Zanzibar wataka wajitungie mitihani Kidato cha IV

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
1,449
574
WANANCHI mkoani Unguja Kaskazini wametofautiana juu ya suala la elimu katika Muungano kutokana na baadhi kutaka ushirikiano uanzie shule za awali hadi vyuo vikuu, huku wengine wakitaka liondolewe hata kwenye elimu ya juu. Aidha hatua ya wanafunzi wa Zanzibar kufutiwa matokeo na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) imekuwa hoja kuu kwenye mikutano ya kuchangia maoni ya Katiba baada ya asilimia kubwa ya wachangiaji, kutaka mitihani ya kidato cha nne itungwe na kusahihishwa visiwani hapa.

Katika mikutano ya kukusanya maoni ya katiba inayoendelea katika shehia mbalimbali mkoani Unguja Kaskazini, wapo baadhi ya wachangiaji hususan wanafunzi na walimu waliotaka Zanzibar ijiondoe katika ushirikiano kwenye mitihani ya kidato cha nne na elimu ya juu. Mbele ya wajumbe wa tume, walitaka Katiba mpya itamke kwamba Zanzibar iwe na Baraza lake la mitihani na Necta ibaki kuwa ya bara, wakisema imekuwa ikiwahujumu wanafunzi wa visiwani hapa kwa kusahihisha vibaya mitihani yao na kuwafutia matokeo.

Tofauti na msimamo wa kutaka kila upande ujitegemee kielimu, mkazi wa Shehia ya Gamba, Rahma Abdalla Maisara alitaka Katiba itamke pande mbili za Muungano zishirikiane kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu. Hata hivyo, Maisara ambaye ni Mtumishi wa Idara ya Afya Zanzibar, aliungana na wanaotaka utungaji na usahihishaji wa mitihani ushirikishe pande zote za muungano, akisema hatua hiyo itaondoa utata uliopo.

Akikosoa wanaotaka elimu ya juu iondolewe kwenye ushirikiano, mkazi wa Shehia ya Moga, Tano Hamisi Issa alisema ni vyema Zanzibar ikabaki kwenye muungano utakaowawezesha kupata elimu yenye viwango. Elimu ibaki kwenye Muungano. Tunapiga kelele angalia mwalimu ana digrii lakini anachozungumza hakieleweki, alisema Issa ambaye alikuwa akirejea kwenye kauli ya mchangiaji katika moja ya mikutano ambaye licha ya kujitambulisha kuwa ni mwalimu wa sekondari, hakumudu kutoa ufafanuzi wa hoja zake
 
Nadhani lengo lingine ni kupanua ajira kwa wazanzibar na kunufaika zaidi na fedha za muungano (watungaji, wasahihishaji, wachapaji nk)
 
Nadhani lengo lingine ni kupanua ajira kwa wazanzibar na kunufaika zaidi na fedha za muungano (watungaji, wasahihishaji, wachapaji nk)
hujasikia taarifa ya habari leo wameunda wizara ya kilimo sijui ili kuwanufausha wakulima wa zanzibari hivi ile inalimaga kweli sijui kama si ufujaji wa hela tu hapa .
 
hujasikia taarifa ya habari leo wameunda wizara ya kilimo sijui ili kuwanufausha wakulima wa zanzibari hivi ile inalimaga kweli sijui kama si ufujaji wa hela tu hapa .

mkuu nivea

labda itakayoshughulika na majahazi kusafilisha chakula kutoka huku Tanganyika. si wanajuwa hela itatoka jamhuri? Shukrani ya punda mkuu..... Hawana shukrani hata kidogo.
 
mkuu nivea

labda itakayoshughulika na majahazi kusafilisha chakula kutoka huku Tanganyika. si wanajuwa hela itatoka jamhuri? Shukrani ya punda mkuu..... Hawana shukrani hata kidogo.
hivi zanzibari wana kilimo gani kule au ndio hiyo karafuu ,iliki na urojo inaundiwa wizara?
 
Mtihani wa hesabu utaanza hivi,,,

Bismilah rwahiman rwahiim.

1. 1-0= ?(a) 2 (b)1 (c) -1
2. 10 x 0 =? (a) 10 (b) 100 (c) hakuna jibu
 
hivi zanzibari wana kilimo gani kule au ndio hiyo karafuu ,iliki na urojo inaundiwa wizara?

mkuu kwa uelewa wangu mdogo baada ya kuishi mikowa ya mwambao.

- zao la karafuu ndilo peke mashuhuri ninalolifahamu, yawezekana na mengine yakawapo lakini kwa uchache sana.

- Asilimia kubwa ya vyakula hutoka huku tanganyika na majahazi ndio njia kuu za kusafilishia.

hata hivyo watanganyika tunaonekana kuupenda muungano zaid, lakini kule wete, mwanakwerekwe, mkokoton,

kyembesamaki nk hawautaki kabisa hata kuusikia siumewasikia uamusho?

Dhambi ya ubaguzi nikama kula nyama ya mtu, ukisha kuila tu huachi - JK Nyerere.
 
huwa najiuliza tena tukivunja muungano hivi ndio marufuku kutinga mguu kuchukua hivyo vitu?
 
Mtihani wa hesabu utaanza hivi,,,

Bismilah rwahiman rwahiim.

1. 1-0= ?(a) 2 (b)1 (c) -1
2. 10 x 0 =? (a) 10 (b) 100 (c) hakuna jibu

Mkuu

tusiwabeze sana may be they can do better who knows anyway? although a lot of energy need to be poured in.
 
huwa najiuliza tena tukivunja muungano hivi ndio marufuku kutinga mguu kuchukua hivyo vitu?

Hapa mkuu inabidi

1. Kulinda mipaka yetu

2. Mapato mkuu, lazima TRA waboreshe makusanyo

3. Uhamiaji lazima wafanye kontrol kama ilivo Tunduma, kigoma, matema, horohoro nk

4. Kuingia lazima uwe na sababu za msingi na uhamiaji wakihisi tofauti na amani haingii mtu.

5. Labda visa inaweza kusamehewa lakini Pass port itakuwa lazima na kwa mdagani watakaa ili wasilowee kigamboni.

6. Mizigo na chochote kile lazima kwanza tushibe wenyewe ndipo wapate ruhusa kuloadi majahazi kama ilivo mpaka wa namanga kwa wakenya.

7. Wale wote walochukuwa maeneo pale kaliakoo, kigamboni, pagani-tanga nk itabidi tutafute utaratibu wa majahazi ya kuwatosha wao na mizigo yao kuelekea mwembe madafu na nungwi maana watakuwa wakimbizi sio watanganyika ati!

Kwa kifupi tutakuwa na taifa jipya la watanganyika na uzanzibara tutauweka kando.

Huwa najisikia vibaya sana kuona tunatukanwa watanganyika na wakituzushia tunawanyonya sijui kivipi? very bad.
 
Tuwaachie tu watunge mitihani yao wenyewe, hata regulations za usajili wa meli waling'ang'ania waweke zao wakaruhusiwa na matokeo yake tumeyaona!! sasa wameamua kurudi tena kwa kaka yao TZ bara! tuwaachie watunge mitihani yao, watarudi wenyewe kwa bro Tanganyika!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom