Zee World na Indian Drama!

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
Kiasi cha wiki mbili tu zilizopita endapo pangetoea wa kuniuliza nawafahamu waigizaji wangapi wa Kihindi, jibu lingekuwa mmoja tu, Amitabh Bachchan! Na kama angeendelea kunitaka nitaje japo filamu moja aliyocheza Amitabh, it's definitely nisingekuwa na jibu! Katika maisha yangu yote, sijapata kuzipenda filamu za Kihindi, pamoja na mambo mengine, ni ile staili ya mlio wa magumi wanayopiga!

Wakati hayo yakiendelea, jumapili ya 15.03.2015 nikiwa ghetto nimetulia, vidole vikicheza kwenye remote, nikajishitukia tu naishia kwenye Zee World! Hii ni moja ya Channel ambazo endapo service provider angenipa option ya kuondoa channel yoyote na ili iwe replaced na yoyote hata kama ni Clouds TV, basi sina shaka ninge-opt waiondoe Zee World! Hapo kabla, sikuwahi kuiangalia hata siku moja... mara zote nilikuwa naipita tu !

Bila kutarajia, nikajikuta nimetuliza macho hapo Zee World... sina hakika ni nini kilinivutia, labda huenda nilivutiwa na binti wa Kihindi mwenye ngozi nyeusi! I think her innocence appearance ndiyo ilinivutia kutuliza macho hapo! Bila kutarajia, nikajikuta nimepoteza karibu dakika 15 na hatimae kuiweka remote pembeni... kuonesha ni kama nimefika! Punde si punde, nikagundua naangalia tamthilia iitwayo SALONI na huyo Binti wa Kihindi mwenye ngozi nyeusi ndie Saloni mwenyewe!!!

Niishie tu kusema kwamba, bila kukusudia, nikajikuta nimefuatilia episodes zote tano ambazo ni marudio ya wiki mzima!!! Wiki iliyofuata, nikajikuta siku mbili za awali (jtatu na jnne) naangalia marudio ya Saloni siku ya pili yake lakini hapa ninaposema, nimekosa kabisa ujasiri wa kusubiria marudio bali naangalia siku hiyo hiyo ya kwanza!!!

Wakati ya SALONI yakiwa hayo, Jumapili(au jumamosi, sikumbuki vizuri) iliyopita nikajikuta tena nimenaswa kwa staili ile ile ya jumapili iliyotangulia! Hata hivyo, siku hiyo nafahamu ni nini kilinivuta! Nikiwa nachezesha remote nikajikuta tena natua Zee World na hapo hapo nikakuta binti mwingine mdogo wa Kihindi mwenye umri wa takribani miaka 17-19. Kama ilivyokuwa kwa Saloni, Binti huyu nae alikuwa amejawa na innocence look lakini akionesha kuwa kwenye maswahibu makubwa zaidi kuliko alivyokuwa anaonekana Saloni! Kitu ambacho kilinivuta (sio kunivutia) ni kuona Binti huyu amepigishwa magoti huku mikono yake ikiwa imeegemezwa kwenye meza na jamaa mwenye jambia akiwa pembeni yake! Ilionesha dalili zote kwamba Binti yule alikuwa kwenye hukumu ya kukatwa mikono! Nikajikuta nataka kufahamu maswaibu yaliyomkuta binti wa watu!

Mikono ya binti yule haikukatwa lakini kama ilivyokuwa kwa Saloni, nikajikuta nimemaliza dakika 15 kama masihara na haikuchukua muda kubaini kwamba naangalia tamthilia ya LAALI na huyo binti aliyetaka kukatwa vidole ndie Naali mwenyewe! This's Laali, omg! Is the one of strongest characterization ever seen!!!

Kilichonikuta kwa Saloni, ndicho kimenikuta kwa Naali kiasi kwamba hivi sasa naogopa hata kuangalia matangazo ya tamthilia nyingine ninazoona wanazitangaza hapo Zee World kwa hofu ya kuwa mtumwa wa Zee World!!!

Swali ni kwamba, je humu jamvini kuna anayeziangalia hizi tamthilia? Kama yupo, ni kwamba ni uboya wangu ndio umenifanya hizi tamthilia zinibambe au kuna wengine ambao nao pia zimewabamba kwahiyo kama ni uboya basi tupo wengi?
 

