MduduWashawasha
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 1,653
- 602
Machale HAYAKUKUNDECHA MEKU!!!!!!!!!!!!!ilitakiwa ubadilishe deed of transfer aisee.BIASHARA KWISHNE.tujipange utafte kingine ujenge.KIFUATACHO ITV UNAKIJUA......?
Miaka kadhaa nyuma, nilimpata binti mmoja wa kunifaa kwenye maisha nikaamua kufunga naye ndoa. Tukio hili lilitokea takriban miaka kumi na mbili iliyopita nyuma.
Harusi yetu, haikuwa ndogo kwa wakati huo, mamia ya watu walihudhuria na zawadi kem kem tulipewa. Mojawapo ya zawadi ilikuwa ni kiwanja ambacho baba mkwe alituzawadia mbele ya hadhara.
Baada ya harusi, nilifanikiwa kujenga nyumba kubwa kwenye kiwanja hicho cha zawadi kwa ushirikiano na mke wangu. Baada ya nyumba kukamilika, sisi tulikuwa tunaendelea kuishi kwenye nyumba ambayo ilikuwa inalipiwa na shirika maeneo ya Oysterbay. Baba mkwe alistaafu na kuomba kukaa kwenye nyumba yetu kwa miezi michache wakati akimalizia ya kwake maeneo ya mbezi. Mimi na mke wangu bila hiyana, tukawakubalia wazee wetu wakae kwenye nyumba yetu kwa muda ma miaka 3 bure huku wakimalizia ujenzi wao.
Ndugu zangu, sasa yapata miaka 7 baba mkwe na mkewe hawataki kutoka kwenye nyumba yetu kwa kisingizio kuwa kiwanja ni chao na sisi tumejengwa kwenye kiwanja chao. Kinachoshangaza ni kuwa mpaka mikanda ya video ya harusi yetu nilishawahi kumuonyesha akitukabidhi hati za kiwanja kama zawadi, lakini mzee huyu katugeuka kabisa akishirikiana na baadhi ya watoto wake.
Kamtenga mke wangu-ambaye amekuwa karibu sana na mimi katika hili, na pia hataki hata kumuona na mimi kanizushia mambo kibao mabaya yasiyo ya kweli, naomba ushauri ndugu zangu nimtende nini mzee wangu maana na mimi nataka kuhamia kwenye hiyo nyumba na yeye hataki kutoka na nyumba yake keshamaliza! Hati ya kiwanja ninayo mimi maana alitukabidhi siku ya harusi.
Kosa langu ni nini, na nimfanyaje huyu mzee? Nimtoe kwa nguvu? Nahisi zawadi yake imenitokea puani!
***** Ombi hili la ushauri limetumwa na rafiki yangu mmoja toka Dodoma akiomba tumsaidie mawazo. Halina uhusiano na maisha yangu binafsi ***
Wenu
HorsePower
Sasa ndio umekuwa mwanaume, sio mbaya kumjengea mkweo nyumba.
Jipange, nunua eneo sehemu nyingine kisha jenga nyumba nyingine
wa kule, kule, kule kule, mbokomu, useri, kirua na machame mpooo?
Wa kule, kule, kule kule, Mbokomu, Useri, kIRUA na Machame mpooo?
kweli jf ni chuo cha maisha ,,,,point well noted.Mpe pole ndugu yako.........mwambie aanze upya hapo hakuna suluhu....mimi nilipewa zawadi kama hiyo nikauza....halafu nikanunua changu mwenyewe
Je alikumbuka kuibadili jina baada ya kupewa? USHAURI WA BURE: Akubali kuwa imekula kwake! na ajipange upya ili kuepuka madhara zaidi.Lakini si ameshapewa hati ya kumiliki, ina maana yeye ndio mmiliki halali wa kiwanja kile. Aende tu mahakamani na hati miliki anayo.
Kama hati imeandikwa kwa jina la yule mzee na haikubadilishwa kuwa na majina ya watoto, hata kwenda mahakani ni kazi bure. Kimsingi washirikishwe ndugu ili swala hili liishe kifamilia. Vinginevyo huyu mzee alipiga hesabu mapema. Hakutoa zawadi.Lakini si ameshapewa hati ya kumiliki, ina maana yeye ndio mmiliki halali wa kiwanja kile. Aende tu mahakamani na hati miliki anayo.