Muungano ulipoanzishwa upande wa Bara ndio uliopendekeza na sasa katika mabadiliko ni zamu ya Zanzibar kupendekeza. Ni uungwana kuwa Bara nayo ikubali mabadiliko moja kwa moja kama alivyofanya Karume kwa Nyerere. Usifutuke hiyo ndiyo demokrasia!
MKJJ
Tanzania bara na bunge la muungano halina gutz hizo na mifano iko mingi sana, hakuna mtu wa kusema NO mbele ya zanzibar kwa sasa, kina Werema na Chikawe hawa ni yes bwana ni majina ya vyeo tu hawana kitu chochote, wanafuata wanachoambiwa na bosi wao professional haipo tena, mbaya zaidi anayewaambia naye hajiamini chama kitamvunjikia.
Hivi Watanzania (siku bold Zan kwa makusudi ) hatuwezi ku petition Mwanasheria mkuu wa serikali na waziri wake wa sheria wakajiuzulu kwa jinsi ambavyo wame handle hili suala la Katiba hadi zanzibar wakafanya haya madudu?? siamini kuwa haya yanayotokea hayatokani na ufafanuzi ule usiokwenda shule aliotoa Rais Kikwete wakati akihitimisha msimamo wa Waziri mkuu aliotoa bungeni kuhusu znz kuwa nchi. Viongozi wa sasa wa nchi yetu wamelala na hawafai kabisa.
Kheri kumchagua Dk. Slaa ili hili liwekwe sawasawa.
zanzibar ina mikoa mitano, Unguja ina mikoa mitatu na Pemba ina mikoa miwili...Pemba (kusini) na Pemba (kaskazini) na Unguja (mjini magharibi) na (kusini na kaskazini)Hivi Zanzibar ina majimbo mangapi? Na kila jimbo lina wilaya ngapi? Na kila wilaya ina watu wangapi? Nauliza kwa sababu naona kuna mahali
wanasema rais wa Zanzibar awe na mamlaka ya kuteua Regional Commissioners bila kushauriana na serikali ya Mwungano. Pandora's box is now open.
Wakuu mnapoteza pumzi zenu bure kuhusiana na hawa jamaa zetu. Ndio yale ya mh. Mwinyi kuondoa dira ya Taifa, miiko na maadili ya Viongozi ambazo ndizo nguzo kisha akaendelea kudai hakuliua Azimio la Arusha. Wakati kilichotakiwa kwa ubora zaidi ilikuwa kuua Azimio la Arusha (serikali kumiliki njia za Uchumi) na kubakiza dira ya kitaifa inayowafunga viongozi na wananchi wake ktk miiko na maadili.
Kwa hiyo, msiwe na wasiwasi zaidi kwani nina hakika tumefika mahala njia panda. Wanajua fika kwamba JK ni kiongozi dhaifu na wanajaribu kutingisha kiberiti lakini sasa wamefika mahala ambapo watagota. Na ili haya maombi yao yakubalike ni lazima wakubali pia mapendekezo ya bara kama yafuatayo. Tanzania Costitution itafanyiwa mabadiliko waliyopendekeza ikiwa tu:-
1. Zitaundwa serikali za nchi tatu (Zanzibar na Bara) na ile ya Jamhuri (Tanzania) itaongozwa na chama kilichoshinda uchaguzi mkuu pasipo kujali viongozi wake wanatoka upande gani au dini gani. Kila serikali itawakilishwa na wajumbe wake ktk serikali kuu kulingana na idadi ya washindi wawakilishi ktk serikali za nchi husika.
2. Hakuna serikali ya mseto kwa sehemu moja ya nchi isipokuwa vyama vitaweza kuwa na serikali ya mseto ikiwa tu kuna tofauti ya asilimia 10 Kitaifa. Vyama vilivyoshinda ktk serikali mbili watashika madaraka ya nchi hizo chini ya mshindi wa serikali kuu (Taifa).
3. Kuondoa utaratibu wa uchaguzi wa winner takes all - Rais wa nchi atachaguliwa kutokana na ushindi wa chama ktk majimbo mengi (electral vote) kinyume cha Umaarufu wa kiongozi (Popular vote) anayegombea Urais.
