Zanzibar Wamedhihirisha kuwa ni Nchi

Zanzibar Wamedhihirisha kuwa ni Nchi

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,949
Mara nyingi katika mijadala mbalimbali, Watanganyika wamekuwa wakiwabeza Wazanzibari. Lakini kwa mtazamo sahihi Wazanzibari wameonesha wana ukomavu na uzalendo kuliko sisi Watanganyika.

Uzalendo kwanza hupimwa katika umoja wa kuetetea utaifa na kujivunia utaifa wako. Wazanzibari katika hilo, kwa kiwango kikubwa wameweza kulionesha. Tunajua utofauti wa kiitikadi, kimaeneo na kiasilia uliopo Zanzibar. Wazanzibari kiitikadi wamegawanyika hasa kwa misingi ya vyama viwili, CUF na CCM. Kimaneneo wamegawanyika kwa kufuata kisiwa cha Unguja na Pemba, na kiasilia ni kati ya wale waafrika wa asili ya bara na asili ya kiarabu.

Wazanzibari wana tofauti hizi kubwa wakiwa ndani ya nchi yao, lakini watokapo nje, katika kutetea utaifa, uhuru na kutambulika kwa Zanzibar, wanasahau tofauti zao, na kwa kiwango kikubwa wanasimama pamoja. CCM imejitahidi sana kuvunja Umoja wa Wazanzibari lakini hawajaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa. Wameweza kufanikiwa kwa lile tabaka la kufaidika, tabaka linalotawala Zanzibar ambalo linapewa madaraka hayo Dodoma. Lakini kwa kiwango kikubwa Wazanzibari wa kawaida wameendelea kusimama pamoja kudai maslahi na uhuru zaidi wa Zanzibar. Kwa ujumla haki hiyo Wazanzibari wanayo maana mwungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kiasi kikubwa ulikuwa ni mwungano shirikishi katika mambo saba tu, na yaliyo mengi yalibakia kuwa chini ya mamlaka ya Zanzibar, na katika hayo ni lazima wawe na uhuru kamili.

Watanganyika, pamoja na kujigamba kote, kuwa sisi ni wasomi, tuna ardhi kubwa na watu wengi, tuna rasilimali nyingi, lakini tumeendelea kuwa ni jamii iliyoparanganyika na isiyoweza kusimama pamoja kutetea na kulinda utaifa wetu. Mambo yetu mengi yamefanyika kinafiki. Laiti kama, kwa jinsi Tanganyika ilivyo, tungeweza kuwa na uzalendo hata wa robo ya ule wa Wazanzibari, tusingeweza kuchezewa na huu uongozi dhalili wa CCM. Wanatuchezea kwa vile wanajua hatuna umoja, hatuna uzalendo wala vipaumbele. CCM wanajua pia Watanganyika walivyo waoga, wabinafsi, watu wa kujipendekeza na watu wenye tamaa ndogo ndogo kama za kugawiwa vitenge, chumvi, ubwabwa, sukari, ukuu wa wilaya, ukuu wa mikoa, ujumbe wa tume na bodi, n.k.

Ili Taifa liweze kusonga mbele ni muhimu sana kuwa rasilimali iliyokuwa kubwa kuliko zote ambayo ni rasilimali watu. Rasilimali watu inayozungumziwa hapa ni watu wenye uwezo kiakili, kielimu, kiujuzi, watu wenye uzalendo, watu wenye kujitambua na wenye dhamira ya kujitoa kwaajili ya jamii yao. Watu wa namna hiyo, Tanganyika ni wachache mno. Ukiwa na watu wengi wala rushwa, waoga, wasio na umoja, wanaohongeka kiurahisi kwa kanga na chumvi, watu hao siyo rasilimali bali ni janga/burden. Watanganyika tuna watu wengi ambao siyo rasilimali bali ni majanga.

Kwa hapa tulipo hatuna namna yoyote zaidi ya kuwapigia magoti Wazanzibari, wakazane ili tuweze kuwa na mwungano wenye tija kuliko mwungano huu ambao hauna principles za kuungana. Dhamira yetu iwe ni kujenga mwungano imara lakini mwungano unaoelezeka, siyo huu uliokaa kiujanjaujanja. Tuwe na mwungano unaoeleweka kwa kila mtu, unaoeleweka wazi misingi na mipaka ya kuungana kwetu. Watanganyika tujifunze uzalendo kutoka kwa Wazanzibari.

Ndugu zetu Wazanzibari, tusaidieni katika kufikia mwungano wenye mantiki na maslahi yanayoeleweka kila upande, sisi huku Tanganyika watu wetu walio wengi wapo miaka 20 nyuma katika kuuelewa uzalendo. Wengi wa watu wetu wameharibiwa na rushwa dhalili kabisa za kupewa kanga, chumvi na sukari; na baadhi ni waoga kupindukia wa kukosa kupitishwa na chama chao katika kuupata ubunge, au kudondoshewa ukuu wa wilaya au ujumbe wa bodi, kama wakithubutu kutumia akili na utashi wao. Wameamua kujitoa ufahamu, wakamwacha Kikwete, Kinana na Nape wafikiri badala yao.
 
