Zawadi aliyopewa imemweka njia panda

Zawadi aliyopewa imemweka njia panda

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
1,911
Reaction score
1,322
Kama walivyosema wahenga wa kiingereza, 'The end justify the means'. Vita ni vita na kilicho muhimu ni ushindi, mbinu gani imetumika na kwanini huja baadae. Kuna rafiki yangu ambae siko nae rika moja. Mimi ni mkubwa kiasi kwake. Jamaa alipomaliza chuo kikuu alikaa mtaani kwa karibu miezi 18 pasipo kazi.

Katika kujihami akaingia kwenye mahusiano na mama mtu mzima ambae ana jishughulisha na "mama lishe". Dhamira ilikuwa inamsuta, lakini ndio basi tena. Pamoja na utu uzima wake mama wa watu anajua mapenzi. Anajua ku'care' ana utu na zaidi ya yote ni mtu mwenye moyo mzuri.

Ilikuwa ni kama kujaribu lakini taratibu kijana akajikuta kakolea hadi watoto wa yule mama wakahisi kuna jambo. Hakuchi hakuchi mwisho kunakucha, jamaa yangu akapata kazi mgodini. Baada ya kufanya kazi kwa miezi 6 baadhi ya mambo akayaweka sawa na pesa ikaanza kumfuata badala ya yeye kuitafuta.

Akarudi kwa mama na kumdanganya kuna watu wa benki nimeongea nao ili wakupe mkopo ujenge vizuri jiko na sehemu ya kulia wateja. Mama akakataa "mimi siwezi mikopo inafirisi". Ikaanza kazi ya kumshawishi hadi akakubali. Jamaa akatoa pesa mfukoni akajenga jiko na sehemu ya kulia wateja vizuri.

Mama akapangiwa lejesho ila akaambiwa awe anaweka kwa jamaa then yeye ataziwasirisha benki. Miezi 9 ya marejesho iliisha mwezi wa 3 na mama alirejesha kwa uaminifu mkubwa. Jamaa akachukulia riba na kumnunulia mama nguo (wax, Madera) akamwambia huwezi amini benki wamekupa zawadi kwa urejeshaji wako mzuri.

Pesa zilizobaki akanunua mchele, sembe & dona, sukari, unga wa ngano, tambi, mafuta ya kula na maharage. Akampatia mama na kumwambia ni mkopo wa benki atakuwa alirejesha kama mwanzo. Juzi alipokuja kwenye pasaka mama wa watu kamkalisha chini jamaa yangu na kumwambia "Wema unaonitendea hauna mfano, nimeamua nikuozeshe binti yangu (akamtaja jina).Usiwe na wasiwasi huyu nimejizaa mwenyewe hata kusumbua". Jamaa akasema asante nipe muda wa kutafakari.

Zawadi hii maalumu imemwacha jamaa yangu njia panda. Mama huyu ni mjane.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
mmmmmmmmmmmm,yataka moyo,umeshakula mama na watoto wakajua sasa unakula mtoto na mama anajua mbona kama na smell kitu zaidi ya fadhila? kama fadhila ameshalipa aseme Ahsante aende zake.
 
kwanza jamaa ameshaacha kumgegeda huyo mama? au ndo anataka amwoe huyo mtoto awe anakula kuku na mayai yake? hili lataka moyo kwa kweli
 
heeh hivi haya yapo enh huyo mama mh ngumu kumeza hii sasa akishaolewa ndo na yy uhusiano utakata ama ila jaman dah haiswih
 
kwanza jamaa ameshaacha kumgegeda huyo mama? au ndo anataka amwoe huyo mtoto awe anakula kuku na mayai yake? hili lataka moyo kwa kweli
Jamaa tangu alipoanza kazi aliacha kumgegeda mama. Aliamuamu kumsaidia sababu ya Wema aliomfanyia wakati hana kazi. Maana alichokipa kwa huyo mama ni zaidi ya mapenzi.
 
heeh hivi haya yapo enh huyo mama mh ngumu kumeza hii sasa akishaolewa ndo na yy uhusiano utakata ama ila jaman dah haiswih
Mama kwa kuwa ni mtu mzima huenda kuna vitu kaviona kwa huyu jamaa yangu ambavyo ni "unique". Na kaona mtoto wake akiolewa atakuwa kwenye mikono salama. Kwani urithi lazima iwe Mali?
 
Hili jambo ni gumu sana, ina maana mama mkwe anakuwa ex wako na mwanao wa kufikia anakuwa mkeo???? Ni zawadi ndiyo lakini haitekelezeki. ili kuepuka matatizo huko mbeleni bora huyo jamaa aachane nao wote tu
 
Mama kwa kuwa ni mtu mzima huenda kuna vitu kaviona kwa huyu jamaa yangu ambavyo ni "unique". Na kaona mtoto wake akiolewa atakuwa kwenye mikono salama. Kwani urithi lazima iwe Mali?

mmmmh napita tu
 
Kwa experience yangu na wanawake, hili jambo umelitunga. Mwanamke mliyeclick, tena mjane hana comitment walahi hawezi kuacha kirahisi rahisi hivyo hata kama kashapita mda wa kukupa watoto.
 
Aisee, mambo mengine hata hayafikiriki. Anaanzaje sasa kumuoa huyo binti wakati ameshalala na mama...!
 
Kwa experience yangu na wanawake, hili jambo umelitunga. Mwanamke mliyeclick, tena mjane hana comitment walahi hawezi kuacha kirahisi rahisi hivyo hata kama kashapita mda wa kukupa watoto.
Waingereza husema "don't say impossible even if it is impossible". Hiki ni kisa mkasa cha ukweli tena nimekiwasirisha "live". Na tunayaweka bayana ili wengine wajifunze Lakini waweze kutoa ushauri wao.
 
Sikamona na zawadi ya ushindi. Ila kama mama ameridhia kamata kichwa kimtindo, chamsingi anagalia kama mnaendana isije leta mkangangiko na ndoa ikawa chungu sababu mitihani ni mingi sana.
 
Back
Top Bottom