4. National Identity ya kila Mtanzania itakuwa Mtanzania hakuna matumizi ya Uzanzibar au Ubara.
Wakiweza kukubali haya tupo tayari kuendelea na Muungano kinyume cha hapo wakubali kwamba Zanzibar huru ni ile iliyofuatia Mapinduzi ya mwaka 1964 hivyo Muungano uliowekwa mwaka 1964 utaenziwa kama ulivyo laa sivyo tuvunje Muungano na kila mmoja wetu ajikate kivyake kama walivyofanya Yugoslavia baada ya kifo cha Tito (Mjamaa).
Wakumbuke tu kwamba Yugoslavia ile exodus ya ku move watu kurudi makwao iliwaku chanzo cha Serbia kuvamia nchi nyingine kudai sehemu ya mipaka ya nchi hizo na tofauti za kiimani (dini) na makabila played a big role ktk kuzigawa nchi hizo kuliko uzawa wa wahusika.
Na inasemekana nchi zote hizo hakuna hata mojawapo imepiga hatua kimaendeleo isipokuwa zote zimerudi nyuma na kukosa nguvu waliyokuwa nayo Yugoslavia. Inasemekana kama Yugoslavia ingebakia vile ktk mfumo huu wa soko huria na Utandawazi pengine ingekuwa Taifa tajiri na lenye nguvu kuliko France...
Kwani sasa hivi tunapata nini kutoka Zanzibar ambacho kesho asubuhi tukikuta wameondoka tutakikosa?
Tanzania Bara inapata nini kutoka Zanzibar?
Well, tell us how much Znz contribute to run the Union government
Why more tha 500,000 znzbarian live in mainland
How much the Tanganyika gov lose through ''free port in znz'' which is a conduit for tax evasion.
Tell us how much tanganyika tax payers money have been used for island payroll.
Tell us who pay 80 MPs in union parliament.
Finally, with 500 billion budget who want to steal from this another Ilala municipal budget.
Hivi huu msururu wa mambo naona kama ni mwiba kwenu kuliko Zanzibar. Kwanza hamna ubavu wa kuilazimisha Zanzibar kufanya chochote wasichopenda wenyewe. Mbona unajifanya kipofu wakati mifano ipo tele. 1995 Mkapa alituma jeshi na kuuwa Pemba na badala yake Salmini na Seif wakafikia muafaka bila ya msaada wenu. Alipoingia Kikwete alitowa ahadi tele za kutatuwa tatizo la Zanzibar na kupoteza fedha nyingi only kuangushwa juhudi zake Dodoma.Na Wazamzibari walipoamua kuafikiana ilikuwa kama mchezo wa kuigiza.
Usidanganyike na udogo wa Zanzibar ukasahau kuwa ni zanzibar inayoifanya Bara ipige chafya! Hebu jiulize hizi harakati za Demokrasia Tanzania zimeanzia wapi kama si Zanzibar walipomdindia Nyerere na yeye kuamuwa kuwafukuza CCM. Usijidanganye hebu fikiria gharama mnazozichukuwa kubembeleza Muungano huu mtaweza kuweka masharti? Unajuwa zanzibar wanahisi hawapotezi kitu ambacho bado hawajapoteza katika mfumo huu wa Muungano ni nyie mnaweka mbele sifa ndio mnaoona kuwa mtapoteza kitu Muungano huu ukivunjika!
Very simple equations my brother
1. No need to contribute because we pirate everything at ports (harbour and airport) as it turns that these are the only source of their income.
2.Are you sure that you talking about Tanganyika? There is not such thing and if it exist it has not reach as far as Zanzibar.
3. As far as we know Taanganyika is not ready to share with Zanzibar aids and grant from abroad (only forced) it will be the eighth wonder if they will pay the payroll through their money
4. Who did ask for the charity? It happens that Tanganyika is very famous of showing off that it ready to let its people to suffer only to make sure they are praised. What is the use of those 80 Mps who do nothing and have no say to the issues prevail in the perliament.Is not the house for Tanganyikaissues? No wonder we are still poor and those we spent our money on9tuliowakomboa) wanatanua!
5.Those 5oo billion include the collections pirated at ports ofwhat you refer as Ilala
Good day my brother!
