Mapenzi ya sasa yamejengwa zaidi katika zawadi. Usipomnunulia mpenzi wako zawadi, mpenzi wako anakuwa na negative thoughts kuwa humpendi. Huwa kun imani kuwa unapomnunulia mpenzi wako zawadi ndivyo anavyokuthamini. Na ukisha jenga hii dhana ya zawadi mara kwa mara, ikatokea kipindi fulani umekaa sana bila kumpa zawadi basi huamini kuwa una mwingine.
Wengi niliowauliza wanaamini maisha haya ya zawadi zaidi kuliko utu. Watu wa miaka ya nyuma wa hawakuwa hivi. Hi ni kwa sababu ya ushindani wa hali ya kimaisha yanayotuzunguka. Mathalani, kijana hatathubutu kumkaribisha ndani kwake msichana wake kama hajakamilika ndani, likewise. kwa hiyo kuna imani kuwa vitu kwanza, utu baadaye!