zawadi gani mimi........................ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

zawadi gani mimi........................

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by gfsonwin, Jul 1, 2012.

 1. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,900
  Trophy Points: 280
  Wapenzi wa jf ni jumapili njema sana, kwangu na kwako pia naamini. Napenda kabla ya yote nitoe pole sana kwa Dr Ulimboka na kwa mkewe specifically Bi Myovella kwa yaliyoikuta familia yake Pia napenda niwaombee safari na matibabu mema sana, shemeji yangu mpenzi Pascal Lugajo naamini Mungu atakulinda na atakuwa pamoja na wewe.

  Siku ya leo naomba kila mtu atayatafakari haya maneno katika moyo wake ili aweze kujitambua yuko wapi na kwanini yupo hapo alipo.

  Zawadi gani gani mimi, nitamtolea Bwana, ila roho yangu tu.
  Pokea vitu hivi Bwana tena,
  uvibariki Bwana,
  uvijaze baraka zako
  pia na Roho yangu.


  Nami nitoe nini kilicho cha thamani kwako,
  Ila roho yangu tu.
  Pokea vitu hivi bwana
  uvijaze baraka zako
  Pia na roho yangu.

  Pia tafakari maneno haya mpendwa ya wimbo huu

  Nalistahili kupotea,
  lakini nahurumiwa.
  Mungu amenipatanisha na
  yeye kwa Yesu Kristo.
  /: Hivi vyote vyatoka wapi?:/
  /:Nasema ni huruma tu:/

  Ni hayo tu wapendwa wangu leo najiskia kuadhimisha Mungu zaid nafsini hasa ninapotazama pale anapopita Dr Ulimboka lakin pia pale wanapopita wale waliopoteza wapendwa wao kwasababu ya mgomo wa madaktari. je mimi ni nani leo hii niwe mzima na wanangu ukilinganisha na hawa wengine? hakika sina kubwa zaid kwa Mungu ila ni kwa neema tu na mimi namrudishia yeye sifa na utukufu na heshima.
   
 2. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,650
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  Amen! Umeniimbisha pasipo kutarajia. Be blcd!
   
 3. a

  asumpta Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Asante kwa kutumbusha tuwaombee wenzetu.
   
Loading...