona kuwa usomi ni swala lisilo na tija kwa taifa hili, bali siasa za kifisadi ndizo zenye tija..

  Naomba mwongozo:Kuna haja gani ya kuwa na majengo kibao ya shule, baadhi yaliyojengwa kwa kunyang'anya kuku na mbuzi wa wananchi, wakati walimu wa kutosha hakuna?? Ni bora kuwe na mwalimu makini anaewafundisha wanafunzi chini ya mti, kuliko kuwa na majengo ambayo wanafunzi wake wanafundishwa na ubao mweusi.

  Ndg. Majembe asimame sasa, atueleze kwamba mwaka huu katuzawadia zero 65,700. Anatupeleka wapi?? Mipango iko wapi?? Je, ndo kusema wanaongeza wajinga ili watutawale milele?? KWA NINI SERIKALI YA TANZANIA HAMJALI ELIMU??? Ingekuwa ni nchi zenye adabu, waziri huyu angejiuzulu mara moja, au Rais angempa adabu yake! Ila kwa sababu bongo ni TAMBARARE, anapeta tu na kodi za wananchi na wala hana shida.. Inasikitisha!!

  Wenzetu wa amerika na ulaya wanawaza jinsi ya kugundua vitu vizito na vyenye technolojia ya hali ya juu, SISI TUNAKAA KUJADILI JINSI YA KUPUNGUZA ZERO, Mmmh!! Huu ni upuuzi.. Haya mambo ya ajabu kabisa.

  Lazima watanzania tukae chini tujifikirie kuwa, Mfumo wetu huu wa elimu utatufikisha?? Wasomi wa Tanzania wanatapatapa tu huko duniani wanatafuta elimu, ingawa cha kusikitisha serikali yao haiwajali! Kama hatutakaa chini na kujipanga upya juu ya swala la elimu, basi hakuna sababu ya akina MKURABITA wala MKUKUTA, Maana yatupasa kuandika maumivu kuwa, sisi ni MASKINI MILELE..

  SO SAD!!
  Nawakilisha
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,153
  Likes Received: 27,131
  Trophy Points: 280
  Anatakiwa aresign..tena kwa haraka sana..huyu kwanza umri wa kustaafu haujafika??.hopeless kabisa.
   
 3. Einstein

  Einstein Senior Member

  #3
  Feb 8, 2010
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama hatajiuzulu, wanachi tunatakiwa kumfanya nini sasa? Maana huyu jamaa kazi imemshinda...
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,153
  Likes Received: 27,131
  Trophy Points: 280
  Wananchi hawawezi kumfanya kitu. yeye kawekwa na mshikaji wake.unaweza kukuta fani yake sio uongozi fani yange ni kufundisha tu .these are two different things then unategemea what gonna happens???
   
 5. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 8,378
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndio legacy ya CCM bana wametuletea shule za kata aka Bora shule,akina Lowasa na JK wakashupalia hizo shule kwa takwimu na mbwembwe nyingi ati ndio ilani ya chama kuboresha elimu loh hayo ndo matokeo yake na huyo profesa mzima kama kawa analeta visingizio vya mtoto aliyeshikwa akimung'unya sukari,anasingizia vitabu
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,153
  Likes Received: 27,131
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna mgongano ulitokea kati ya uanzishwaji wa hizi shule na ratio ya waalimu. ok hii product -hawa waliofeli wote wataenda wapi? na % kubwa ipo kijijini. je si watakunywa gongo hawa na kupewa zawadi za mimba?nani wakulaumiwa tena hapa? inabidi tuililie nchi yetu. What will be our future in this worlid of competition.?
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 23,169
  Likes Received: 6,881
  Trophy Points: 280
  Shule za kata zilianzihwa na Kikwete and Co hapo 2006 kwa hivo

  2006(FI)... no indicators than pomp and plumb
  2007(FII)...no indicators again,more political bashfulness
  2008(FIII)...teachers misbehaves,Col Mnali whips them and got fired
  2009(IV)...teacher got back to the old game...resulting with 65,000 failures!
   
 8. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,681
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Fanikio mojawapo ya mafanikio ya CCM ni kujenga shule nyingi na kuboresha elimu nchini, MAKAMBA MPIGA DOMO UPOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO! haya maziro yenu hayo hapo 65,000 watoto wa walala hoi wamepigwa chini na sera yenu. MAONI YANGU, WARUDIE KUFANYA MTIHANI SASA TUTAWAPELEKA WAPI????????????????????SOKO LA EAC KWELI HAWA WATAFANYA NINI KAMA KAZI ZOTE SI ZA WAGENI????????? Kiongozi wa CCM anapoingia ukumbini wanachama wanashangilia CCM, CCM,CCM,CCM
   
 9. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,840
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  I feel your pain brother. Inatisha.
   
