Ze komedi -vs- Futuhi


acha uongo wako hawa futuhi wnaiga tuu mambo hii mbona joti na mpoki wameionyesha longtime wewee!! semaulikuwa hujatoka kijijini kwenu usukumani kuja mjini ukaona tv, pole mwanangu. The comedy wapo juu, waniga ze comedy hamuoni tuu?au ndo ukanda ya ziwa na ukanda wa bahari umeanza?
 

Acha bwana jamaa wana CURRENT ISSUES bwana sema wanaleta kwa style POA kama wanakubore JIFUNZE kuwazoea au usiwaangalie inawezekana nia yao ni kuwaopunguza watu kama wewe. bora ujumbe na nakumbuka enzi zile hata wanaume walikuwa wanapanda jukwaaani na kuimba nyimbo wakililia uke wenza lakini mpaka leo tunakubali nyimbo zao ni bora kuiliko za sasa!!!!

MMEFULIAAAAAA.........
 
nini futuhi bana!MAMBO IKO KOMEDI.kwa wasiolifahamu hili ni kwamba futuhi ipo maalum kwaajili ya watu wa janda ya ziwa.na wanaoibeba futuhi humu ndani ni walewale!

kina rwagubiri,kina mziwanda,kina nani sijui...........

FUTUHI BADO SAAAAANA KWA SASA!kwanza wana kamera moja tu,hawana edita mzuri,wanachemka sana tu,ni wanafunzi tu wale.na kila kitu wamedesa kwa komedi original
 
Ze comedy juu juu juuuu zaidi.
hapo mwana nakusapoti 100% hao futuhi wameiga vitu vingi kutoka kwa ze commedy nimeangalia vipindi vyao kama mara tatu i don see any creativity jamaniiii kuweni wakweli, kitu gani wamecreate just tell me? zaidi waweza kusema wameongezea na vyao kidogo lakini ile program nzima haina tofauti na ze commedy infact ukitaka kujua uzaidi kati yao angalia siku hivyo vipindi vinaonywesha halafu pita mitaa ya uswahili utaona population ya watu waliosimama bar kunaglia ze comedy kisha linganisha na futuhi jibu utapata,.
 
nimegundua JF wa kanda ya ziwa wako wengi sana, maaana mhhhhhh
afadhali mngesema kipindi cha ZEMBWELA cha ITV, nao wako kivyaovyao na wako juu
 
Kumbukumbu zangu ni kuwa Ze Komedi ndio wameiga star tV. Kabla ya Futuhi, start tv walikuwa na kundi la vichekesho na maigizo, kila walipokuwa wanamalizia vichekesho vyao walikuwa wanatumia sana nyimbo za Mbaraka Mwinshehe kuigiza (waliweza kuvaa raizoni, magitaa feki, wanaume waliweza kuvaa magauni n.k), mara tu hawa jamaa walipopotea ndio pengo hilo likazibwa na Ze Comedy (wakati huo Channel 5).
Hivyo basi Ze Komedi waliiga na sasa si muda mrefu watafulia na maji ya matope.
 
ze comedy wajiangalie maana upuuzi wanaofanya mtaani wakijafulia sijui watakuwa wageni.
utoto na ubitoz umewazidi

wajinga ndio waliwao!!!
 

Mkuu mm nikiangalia FUTUHI naona wanachekesha halafu wanacheka wenyewe ila ZE KOMEDI sometimes lazima ucheke mfano jana walinichekesha eti mtu anataka kuoa ana sh 7500/= Haya mambo yapo kwenye jamii.
 
salaam.

sijawahi kuiona futuhi, hivyo siwezi kuwalinganisha ( compare) na kueleza nani ni bora; ila tu tusiwalaumu ze komedi kwa kutia drag, hiyo nayo ni sehemu ya vichekesho. Angalia kwa mfano John Travolta kwenye hair spray au Robin Williams alivyocheza kama Mrs. Doubtfire hata Wesley Snipes amewahi kutia drag. Ni kutaka kuchekesha tu.
 
Last edited:
Futuhi bana wako juu.Nawapenda sana hawa jamaa. They are very original. Hao wengine pambafu tuu. Weka ile kitu ya poll tupige kura utaona wengi wataisaport Futuhii. This is only if kama umeziangalia zote.
 

Umenena bosi manake hata mimi jana nilicheck those guys wako vey samrt. Pia ile issue ya yule disabled aliyepewa wheel chair akasema hataitumia kwa kuwa watu hawatampa tena hela ya kutosha akiombomba manake wataona yuko vizuri lakini akiwa anatambaaa kwenye vumbi then watu wengi watamsaidia. This is the kind of things ambavyo vinatokea. So these FUTUHI guys wako safi.
 

hujawaangalia vizuri hawa futuhi. Wanajua wanachofanya na ni wasanii haswa. Give them 2nd chance
 

aisee babaangu mi nimetokea mo- moshi. Suala la vifaa ni la muda tu. Wako makini. Ze komed wabadilike
 
uzuri wa ze comedy kwamba wako creative zaidi anytime wanaweza kukusuprisze na kitu kipya kabisa, na hata kama una mastress yako utaishia kucheka na kuwa refreshed, na mara nyingi ukiwa unaangalia comedy hutakiwi kuwa serious sana na hata hao comedian hawatakiwi kuwa serious sana, kwa mtazamo wangu ze comedy are the realy comedians
 
Kwa mtazamo wangu naona FUTUHI wako juu ukilinganisha na hawa orijino komedi. Tatizo la Orijino komedi ni kwamba watu wengi wamewazoea na inaonekana hawana jipya. Ukiangalia uvaaji, mwanzoni ilikuwa ukimwona Joti amevaa kimini ndio ilionekana wanachekesha. Lakini hebu angalia kuchekesha kwao je kunafundisha jamii? Si ndio kwanza ukipita mitaani utakuta lidume lizima limesuka nywele au limevaa sketi, pamoja na kuwa ni wasanii je wanafundisha jamii?

Kwa upande wa FUTUHI kwa mfano kipindi kilichorushwa jana kuanzia saa tatu usiku kwenye tukio la mama mjamzito kupakiwa kwenye mkokoteni kutoka kijijini hadi mjini kujifungua, pale tayari wanatufundisha kuwa wananchi wanaotoka mbali sana na vituo vya afya (Hospitali) wanapata shida hasa kwenye suala la usafiri. Ukichukua tukio hilo na kulileta kwenye jamii si tayari wanatufundisha?

Kwa hali hiyo basi ndio maana nasema FUTUHI wako juu.
 
Ze Komedi wananiboa siku hizi, hasa yule anayejifanya muhaya mwenye pesa.
Siku hizi naweza kusahau hata muda wa kipindi, nimepoteza interest kabisa.
 

hunishawishiiii! sishaishikiiiiiiiiii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…