punainen-red
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 1,731
- 450
Jamani! Hii weekend imewafanyaje wakuu??? Mbona ni kama wengi wenu mmemtafsiri six tofauti? Au nimepata makengeza labda.. Sita anapinga hoja ya serikali tatu, anataka mfumo uliopo uendelee, anasema kuweka serikali tatu ni sawa na kuuvunja muungano, anadai sasa hivi bara ndo inabeba gharama za muungano, hivyo tukiwa na serikali tatu itabidi bara ibebe serikali yake na ya muungano. Binafsi siutaki wala siupendi muungano, lakini sijaona mahali sitta amesema zanzibar haitaweza kujitegemea nje ya muungano.