Zanzibar wametoa wapi pesa za kununua hiki Kifaru?

Zanzibar wametoa wapi pesa za kununua hiki Kifaru?

profkobayashi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
224
Reaction score
71
nimeshangazwa sana kuona kijisiwa cha zanzibar kuwa na kifaru cha kivita kama hiki

Linalonishangaza hapa ni kuwa hali yao kiuchumi ni mbaya sana na kwa kweli kama wanatutegemea sisi kuwalinda kulikuwa na haja gani ya wao kununua kifaru kikubwa kama hiki

27.jpg



michuzi
 
Walikuwa wanaonyesha kuwa vifaa vingi vya kijeshi vipi Zanzibar hivyo bara mpunguze chokochoko; au hujui kuwa kwa katiba mpya ya Zanzibar (ya sasa) Rais wa Zanzibar ni Mkuu wa vikosi maalumu vya jeshi?! sasa kakosea nini kununua kama yeye ndo mkuu wa mambo ya ulinzi visiwani; Wadanganyika bado hajajitambua kuwa nie ni Watanganyika, siku mkijitambua tu...kumekuchwa.!
 
Mkuu, hicho kifaru ni cha Tanganyika hicho. Tumewaazima tu warembeshe hiyo shoo yao. Si unawajua kwa vya bure hao🙂 Wiki hii hii kinatiwa kwenye meli kurudishwa storage Lugalo.
Watu wenyewe si umeona kuwa wameshaanza kulalama kuwa hawana hata pesa ya kuchangia serikali ijayo ya muungano baada ya muundo wa Katiba mpya hapo 2015 tena kwa mtindo waliokuwa wakiutaka wenyewe kuwa mambo yawe ("pasu kwa pasu" 50-50).
 
comments za kichuki chuki !!! chuki hii inatokana na nini hasa dhidi ya wazanzibar?? kama mnaona mzigo kwenu,, kama mnaona hawana kitu,,, kama mnaona ni mbumbumbu sasa mnawag´ag´ania wa nini,, acheni ubaguzi kuna yenu mlo yaficha vifuani mwenu!!!??
 
Wale komandoos uliona kofia zao?
Zilikuwa na nembo ya mwenge alama ya jwtz na sio smz.
 
Huyu naye anajiita great thinker!!!! Hajui hata mambo ya Muungano!!

Mwishowe atauliza Zanzibar imetoa wapi hao wanajeshi waliokuwa wanafanya maonyesho yao siku ya mapinduzi day.Katiba tuliyo nayo kwa sasa inasema maswala ya ulinzi yako kwenye muungano,hivyo vifaa vingi na wanajeshi wanakaa bongo na wengine walitokea vikosi vya jeshi Tz bara.
 
Jeshi ni swala la muungano jamani...kweli watu wengine mnaitaji kuelimishwa kuhusu huu muungano.
 
Back
Top Bottom