Zawadi ya Pasaka kwa wana Tegeruka na Mugango

Zawadi ya Pasaka kwa wana Tegeruka na Mugango

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
Tunaanza kwa kutoa shukrani nyingi sana kwa Serikali yetu inayoongozwa vizuri na Rais wetu, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

Kata 2 zilizokuwa zimeachwa kwenye Mradi wa Tsh Bilioni 71.5 wa Maji ya Bomba la Mugango, Kiabakari, Butiama, sasa zimepatiwa fedha (Tsh Bilioni 4.75) za kujengewa miundombinu ya usambazaji wa maji kwenye Kata hizo, zawadi ya Pasaka!

Kwa hiyo, wananchi waishio penye chanzo cha maji (Kata ya Mugango yenye vijiji 3) ya Bomba la hili, na wananchi waishio kwenye njia ya Bomba hili (Kata ya Tegeruka yenye vijiji 3), na wao watapata maji kutoka kwenye Bomba hili hili, hawajaachawa!

UWEKAJI SAINI WA MRADI WA TEGERUKA- MUGANGO
Mkandarasi wa Mradi huu wa Kata 2, ameishapatikana na taratibu zote zimekamilika, kifuatacho ni uwekaji wa saini.

Kijijini Mayani:
Jumatano, 12.4.2023, Saa 4 asubuhi,
WAHUSIKA watawekeana saini ya utekelezaji wa Mradi huu Kijijini Mayani, Kata ya Tegeruka.

Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali watakuwepo kushuhudia tukio hili la muhimu sana sana!

Karibuni sana kijijini Mayani tarehe 12.4.2023

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

Tarehe:
Alhamisi, 6.4.2023
 
Back
Top Bottom