Baada ya wiki mbili kutoka sasa, (tarehe 10 Disemba 2016) inafika siku ya Uhuru wa Zanzibar, siku ya Zanzibar kujigomboa na makucha ya ukoloni wa Kingereza mwaka 1963. Kwa muda ya miaka 53 tumesahaulishwa siku hii tukufu ambayo walishirikiana wazee wetu wa pande zote za siasa na makundi ya kabila zote na tabaka zote kupigania Uhuru na wakasherehekea pamoja tarehe 10 Disemba 1963. Leo siku hii tukufu haisherehekewi Zanzibar wala hapana kiongozi yeyote aneitaja siku hii, si CCM wala si CUF. Anakuja kijogoo cha Bara Tundu Lissu kuwafundisha vizazi vipya vya Zanzibar kwamba nchi yao ilipata Uhuru kutokana na utawala wa ukoloni wa Kingereza tarehe 10 Disemba 1963.
Baada ya kupita miezi minne kutoka siku ya Uhuru (26 Aprili 1964), Zanzibar ilipoteza Uharu wake kwa kuingia kwenye makucha ya mtawala mpya na kugeuka kuwa sehemu ndogo ya jamhuri mpya ya Tanzania. Tokea hapo 1964 mpaka hii leo nchi yetu ya Zanzibar haijasita kudai iwe na haki Zaidi katika huu utawala wa ukoloni mpya wa mabavu unaoitwa Muungano wa Tanzania. Mzee Rais Abeid Amani Karume kapoteza roho yake huku anajaribu kulivua koti la Muungano lililokua linaibana Zanzibar. Si siri kwamba Sheikh Karume alifika kuwa hasemi na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa sibabu karume anataka kutokana na Muungano. Nyerere akamuweka Alhajj Aboud Jumbe kushika pahala pa Sheikh Karume. Rais Alhajj Aboud Jumbe nae akataka kutokana na maonevu ya Muungano. Nyerere akawatumia vibaraka vyake kutoka Zanzibar kumfitini Rais Alhajj Aboud Jumbe akaishia kufukuzwa kwa adhara na kashfa.
Miaka michache iliyopita alisimama mwana halisi wa Zanzibar Sheikh Farid na Mashekhe wenziwe wa Uamsho wakadai Uhuru kamili wa Zanzibar. Leo Mashekhe hao wametupwa gerezani na kuadhibiwa na kunajisiwa kwa sibabu ya mapenzi yao ya Uhuru wa Zanzibar yao. Badili ya kudai Mashekhe wa Ukawa watolewe kifungoni, anasimama mwanasiasa anawakejeli kua “leo wako jela wanakunya kwenye ndoo”. Aibu gani Zanzibar kua na wanasiasa kama hawa?
Jitihada ya kudai Uhuru wa Zanzibar zimeendelea baina ya wananchi wa Zanzibar miaka yote iliopita. Wananchi wamechoka na utawala wa kikoloni wa Tanganyika. Kwa bahati mbaya viongozi wa Zanzibar hawakuthubutu kupeleka mbele matakwa ya wananchi. Badala yake wakawa wanababaisha wanachi kwa kudai serikali tatu au mengineo. Hapana kiongozi yeyote Zanzibar anaethubutu kuisemea nchi yake na kudai Uhuru wa Zanzibar kama anavyo isemea Zanzibar kijogoo cha Tanzania Bara Tundu Lissu.
Sasa imefika wakati wanasiasa wa Zanzibar washughlikie matakwa ya Wazanzibari kudai Uhuru wao kutokana na Muungano. Wananchi hatutaki Muungano. Wanasiasa wa CCM na CUF ama watuunge mkono kudai Uhuru wetu kamili mwaka 2017 au wawe tayari kutupwa na wananchi kwenye madebe ya taka ya historia.