Constitutional Law 101:... Walikula kiapo kulinda Katiba hii na Muungano huu sasa wanapata wapi ujasiri wa kutaka Muungano uvunjwe? Au waliapa hawakujua wanachoapa ni kitu gani?
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
98.Utaratibu wa kubadilisha Katiba hii na baadhi ya sheria.
1) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kubadilisha masharti yoyote ya Katiba.
2) Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara ndogo ya (1) kubadilisha masharti ya Katiba hii au masharti ya sheria maana yake ifahamike kuwa ni pamoja na kurekebisha au kusahihisha masharti haya au kufuta na kuweka masharti mengine badala yake au kusisitiza au kubadilisha matumizi ya masharti hayo.
Maana yake nini?
Ukiapa kulinda katiba unaapa kulinda na kuheshimu kila ibara. Moja ya ibara hizo, ya 98, imelipa ruhusa Bunge kusaili kurekebisha, kufuta kipengele chochote cha katiba kwa kufuata taratibu. Moja ya hatua za taratibu za kufuta vipengele vya Katiba ni kupigiwa kura na Wabunge. Sasa kabla ya kura huwa kuna majadiliano Bungeni. Hivyo, Mbunge anaweza kujadili chochote ikiwemo kutaka kufutwa kwa vipengele vya Katiba, ukiwemo Muungano, bila kuambiwa anavunja Katiba.
Kwa nini?
Kwa sababu, adhama moja kubwa ya Katiba hii ni kuwa imesema hakuna kitu ambacho hakizungumziki, chochote kinaweza kurekebishwa, nini kurekebishwa, kinaweza kufutwa, bila ya kusema mjadala wa kufuta masharti fulani ya Katiba unavunja kiapo cha kulinda Katiba.
Na ndio maana Rais Kikwete aliyekula kiapo cha kwanza cha kulinda Katiba aliruhusiwa na Ibara ya 98 kutangaza kuwa Katiba hii sasa tunakwenda kuifuta. Kwa sababu chochote na lolote kikatiba linaweza kufutika, na Muungano nao, kwa hiyo, unafutika.
Na sidhani kama Muungano uta survive Katiba mpya katika sura uliyo nayo sasa. Thank God Katiba inaruhusu, thank God. Mzee Mwanakijiji si mwanafunzi mbaya sana wa masuala ya kikatiba na kisiasa ya Tanzania, utakuwa umeelewa.