Gefu
JF-Expert Member
- Nov 30, 2010
- 6,929
- 2,567
Nimefuatilia kwa muda mtazamo wa huyu mwanahabari zembwela na nimegundua kunamambo hafikirii sawa. Kwa mtazamo wake ni kwamba mbunge na diwani ndo mwenye dhamana ya maendeleo ya jimbo. Sitaki kuhoji kiwango chake cha elimu,lakini kwa mtu mwenye ufahamu unajua nani anawajibika kuleta maendeleo na nani anapaswa kupeleka vipaumbele vya wananchi husika. Bwana mdogo zembwela nadhani unapaswa kuwaunganisha vijana kuishinikiza serikali kutimiza yale mliyowatuma wabunge wenu wakayapeleke serikalini kwa kutengewa bajeti na utekelezaji. Lakini ukiendelea kuwaaminisha watu uzembe wa serikali ni wa mbunge unakosea. Sote tunawajua wabunge wawajibikaji na wazembe na lazima tuwawajibishe,lakini hujuma za serikali kwa baadhi ya wabunge kuwafanya hawawajibiki ndo kumezaa mfuko wa jimbo. Sasa wabunge wakiwa watendaji nani ataisimamia serikali ? Mwisho nilistuka na kuogopa zembwela alipowahamasisha wananchi kumng'oa diwani bila uchaguzi eti hawawezi kusubiri uchaguzi wakati anachelewesha maendeleo. Nahisi sheria ya uchaguzi haijui. Amekomaa na azimio la arusha bila kujua kuna azimio la zanzibar wameleta ccm.