Zawadi.... Ushawahi pata au kutoa?

Gaga

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
4,558
1,968
Habari za ijumaa wakuu, najua leo kila mtu anafurahia kuanza week end kwa namna yake.....Mie napenda kuja na hii,...... Zawadi, mnajua kwamba zawadi ni kitu kidogo sana lakini impact yake huwa ni kubwa sana hasa kwenye swala zima kwa wapendanao, kuna wanaopenda kupokea zawadi toka kwa wapenzi wao, lakini wao hata siku moja hawajigusi kuwapa wenzao zawadi ya aina yoyote ile, yaani unakuta mwenzake kila tukio au hata kusipokuwa na tukio lolote lile anachukuwa muda wake anamtafutia zawadi nzuri, embu jiulize kwa nini huwa humpi na yeye zawadi?

Nimeleta hili kwenu leo baada ya jana kukuta home nimeletewa sasa kama mnavyojua tena sie wadada huwa hatukawii kusumulia mashost ofisini na kama vile, mmoja wa marafiki zangu akawa analalamika kwamba kila mara huwa anampelekea zawadi mpenzi wake, iwe perfumes , shati, hata chocolate na cake za birthdays ila huyo wake hata siku moja hajawahi mpa zawadi hata ya pipi na sasa wana miaka mitano ya uhusiano.

Mwisho kabisa namalizia kwa kusema, zawadi sio kipimo cha mapenzi, ila ina maana sana kwa mpenzi wako, anaona kuwa unamjali na kumthamini sana, Pia umeacha shughuli zako ukakumbuka kuna mtu wako wa muhimu ukamnunulia zawadi, na zawadi inaweza kuwa yeyote kulingana na uwezo wa mtu, na nawakumbusha wadada kuwa wasijibweteke kwa kuona wao ndio wana haki ya kupewa zawadi na waume na wapenzi wao hata sie pia tuwe tunajitoa na kufanya hilo.. sasa nakuuliza wewe lini umemnunulia mpezi/mke/mume wako zawadi? embu jaribu leo hata pipi tu uone atakavyofurahi
Nawakilisha, ahsanteni wakuu.
 
Kuna wengine (wakati bado tuko kwenye mahusiano) tulikuwa tunanunua sana, yeye angalau hata kukumbuka kununua soksi wapii.
 
Aiseeee....pole sana!Embu niambie nikija daslamu nikuletee zawadi gani?!
Pitia Masai Camp uniletee jani la uhakika ambalo halijachakachuliwa maana kichwa changu kimeishakuwa kibovu sasa hivi kwahiyo bora kujilipua tu usisahau na ile kofia
 
Kuna wengine (wakati bado tuko kwenye mahusiano) tulikuwa tunanunua sana, yeye angalau hata kukumbuka kununua soksi wapii.
Ndio hao tunawakumbusha maana mtu unajituma mwenzio waapi, pole i hope mbele huko utapata mnaefanana kwa kila kitu
 
Pitia Masai Camp uniletee jani la uhakika ambalo halijachakachuliwa maana kichwa changu kimeishakuwa kibovu sasa hivi kwahiyo bora kujilipua tu usisahau na ile kofia
Mhhhhh unahisi inasaidia ile
 
Bora umenikumbusha mamito, nimezoea kupokea tu sikumbukagi kabisa kununua zawadi.
 
Yaaani mie napenda sana kubadilishana zawadi na mtu wangu nina imani nikiwa na kazi yangu ya maana nitanunua zawadi mpaka achoke,
 
Ilaa basi tu nimekaa na mwanamke miaka 5 sijui zawadi ya Bday yangu yeye anapata kila msimu wa matukio!bora ameondoka tu,kuna watu sijui ni uchoyo au malezi
 
Ilaa basi tu nimekaa na mwanamke miaka 5 sijui zawadi ya Bday yangu yeye anapata kila msimu wa matukio!bora ameondoka tu,kuna watu sijui ni uchoyo au malezi
looo ndio wale wanaopenda kupewa tu wao hata tie kununua anaona hasara
 
Safety last 04:30 PM Today Ilaa basi tu nimekaa na mwanamke
miaka 5 sijui zawadi ya Bday yangu
yeye anapata kila msimu wa matukio!
bora ameondoka tu,kuna watu sijui ni uchoyo au malezi
Mkuu Safety dah! Hiyohutokea aisee!
 
Duuu mie napenda sana kununua zawadi mara kwa mara na yeye pia hivo ngoma droo, mara nyingi huniambia angekuwa na uwezo angeninunulia dunia nzima ili niwe na furaha, kupendwa raha sana ndugu zangu
 
Pitia Masai Camp uniletee jani la uhakika ambalo halijachakachuliwa maana kichwa changu kimeishakuwa kibovu sasa hivi kwahiyo bora kujilipua tu usisahau na ile kofia
Nakuletea present card ya mtoa ushauri mmoja hivi anaitwa LIS...mtafute skype uongee nae mwambie nimekutuma!!
 
Mama watoto naenda kumnunulia hii zawadi leo
Sexy_Night_Dress.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom