Zanzibar yagoma kulipa Sh40 bilioni Tanesco | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar yagoma kulipa Sh40 bilioni Tanesco

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Apr 6, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tuesday, 05 April 2011 19:34

  [​IMG] Waziri wa Ardhi, Maji, Makazi na Nishati wa Zanzibar , Ali Juma Shamuhuma

  Salma Said, Zanzibar
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekataa kulipa deni la umeme la Sh 40 bilioni kwa TANESCO baada ya kupandishiwa kiwango.Waziri wa Ardhi, Maji, Makazi na Nishati wa Zanzibar , Ali Juma Shamuhuma alisema baada ya kiwango kuongezeka, serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatakiwa kulipa kwa asilimia 168 badala ya asilimia 21 kwa uniti.

  Shamhuna alikuwa akichangia katika majumuisho ya mjadala juu ya ripoti ya Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambapo Shamuhuna alisema, “hatukubali kulipa deni la Sh 40 bilioni kwa kiwango cha asilimia 168 asilani.”

  Tanesco ilipandisha viwango vya malipo kwa wateja wake tangu mwaka jana kwa asilimia 21, kwa upande wa Tanzania bara ambapo kwa Zanzibar shirika hilo la umeme limepandishwa kwa asilimia 168 na kusababisha malalamiko makubwakutoka kwa wateja.Shamhuna alisema kuendelea kwa Tanesco kudai deni hilo kunakwenda kinyume na agizo la Rais Jakaya Kikwete kwamba pande zote mbili za Muungano zilipe viwango sawa vya asilimia 21.

  Waziri huyo ambaye alikuwa akichangia na kupigiwa makofi na wajumbe wengine alisema ili kuepukana na utegemezi wa umeme kutoka Tanesco ambao unaigharimu SMZ fedha nyingi, serikali umeanza kuchukua hatua za kuzungumza na wawekezaji wazoefu ili kuzalisha umeme kutokana na jua na gesi utakaojitegemea.

  Shamhuna aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba mradi kama huu umefanikiwa Dubai na Malaysia unaweza kuzalisha kati ya Megawati 50 na 100 ambao unatosheleza mahitaji ya sasa ya Zanzibar ya Megawati 50.  Hata hivyo, akizungumzia kuhusu madai ya baadhi ya Wajumbe wa baraza la Wawakilishi wanaotaka Zanzibar izalishe umeme kwa kutumia mawimbi ya bahari, Shamhuna alisema utafiti unaonyesha kuwa ni mradi mkubwa wenye gharama kubwa na pia haujafanikiwa katika nchi nyingi duniani.

  wakichangia mjadala huo wajumbe wengine wa baraza hilo wamesema suala hilo linahitaji kuangalia vyema na serikali ya muungano kwani haiwezekani serikali hiyo kukaa kimya na baadhi yao kutaka fedha hizo kutolipwa kwani haitowezekana.
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwani mtu asipolipa bili ya umeme anafanywa nini? Labda wawekewe luku.:hug:
   
 3. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wasipolipa si mnawakatia tu huo umeme?
   
 4. f

  fisi 2 JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,330
  Likes Received: 516
  Trophy Points: 280
  Zanzibar ni practically wilaya tu ya Nchi yetu tukufu ya Tanzania. kuleta ukorofi ni kichwa ngumu. Nawaamrisha walipe faster kabla hatuja ka Gadafi.
   
 5. n

  nndondo JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na Zanzibar, hii serikali ni shenzi ni sisi bara tu huku ndio tumejaa ujinga na upumbavu,
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Kama hawalipi wawekewe LUKU.
   
 7. f

  fisi 2 JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,330
  Likes Received: 516
  Trophy Points: 280
  "hii serikali ni shenzi "
  Mtume simama,UHAINI LIVE
   
 8. Mkubwa ndevu

  Mkubwa ndevu JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Luku zipo kila nyumba znz bt huku zinaitwa TUKUZA hapa mimi cjafahamu hizi pesa wanadaiwa znz hawajalipa au wanataka kulipa wanaambiwa kidogo
   
 9. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  Angalia ukubwa wa Taifa la Zanzibar ulivokuwa wakati huo na ulinganishe na ile ilivyokuwa kabla ya 26 April 1964 .Ni jambo la kusikitisha kuona Utaifa wa Zanzibar uko ukingoni kupotezwa katika Ramani ya Dunia. Nawaletea ramani kongwe ya Bara la Afrika ambayo inaonesha mipaka ya Zanzibar mpaka mwaka 1669
  MAPAFRICAL0011.jpg
   
 10. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,187
  Likes Received: 704
  Trophy Points: 280
  Ni jambo la kusikitisha kuona Utaifa wa Zanzibar uko ukingoni kupotezwa katika Ramani ya Dunia. Nawaletea ramani kongwe ya Bara la Afrika ambayo inaonesha mipaka ya Zanzibar mpaka mwaka 1669. Angalia ukubwa wa Taifa la Zanzibar ulivokuwa wakati huo na ulinganishe na ile ilivyokuwa kabla ya 26 April 1964 . View attachment 26805

  Ramani hii inaonesha kuwepo kwa Zanzibar kabla ya kuzaliwa nchi za Afrika Mashariki, Zambia na Zimbabwe.
   
 11. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mbona huleti ramani ya UARABUNI ili tuelezwe Zanzibar ilivyo sehemu ya Uarabu?
  Mbona wazunguka sana?
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Post yangu ya kwanza leo(post no 2),ya msemo maarufu wa Kizenji, Changu changu, chako chetu mbona imechakachuliwa?
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Katia UMEME hao wake wa CCM.... maana Chadema wakiandamana kuwa Maisha ni Magumu, wao wanaKEJELI.

  Sasa mambo yanaanza kuwa ma-HARD, wanakuja na mambo ya Nyerere kukataa kulipa.

  Nawashukuru sana CCM kuwapandishia hatimaye Wazenji UMEME ili na wao wakome.

  Mnalilia kujitenga, si muwe na UMEME wenu wenyewe?

  Waiteni Mabwana zenu wa zamani kutoka Uarabuni waje wawawekee UMEME wa BURE.
   
Loading...