MVUMBUZI
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 5,182
- 2,304
-Vijana wabunifu sana, wasanii wa kweli! Walianzia EATV-walifanya vizuri, wakawa maarufu wakaitwa Bungeni mpaka Ikulu wakajisahau wakadhani ni maarufu kuliko EATV yenyewe, wakatemwa!
-Wakaja TBC wakaanza vizuri, wakapata tenda nono, wakajiona wako juu ya DUNIA, matanuzi kwa sana, wakaanza kutukana watu (kwamba wamefulia)!
-Sasa, hawana mvuto, hawaeleweki wanafanya nini, wanaburudisha au wanaganga njaa tu! mashabiki hakuna tena, Wapo TBC tu kwa sababu ya Contract ya Vodacom, Ikiisha-KAZI BASI! Warudi kijiweni...
Tuwaite nao wamefulia kama walivyowaita wenzao??
Message;
Ukiwa Juu usijishau na usione wengine ni wapumbavu badala yake ongeza juhudi zaidi na heshimu watu wote!
Mkuu inaonekana una bifu kubwa na hawa "The original Comedy" lazima kuna mahali mlikwaruzana tu pole sana. Ukweli ni kwamba hawa jamaa wamefulia na wamebakia kunywa bia mpaka wanashindwa kuwa wabunifu. Kwa sasa tunaopenda kucheka tumeamia EATV kwa akina Bambo, Kiwewe na Wenzake wale wako vizuri na ni wabunifu.
Kwa sasa hivi husikii mtu anakimbia home kuwahi the comedy kwani wanachofanya ni pumba tupu. Mfano jana alhamis hakuna walichofanya cha kuchekesha bali wameshindwa kutofautisha maigizo na vichekesho. wanatakiwa waende Kenya wakajifunze kwa kipindi cha "PASUA SHOW" kinachorushwa na KBC1 siku za Jumamosi kuanzia saa 2:30 usiku. wale vijana ni wabunifu ile mbaya hawaongei lakini wanachekesha sana.
Pia wakajifunze kwa akina Bambo kwani hata FUTUI siku hizi wamefulia baada ya Mkombe kuondoka.
Matangazaji wa the original Comedy' Masanja jana aliniboa sana kwani amepoteza mwelekeo kabisa anafanya mambo ya kitaahira badala ya kuchekesha.