Ngekewa,
Mkuu wangu wewe unazungumza kwa lugha ya Kibaguzi pasipo kuelewa kwamba hapa tunazungumza kama ndugu jamaa na hakika mimi nawapenda sana ndugu zangu/zetu WaZanzibar isipokuwa hukereka mnaposhindwa kuelewa kwamba viongozi wote wa Zanzibar ni wanafiki na washenzi.
Zanzibar na mustakabali wake haunihusu ila nazungumzia mtazamo wangu kutokana na historia ya nchi hiyo hivyo hata siku moja Zanzibar haijawahi na haitawahi kuitoza chafya Bara isipokuwa huruma ya bara ndio inatuponza, tupo kama beach safe guards wenu tu.
Kweli, ni Nyerere ndiye alimwambia Karume kuhusu Muungano kutokana na kwamba waliyachukua Mapinduzi toka kwa kina Abrahman Babu na unajua fika kwamba Wakomunsit walikuwa tayari kumwondoa Karume. Karunew had no option hata kufikiri akili iliganda akijua hafiki popote na unyakuzi wake.
Nenda kazungumze na Nassor Moyo sii alikuwa mshikaji wa marehemu Kassim Hanga akueleze vizuri historia ya Zanzibar. Hawa wote walijiunga na Babu na walikuwa tayari kuiendesha nchi isipokuwa huo Muungano ndio ulowaponza na wakahamishiwa Bara kumpa pumzi Karume.
Kwa hiyo huu muafaka ni kanyanga tu. Ni marudio ya miafaka kibao iliyowahi kutokea zanzibar mwisho wa yote hutoana damu.. Ebu nambie kilichomkimbiza Shamte ASP na kuunda coaliation na ZNP ili kuwashinda ASP ilitokana na kitu gani kama sii unafiki? Hali Karume aliwahi kumfuata Shamte na ZPPP waunde umoja kumshinda DSultan (ZNP) lakini akamtolea nje, ili mradi tu yeye na Sultan wachukue nchi akihahidiwa na kupewa Uwaziri Mkuu. Nasema Uongo?..Na Si ndio anayofanya leo Seif Sharrif au naongopa pia!
Hivyo Shamte aliuza nchi kwa sababu tu yeye kupewa Uwaziri mkuu ktk serikali ya Kutawaliwa tena na Sultan, na haikuwa kwa maslahi ya Wanzibar kwani kama sio wao kujiengua ASP kulikuwa hakuna nafasi ya Sulatn (ZNP) kushinda uchaguzi wowote Zanzibar. Na ndio maana unaona sifa sana kuzungumzia nywele ndefu kama ni tuzo fulani vile.
Tuache huko, Baada ya Mapinduzi Karume kamfanya nini Abrahman Babu, na hata hao kina Hanga waliokuwa chama baada tu ya Ushindi. Kawageuka na kuwa maadui zake tena kwa ushenzi mkubwa alipokufa Karume unakumbuka jinsi mlivyowaua watu wasiokuwa na hatia kabisa. Zanzibar na Pemba kulikalika au umesahau mkuu wangu! Jiulize ni kwa nini Zanzibar hawamtaki Babu hadi siku anaingizwa kaburini na kina Salim ndio wanazeeka pasipo kukubalika tena Zanzibar. Yaani viongozi wamejaa chuki na roho za kikorosho sijapata kuona.
Kwa hiyo, Salama ya Zanzibar ipo mikononi mwa Bara na hakika kila mnapotaka kufanyiza ndipo hudai sana mamlaka fulani lakini ndani ya roho za vioongozi wenu wana nia mbaya sana. Nina hakika JK akikubaliana na matakwa kama haya ipo siku mtakuja jutia na hakika kusingizia kwamba ni JK aliyesababisha hali mnasahau kwamba kwa kila ovu na matukio ya mauaji Zanzibar hupangwa na hao hao viongozi wenu. Nitakujulisha tena kwamba ni Seif Hamad Huyu huyu aliyewatonya bara kuhusu dhamira ya Aboud Jumbe kuuvunja Muungano. Sasa kama sii unafiki hivi ni vitu gani?
Mkuu wangu nawajua sana kwa ukaribu.. Unafiki ndio mila ya Wazanzibar, atakuchekea usoni huku akikuimbia Taarabu inayokuvua nguo wewe, mkeo na familia yako yote na hata siku moja hapatakuwepo na mahusiano mazuri kati ya Waunguja na WaPemba kwani kila mmoja wenu anajua zaidi wakati hajui kwamba hamjui mwenzake hajui asichokijua!
Umesema sahihi kabisa but nikuulize kwani serikali si ina taratibu zake? wamejaribu wakashindwa? Mie nadhani maneno haya tuyaseme mimi na wewe baada ya kuwa wmaeshalikoroga kwanini sasa hivi ni kama kumpigia mbuzi gitaa hakuna anayekusikiliza viongozi wa zanzibar wote mategemeo yao ni kushika uongozi zanzibar na kufisadi rasilimali za zanzibar basi hamna jengine (njaa zinawasumbua)
Hivi kwa nini mnapenda mno kung'ang'ania lugha ya wenyewe wakati hamuiwezi? Kweli mnataka Tanganyika wagawane nanyi aids? Baki na kiswahili unachokiweza. There is no shame in it. Au ulitumia Google kukutafsiria?
Amandla.......
Mkuu hapa umekosea sana kwa sababu Wazanzibar hawajioni kuwa karibu na Sultan ila inapofikia utani na Bara. Hawa ni watani wetu yaani inapofikia maswala ya rangi wao sii waafrika (ktk Utani) na pia bara ni Wakristu na wasiokuwa na ustaarabu. Utani kama huu watu kama sisi tumewazoea na mara nyingi huwasumbua sana wa kuja.Aaa
Viongozi wa Zanzibar sio mafisadi.
Ila kinachowasumbua sana wazanzibari wengi nikujiona wao si weusi. Harafu anayewasumbua sana ni yule mfalme wa Oman Nasikia ni mzanzibari kiasili.
Mdondoaji,Umesema sahihi kabisa but nikuulize kwani serikali si ina taratibu zake? wamejaribu wakashindwa? Mie nadhani maneno haya tuyaseme mimi na wewe baada ya kuwa wmaeshalikoroga kwanini sasa hivi ni kama kumpigia mbuzi gitaa hakuna anayekusikiliza viongozi wa zanzibar wote mategemeo yao ni kushika uongozi zanzibar na kufisadi rasilimali za zanzibar basi hamna jengine (njaa zinawasumbua)
Mkuu hapa umekosea sana kwa sababu Wazanzibar hawajioni kuwa karibu na Sultan ila inapofikia utani na Bara. Hawa ni watani wetu yaani inapofikia maswala ya rangi wao sii waafrika (ktk Utani) na pia bara ni Wakristu na wasiokuwa na ustaarabu. Utani kama huu watu kama sisi tumewazoea na mara nyingi huwasumbua sana wa kuja.
Hii discussion yenu inapoteza mda
Taralila nyingi sana. Kitu cha mhimu hapa ni kufanya Watanganyika nao wangeamka na kufanya ile kitu inayoitwa patisheni ikiwashinikiza WAZANZIBAR waseme bayana wanachokitaka.
Yeye JK sijui ndo alitoka wapiWhat an irresponsible Minister for Justice? shame on you bwana Chikawe! to hell with you Attorney General! You all dont deserve to be our leaders. sijui Kikwete aliwatoa wapi?
Mkuu si wote wenye mawazo kama hayo. Wakina Junius na Ngekewa kweli wanaamini kuwa sisi watu wa bara ni watumwa na wao waungwana. Hawafanyi mzaha hapo. Najua wengi tumeoleana na tunaishi vyema kabisa. Tatizo ni kuwa hao unaotaniana nao wako kimya kuwakemea wenzao wakina Junius na Ngekewa wanapoleta lugha za kibaguzi. Hii ndiyo inayowapa nguvu hawa jamaa kuamini kabisa kuwa mawazo yao ni ya wazanzibari wote. Pengine kweli wanapokuwa wenyewe hata wale tuliooleana wanakuwa na msimamo kama wa wakina Ngekewa na Junius. Kama sivyo, mbona wako kimya mno?
Utafanyaje patisheni ili kumlazimisha mwenzio aeme unachudhani anataka kusema? Heri mfanye nyinyi patisheni ya kuukataa Muungano muone kama watawaunga mkono!
Amandla.....