Attachments

  • Saloni.jpg
    Saloni.jpg
    11.1 KB · Views: 318
  • Laali.jpg
    Laali.jpg
    12.2 KB · Views: 249
Una umri gani mkuu, na je umeanza kupenda lini movie?nauliza hivyo kwa kuwa wenye umri mkuba kidogo na tumeanza kupenda movie zamani basi ungejikuta tu unazipenda hizi movie za kihindi ma mastaa wake wengi tu ungewajua kwa kuwa wakati huo movie nyingi zilikuwa za kihindi zikifuatiwa na za kichina na kizungu kwa mbaali, usingekuwa mgeni na majina kama Rakesh Roshan, Amjad Khana, Rish Koop, Shash Kapool, Rajesh Khan, Jeetendra, Dharmendra, Hema malin, Rekha na wengine kibao
 
Una umri gani mkuu, na je umeanza kupenda lini movie?nauliza hivyo kwa kuwa wenye umri mkuba kidogo na tumeanza kupenda movie zamani basi ungejikuta tu unazipenda hizi movie za kihindi ma mastaa wake wengi tu ungewajua kwa kuwa wakati huo movie nyingi zilikuwa za kihindi zikifuatiwa na za kichina na kizungu kwa mbaali, usingekuwa mgeni na majina kama Rakesh Roshan, Amjad Khana, Rish Koop, Shash Kapool, Rajesh Khan, Jeetendra, Dharmendra, Hema malin, Rekha na wengine kibao
Wakati movie za Kihindi zikiwa hot nilikua na akili zangu timamu tena ule umri wa kukaa sebleni na machali wenzako mkiangalia hizo movie! Upepo ambao uliwakumba Watanzania na mimi haukunikumba ni pamoja na muziki wa Kongo... wale akina Awilo Longomba mie nilikuwa najionea wanapiga makele tu.... Niishie tu kusema kwamba, hayo majina yote uliyotaja ndo kwanza nayasikia kutoka kwako!!!
 
mkuu karibu katika ulimwengu wa wadosi.
naicheki sana zee world na hizo tamthilia mbili nazipata vizuri.

kama alivyotangulia kusema mdau hapo mwanzo. umri wako utakuwa wa kati.
wahindi ni wakali sana katika tasnia hii ya maigizo.

tafuta movies kama andhaa kaanon, sholay, yaadon kibarat, amal akbal Anthony, hatya, commando, tarzan halafu uje kutoa ushuhuda tena.
 
mkuu karibu katika ulimwengu wa wadosi.
naicheki sana zee world na hizo tamthilia mbili nazipata vizuri.

kama alivyotangulia kusema mdau hapo mwanzo. umri wako utakuwa wa kati.
wahindi ni wakali sana katika tasnia hii ya maigizo.

tafuta movies kama andhaa kaanon, sholay, yaadon kibarat, amal akbal Anthony, hatya, commando, tarzan halafu uje kutoa ushuhuda tena.
Mkuu wangu, unafikiri nina-doubt ukali wa Wahindi katika uigizaji? I don't doubt at all ema ndo hivyo tena na ndio maana nikazungumzia hata suala la muziki wa Congo! Ingawaje sikuwahi kuupenda but lazima nikubali itakuwa ni muziki mzuri otherwise usingependwa na millions of music fans including hata wale wasio wapenzi kweli kweli wa muziki!!

Katika movie ulizotaja hapo juu, naifahamu moja tu, hiyo ya Tarzan ingawaje sijui ilichezwa na nani!
 
Mi napenda sana movie za Lowassa. Kuna tamthilia mbili zitatoka soon.
1. Wajawazito wataandamana hadi Dodoma kumsihi asrudi nyuma kwenye mbio za urais.
2. Watoto na pampaz zao wataandamana wakitaka rais ajae awe babu mwenye kutetemeka ili wachezee mvi vizuri
 
Me ni mpenzi sana wa tamthilia na movie za kihindi smtime story zao me ndo hhwa nazipenda zinahusisha maisha yet ya kila siku
 
Tamthilia za kihindi cjapata bahati ya kuziona lkn kwa upande wa movies nimeziona nyingi sana, jamaa wanajua sana. Moja ya movies za kihindi ninazozikubali ni Dhadkan, Kuch Kuch hotae, andha kaanon, 3 ------, vishwatma, my name is khan, etc.
 
Tamthilia za kihindi cjapata bahati ya kuziona lkn kwa upande wa movies nimeziona nyingi sana, jamaa wanajua sana. Moja ya movies za kihindi ninazozikubali ni Dhadkan, Kuch Kuch hotae, andha kaanon, 3 ------, vishwatma, my name is khan, etc.
Dah! Hizi tamthilia wangu, nimezikubali sana coz' kama alivyoeleza juan david hapo juu, zinaelezea maisha halisi ya kila siku! Kwa mfano ukiiuchulia hiyo Saloni, moja kwa moja inahusisha maisha yao ya kila siku na changamoto cha desturi za Kihindi ambazo, kwa kiasi fulani zinafanana na za Kiafrika, tofauti ikiwa ni kwamba Waafrika tayari tumeshazibwaga tamaduni na desturi zetu wakati Wahindi bado wanazi-practice.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom