utantambua
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,367
- 321
Jukwaa la sheria ungepata msaada zaidi, sielewi kwa nini umeprefer kuileta MMU, au kwa kuwa kisa kilianzia kwenye sherehe ya ndoa?
apeleke tinga tinga abomoe abebe tofali zake awaachie kiwanja
......................................
Unajua hakuna tensions mbaya kama za kifamilia....huwa hazina ukomo.....namuonea huruma''shemeji'' yetu kususwa na baba yake.....si kitu kizuri pamoja na wehu wa huyo mzee na familia yake........ni bora kurudisha hayo mahusiano japo kwa machalemachale kuliko kuendeleza bifu......akimtoa kwa mahakama itakuwa mbaya sana........am sorry....kujenga lilikuwa kosa kubwa....wengi yamewakuta ndio maana mimi niliuza cha Mikocheni nikanunua Bunju
miaka kadhaa nyuma, nilimpata binti mmoja wa kunifaa kwenye maisha nikaamua kufunga naye ndoa. Tukio hili lilitokea takriban miaka kumi na mbili iliyopita nyuma.
Harusi yetu, haikuwa ndogo kwa wakati huo, mamia ya watu walihudhuria na zawadi kem kem tulipewa. Mojawapo ya zawadi ilikuwa ni kiwanja ambacho baba mkwe alituzawadia mbele ya hadhara.
Baada ya harusi, nilifanikiwa kujenga nyumba kubwa kwenye kiwanja hicho cha zawadi kwa ushirikiano na mke wangu. Baada ya nyumba kukamilika, sisi tulikuwa tunaendelea kuishi kwenye nyumba ambayo ilikuwa inalipiwa na shirika maeneo ya oysterbay. Baba mkwe alistaafu na kuomba kukaa kwenye nyumba yetu kwa miezi michache wakati akimalizia ya kwake maeneo ya mbezi. Mimi na mke wangu bila hiyana, tukawakubalia wazee wetu wakae kwenye nyumba yetu kwa muda ma miaka 3 bure huku wakimalizia ujenzi wao.
Ndugu zangu, sasa yapata miaka 7 baba mkwe na mkewe hawataki kutoka kwenye nyumba yetu kwa kisingizio kuwa kiwanja ni chao na sisi tumejengwa kwenye kiwanja chao. Kinachoshangaza ni kuwa mpaka mikanda ya video ya harusi yetu nilishawahi kumuonyesha akitukabidhi hati za kiwanja kama zawadi, lakini mzee huyu katugeuka kabisa akishirikiana na baadhi ya watoto wake.
Kamtenga mke wangu-ambaye amekuwa karibu sana na mimi katika hili, na pia hataki hata kumuona na mimi kanizushia mambo kibao mabaya yasiyo ya kweli, naomba ushauri ndugu zangu nimtende nini mzee wangu maana na mimi nataka kuhamia kwenye hiyo nyumba na yeye hataki kutoka na nyumba yake keshamaliza! Hati ya kiwanja ninayo mimi maana alitukabidhi siku ya harusi.
Kosa langu ni nini, na nimfanyaje huyu mzee? Nimtoe kwa nguvu? Nahisi zawadi yake imenitokea puani!
***** ombi hili la ushauri limetumwa na rafiki yangu mmoja toka dodoma akiomba tumsaidie mawazo. Halina uhusiano na maisha yangu binafsi ***
wenu
horsepower
hapo pagumu..kama we kauzu mpeleke mahakamani kama unamwonea huruma peleka kesi kwa wazee wenzake wawasaidie...au alipe gharama ulizotumia kujenga nyumba
Hapo imekula kwa mshkaji, akubali tu yaishe kwamba ni sehemu ya mahari. Kwani kuna ubaya gani kuwajemgea wakwe zako nyumba? Hata akienda mahakamani bado itakula kwake, mzee huyo ni mzoefu atakuwa keshajiandaa. Ushahidi wa video ya harusi utatupiliwa mbali maana hiyo hati itakuwa haisomeki kwenye video, na mzee anaweza kusema siyo hiyo aliyokupa, na kwamba ile shamba aliyokupa uliikataa au akatunga uongo mwingine wowote.
Mkuu pole! Msikilize mkeo mkubaliane mnafanyaje maana hukusema mkeo analichukuliaje hili na pia mkumbuke kuna radhi ya baba yake
Hati ina jina la baba mkwe, na hakuna ushahidi wa kumwezesha kufanya transfer, zaidi ya hiyo video ya harusi. Kwa sababu ukitaka kufanya transfer ya hati lazima kuwe na ushahidi mfano mkataba wa mauziano, hati ya mirathi, tamko la donation nk (zote kutoka mmiliki wa awali pamoja na picha zake), sasa hapo kama tayari kuna bifu la kiwango hiki bado huoni imekula kwake?Sheria za nchi gani hiyo? Kakwambia hati anayo, sasa itkulaje kwake na uongo gani utakaotungwa na baba mkwe ili kufuta hati?
Huyo atakuwa ni mchagga tu.
Hati ina jina la baba mkwe, na hakuna ushahidi wa kumwezesha kufanya transfer, zaidi ya hiyo video ya harusi. Kwa sababu ukitaka kufanya transfer ya hati lazima kuwe na ushahidi mfano mkataba wa mauziano, hati ya mirathi, tamko la donation nk (zote kutoka mmiliki wa awali pamoja na picha zake), sasa hapo kama tayari kuna bifu la kiwango hiki bado huoni imekula kwake?
Radhi ya baba kwenye wizi?