Masikini_Jeuri
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 6,829
- 1,296
65000 ziros!
Hili ni shimo ambalo hatukaa tulizibe tukiendelea na mtindo huu!
Hili ni shimo ambalo hatukaa tulizibe tukiendelea na mtindo huu!
Sasa ndo tumeelewa kwa nini ex-dc mnali na Makweta walikuwa sahihi!
Wakati fulani waziri makweta alishauri watoto wanaopata div zero wafikishwe mahakamani kwa uzembe na kuisababishia hasara serikali, nadhani niwakati mwafaka kulifanyia kazi hili wazo.
Kwaupande wa walimu nashauri uanzishwe mpango wa "performance contract" mwalimu atakaefelisha afutwe kazi na ikiwezekana apandishwe kizimbani kwa kuisababishia serikali hasara kwani kalipwa mshahara ili afundishe kazi ambayo hakuitimiza. Walimu wengi vijijini wanachukua mikopo NMB na kununua pikipiki then wanaanza kazi ya kubeba abiria na kusahau majukumu yao.
Madc wapewe jukumu la kufatilia mahudhuio ya walimu na wapewe mamlaka ya kuwafuta kazi watumishi wa umma walevi wazururaji na watoro.
Uwekwe mpango wa kutenganisha majukumu ya utawala na taaluma kwani walimu wakuu sasa wamekuwa "supplies officers" kutwa nzima wako na Quotation kwenye mikoba watasimamia taaluma saa ngapi?