Sio kweli kuwa ukawa ni wazushi sio kabisa,kama hujui naomba niseme na wewe kidogo, ukawa wana hoja, Katiba ni maridhiano sio ubabe au maslahi, CCM Wameshika Mpini ndio maana wanakataa kwa makusudi matakwa ya ukawa kwa sababu yatawaathiri na hasa kwenye uchaguzi.
Kama wewe ni muelewa mzuri katika kutunga katiba maridhiano ni muhimu sana ili kupata katiba ya wananchi inayojali maslahi ya wote, kila kundi katika nchi.
Kumbuka kuwa mapendekezo yaliyokwenda bungeni ni ya wananchi, Hivyo CCM Kutumia wingi wao kupuuzaa maoni ya wananchi sio sawa, walitakiwa wajadili walete kwetu sisi tuone kama itatufaa au la ! hapo ndipo wao wangeanzia.
Na sio kweli kuwa Watanzania wameona ukawa ni wazushi, Vibaraka na wachumia tumbo kama wewe ndio hasa wanaodharau ukawa.