 10. bht

  bht JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  unanitonesha kidonda Fugwe!!!!!!!!!!!
  agrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Feb 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  kwakweli akili ni nywele na kila mmoja anazake ila akili za Maghembe hazilingani na nafasi ya waziri mwenye dhamana na elimu yetu, hastuki wala kuogopa , yeye kwake ni faraja kwasababu mshahara na posho zake ziko constant, ameshindwa kuifanya elimu ya vijana wetu ing'are kwenye mwanga uliobora, watu tulisema sana wakati wanaanza kutumia waalimu wa Voda faster kua ni bomu lingine linategwa kwenye mfumo wa elimu ya TZ...wakazibz masikio, wakatenda walioona yanafaa sasa leo tunawataka wawajibike na matendo yao.
   
 12. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,734
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Napendekeza hizo pesa zitakazorudishwa na Waingereza kutokana na kashfa ya rushwa ya radar, yaani "vijisenti" kutoka BAE Systems, zielekezwe kwenye elimu. (Ila tuna uhakika kama zitafikishwa huko?). Bila kujali hilo, kwanza walipwe waalimu madeni ya haki zao zote bila ya visingizio vya "kuhakiki" kila mwaka. Pili wachukuliwe vijana wanafunzi waliofaulu vizuri masomo yao ya kidato cha sita wajiunge na vyuo vya ualimu kwa ajili ya kusomea stashahada za ualimu. Ualimu ngazi ya cheti ufutwe kama walivyofanya jirani zetu wa Zambia. Walimu wote kuanzia shule ya msingi wawe angalau na stashahada. Sifa ya mtu kujiunga na chuo cha ualimu iwe ni kuwa na angalao ufaulu wa division 3. Walimu wa vodafasta (miezi miwili) waondolewe mashuleni taratibu mpaka waishe kama hawatajiendeleza na kupata sifa zinazohitajika ndani ya miaka miwili. Na vile vile mimi nafikiri ni wakati muafaka wa kukubali kuanza kufundisha masomo katika sekondari kwa Kiswahili. Tunaweza kuwa na njia mbili zinazokubalika wale wanaopenda kufundisha kwa Kiingereza, hasa shule binafsi, waruhusiwe kuendelea. Lakini kwa hizi shule za kata Kiingereza ni mzigo. Waalimu wenyewe hawakijui na wanafunzi wenyewe hawana msingi mzuri na hiyo lugha kutoka huko kwenye shule za msingi. Sasa hii lugha mtu atajielezaje kweli ashinde mtihani wakati hata sentensi moja ya kuombea maji hawezi? Nimewaona vijana wajanja sana (waendesha taxi) wakikimbia wateja wazungu au wageni kwa sababu hawawezi kuongea nao. Hivi nini kinatufanya tufikiri kwamba kwa mwendo huu ipo siku tutakuja ku-master Kiingreza? Tutaanzia wapi? Halafu hili pendekezo (au tusemwe mwongozp wa JK) wa kitabu kimoja kwa kila somo kama utatekekezwa nao utakuwa janga jipya kwa elimu ya Tanzania. Tunaiiga nchi gani inayotumia mfumo huo? Tuache experiment zisizo na maana.
   
 13. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,458
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nilipomsikia Dr. Joyce Ndalichako anatangaza haya matokeo nilijua amekosea na kachanganya takwimu! Baada ya kuingia mtandaoni...nilihisi kutapika!!

  Serikali ya CCM need to be held accountable for this!!
   
 14. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa zile shule nyingi maarufu ka jina la shule za kata zalizoanzishwa kwa kasi miaka ileeeeee minne iliyopita wakati mheshimiwa na yule mwenzie mwenye mvi nyingi walipokuwa wanaingia madarakani ndiyo zimetoa form four wa kwanza sasa, kama kiongozi anafikiria kwa makini ni lazima atagundua haya ni matokeo ya upotofu wa sera ile, haina maana kujisifu kwa kuwa narundo la madarasa na malaki ya wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza wakati hakuna walimu wa kuwafundisha.,hakuna vitabu wala maabara nk, serikali ni lazima ijichunguze na kama hawaoni tatizo wajiunge hapa JF sie tutawaelewesha tatizo ni nini kuliko kupiga kelele majukwaani tu na kujisifu eti idadi ya wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza imeongezeka..,upuuzi mtupu, waziri husika alipaswa kuona aibu hii na kuamua kuwajibika lakini utamu wa madaraka ndio unaomziba masikio.
   
 15. s

  samvande2002 JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 414
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  KILIMO KWANZA!
  WE ARE NOT INTERESTED IN EDUCATION ANY MORE!!
  hahahaha, hahahah
  kaaaaazi kweli kweli!
  LAKINI HAO WALIOPATA ZERO (65,000) SI WANA ULE UWEZO WA KUANDIKA KWENYE ILE KARATASI YA KUPIGIA KURA NA KUPIGA KURA? fyi: SERIKALI INATENGENEZA WASOMI WAPIGA KURA TU!!! hiyo ndio ilani ya ccm; zaidi ya hayo yanatoka kwa yule mwovu!!!
  my take: "TZ U BETTER WAKE UP AND CHANGE THINGS..OTHERWISE ITS GONNA BE DIVERSTATING"
   
 16. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,098
  Likes Received: 716
  Trophy Points: 280
  WE TALK TOO MUCH....!
  SI NDO TUNATAKA WANAFUNZI WAWE WANAENDA NA SIMU SHULENI? WAWE WANATUNGA MISTARI SHULENI NA KUTOA SINGO ZAO? SI HATUTAKI WANAFUNZI WAADHIBIWE PINDI WANAPOKIUKA?
  MWALIMU HAPEWI NAFASI YA KUONYESHA UWEZO WAKE NDANI YA DARASA NA NJE YA DARASA.....!
  TUNAWAINGILIA NJE YA DARASA NA NDANI PIA...MATOKEO YAKIJA HOVYO TWALALAMA....!
  SHAME ON US......!
  Tuwape nafasi, wanetu wakishindwa tuwawajibishe....!
   
 17. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 909
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 80
  imebidi nikatafute kitambaa cha kufutia machozi maana hali hii inaumiza sana.
  Huyu Maghembe mimi nawasi wasi naye sana maana hata elumu yake inatia shaka, anaweza kuwa kama ngugu yake mmoja alikuwa anaitwa Prof Saburi, alishakuwa mkuu VC wa ARDHI (wakati ule ni College).Huyu amegundulika kuwa hakuwa na PHD halali. sasa na huyu jamaa na strategies zake zinanitia shaka sana
   
 18. D

  Domisianus Senior Member

  #18
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii inatisha sana kuna haja ya wadau wa elimu kukaa chini na kulitafakari hili vinginevyo, tutaisha.65700 siyo number ya kupuuza hata kidogo, hii ni status ya wilaya nzima hapa Tanzania, swali la msingi Je hawa wataenda wapi???????????
   
 19. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,581
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  ..........Tatizo mfumo wa elimu yetu ni mbovu na isitoshe zero nyingi hapa zimetoka shule za kata.
  Mtu ukitaka kufanya mtihani wa form 4 inabidi usome mambo yote uliyofundishwa tokea form 1 hadi hiyo form 4, na wakati form two ulishafanya mtihani ukaenda form 3 lakini bado tu usome vitu vyote.
  Ingekuwa bora ungekuwa unafanyika mtihani wa annual kwa kila kidato, baada ya hapo hakuna tena kurudia topic mlizozifanyia mtihani huko nyuma.Hii ingewasaidia wanafunzi kuwa makini kipindi wanaposoma na sio kukariri........huu mtindo wa kutoa mtihani topic zote za form 1 hadi 4 wala sio mzuri.
  ..........Kuna nchi huko magharibi wana system nzuri ya elimu, kama mtu upo grade 8 baada ya muhula kuisha mnatungiwa mtihani ambao una topic ya ile grade tu.......hawawezi kutunga mtihani wa grade 8 halafu kuna topic za tokea grade 1.
  Hivyo elimu yetu bado ipo ya kikoloni sana ya kuwapata watu wachache wa kufanya kazi badala ya wengi. Kwa mtindo huu we have a long way to go.
   
 20. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Prof saburi na Prof Mbyopyo; enzi zile ardhi ni college hawa walikuwa watu wakubwa sana Miungu watu; na si hawa tu kulikuwa na wengi pale nashukuru msimamo uliowekwa na Chuo Kikuu cha sasa walau sasa watu wanauona mwanga bora.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...