Zawadi nono ...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zawadi nono ...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KYALOSANGI, Feb 2, 2011.

 1. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Matokeo ya MITIHANI kidato cha nne yamezua tafrani kubwa ,kinachonishangaza mm ni mshangao wa watu kuhusu matokeo hayo !Ni mshangao kwa sababu kila anayefanya uchunguzi kidogo tu angetarajia hali hii kutokea! Hii ni kwa sababu serikali ya CCM inayataka haya yatokee ,mbona wanaposhereheke kuchaguliwa wanafunzi kwa asilimia 100 nasi tunacheka ! Walipo ulegeza mtihani wa kidato cha Pili mbona tulikaa kimya wakati huo ulikuwa ni mkakati wa kufuta aibu ya elimu bomu inayotolewa .!Ili kufahamu kuwa watunga sera wote hawapeleki watoto wao kwenye shule hizo wanazoringia ...naomba mtu anitajia ni mkubwa gani wa serikali anayesomesha watoto/mtoto shule za kata ...akijitokeza nitampa zawadi ya ....ofa ya Kitimoto!
   
 2. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  acha masihara kwenye mambo mazito ya kitaifa unadhani kila mtu humu anakula kitimoto?
   
 3. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Samahani ni ugeni tu,unajua kwetu kitimoto ni kama maji ya kunywa sijui kama kuna dunia nyingine kuna watu hawali nyama hii tamu ,naomba wanisamamehe wao nitawapa nyama ya ulimi!Ila sifanyi masihara hata kidigokama vigogo hawasomeshi watoto wao huko hizi shule ni za nani!
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  WaTZ tunachekesha kwelikweli; tunataka tukute chakula kizuri mezani tu!
  Ili ukute chakula kizuri mezani lazima uzuri wake uanzie kwenye maandalizi:
  Kwenye kulima/kununua
  kwenye kukiandaa/kukipika nk.
  Hebu fikiria ni mwalimu wa aina gani anamfundisha mtoto toka chekechea hadi darasa la 7? Huyu ni yule aliyefeli kidatocha nne (eti div4 ya point 28) Msisahau kuwa bado tunao wale wa UPE pia.
  Hebu fikiria ni mwalimu wa aina gani anyemfundisha mtoto huyu sekondari? Tumeona karibu nusu ya wahitimu wa diploma za ualimu wamefeli (wanatakiwa kurudia) Je huyu akimfundisha mwanafunzi nae si lazima atarudia rudia tu.
  Hebu fikiria maslahi ya wanaoandaa wanafunzi wetu - yakoje? Mmesikia kuwa serikali iliamua kufuta posho kwa wafanyakazi wake ispokuwa Polisi na JWTZ; hii mana yake mwalimu posho yake ikatwe!
  Kweli tusitarajie miujiza ya kuvuna usipopanda.
  Nilikuwa naongea na mjerumani mmoja yeye alishangaa kuona TZ wanaokwenda kusomea ualimu ni watu wenye ufaulu wa chini na aliniuliza hivi huyu wa ufaulu wa chini ataweza kumtoa mwanafunzi aliyefaulu kwa kiwango cha juu? Kwao Ujerumani waalimu ni watu waliofaulu kweilkweli na ni katika kundi linalopata maslahi ya juu.
  Sisi huku watu wanaukimbia ualimu kwa sababu ya maslahi duni na ndiyo maana aliyepata div2 ukimwambia kwenda ualimu atakwambia humtakii mema.
  Suluhu - ebu tuboreshe maslani yao halafu tufanye hivi - wale wanaohitimu form 4, tukishachagua wa kidato cha tano, wanaofuatia waende ualimu, vivyo hivyo kwa kidato cha sita. Hatuwazuii; kujiendeleza baadae From there tutapata matokeo mazuri yatakayozaa wataalamu; kwa vyovyote kuna kipindi (mpito) tutaumia lakini kwa matumaini mema baadae
   
 5. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  igwee! Kama unatumia ile nyama nakukaribisha!
   
Loading...