Wazanzibar ndo wameshika mpini wa muubgano kwa sababu wao wanaumoja wao tena ambao uko imara kabisa
 
Huo ni ukweli mchungu kabisa ss mitanganyika hata hio elimu tunayosema tunayo me nakataa kabisa hatuna elimu ss kabisaaaaa
 
Watanganyika wana vyeti vya kutambia tu kama vile kwenye mchezo wa karata.Na kiukweli wameyafanya maisha yetu kama mchezo tu wa karata sasa unadhani kitu gani makini watafanya kubadisha style yao?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wazanzibar ndo wameshika mpini wa muubgano kwa sababu wao wanaumoja wao tena ambao uko imara kabisa

Siku zote wanaotawaliwa huwa wana Umoja sana.Hata Tanganyika wakati tunatawaliwa na Uingereza tulikuwa na Umoja sana.
 
Tanganyika ni unafiki uliopitiliza ndiyo maana hatutaki kuelewa mambo muhimu ya msingi likiwemo la Muungano na faida zake, ukweli ni kwamba huu muungano wa sasa hauna tija kwa watanganyika...kunahitajika serikali tatu au moja zaidi ya hapo ni change la macho
 
Mara nyingi katika mijadala mbalimbali, Watanganyika wamekuwa wakiwabeza Wazanzibari. Lakini kwa mtazamo sahihi Wazanzibari wameonesha wana ukomavu na uzalendo kuliko sisi Watanganyika.

Uzalendo kwanza hupimwa katika umoja wa kuetetea utaifa na kujivunia utaifa wako. Wazanzibari katika hilo, kwa kiwango kikubwa wameweza kulionesha. Tunajua utofauti wa kiitikadi, kimaeneo na kiasilia uliopo Zanzibar. Wazanzibari kiitikadi wamegawanyika hasa kwa misingi ya vyama viwili, CUF na CCM. Kimaneneo wamegawanyika kwa kufuata kisiwa cha Unguja na Pemba, na kiasilia ni kati ya wale waafrika wa asili ya bara na asili ya kiarabu.

Wazanzibari wana tofauti hizi kubwa wakiwa ndani ya nchi yao, lakini watokapo nje, katika kutetea utaifa, uhuru na kutambulika kwa Zanzibar, wanasahau tofauti zao, na kwa kiwango kikubwa wanasimama pamoja. CCM imejitahidi sana kuvunja Umoja wa Wazanzibari lakini hawajaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa. Wameweza kufanikiwa kwa lile tabaka la kufaidika, tabaka linalotawala Zanzibar ambalo linapewa madaraka hayo Dodoma. Lakini kwa kiwango kikubwa Wazanzibari wa kawaida wameendelea kusimama pamoja kudai maslahi na uhuru zaidi wa Zanzibar. Kwa ujumla haki hiyo Wazanzibari wanayo maana mwungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kiasi kikubwa ulikuwa ni mwungano shirikishi katika mambo saba tu, na yaliyo mengi yalibakia kuwa chini ya mamlaka ya Zanzibar, na katika hayo ni lazima wawe na uhuru kamili.

Watanganyika, pamoja na kujigamba kote, kuwa sisi ni wasomi, tuna ardhi kubwa na watu wengi, tuna rasilimali nyingi, lakini tumeendelea kuwa ni jamii iliyoparanganyika na isiyoweza kusimama pamoja kutetea na kulinda utaifa wetu. Mambo yetu mengi yamefanyika kinafiki. Laiti kama, kwa jinsi Tanganyika ilivyo, tungeweza kuwa na uzalendo hata wa robo ya ule wa Wazanzibari, tusingeweza kuchezewa na huu uongozi dhalili wa CCM. Wanatuchezea kwa vile wanajua hatuna umoja, hatuna uzalendo wala vipaumbele. CCM wanajua pia Watanganyika walivyo waoga, wabinafsi, watu wa kujipendekeza na watu wenye tamaa ndogo ndogo kama za kugawiwa vitenge, chumvi, ubwabwa, sukari, ukuu wa wilaya, ukuu wa mikoa, ujumbe wa tume na bodi, n.k.

Ili Taifa liweze kusonga mbele ni muhimu sana kuwa rasilimali iliyokuwa kubwa kuliko zote ambayo ni rasilimali watu. Rasilimali watu inayozungumziwa hapa ni watu wenye uwezo kiakili, kielimu, kiujuzi, watu wenye uzalendo, watu wenye kujitambua na wenye dhamira ya kujitoa kwaajili ya jamii yao. Watu wa namna hiyo, Tanganyika ni wachache mno. Ukiwa na watu wengi wala rushwa, waoga, wasio na umoja, wanaohongeka kiurahisi kwa kanga na chumvi, watu hao siyo rasilimali bali ni janga/burden. Watanganyika tuna watu wengi ambao siyo rasilimali bali ni majanga.

Kwa hapa tulipo hatuna namna yoyote zaidi ya kuwapigia magoti Wazanzibari, wakazane ili tuweze kuwa na mwungano wenye tija kuliko mwungano huu ambao hauna principles za kuungana. Dhamira yetu iwe ni kujenga mwungano imara lakini mwungano unaoelezeka, siyo huu uliokaa kiujanjaujanja. Tuwe na mwungano unaoeleweka kwa kila mtu, unaoeleweka wazi misingi na mipaka ya kuungana kwetu. Watanganyika tujifunze uzalendo kutoka kwa Wazanzibari.

Ndugu zetu Wazanzibari, tusaidieni katika kufikia mwungano wenye mantiki na maslahi yanayoeleweka kila upande, sisi huku Tanganyika watu wetu walio wengi wapo miaka 20 nyuma katika kuuelewa uzalendo. Wengi wa watu wetu wameharibiwa na rushwa dhalili kabisa za kupewa kanga, chumvi na sukari; na baadhi ni waoga kupindukia wa kukosa kupitishwa na chama chao katika kuupata ubunge, au kudondoshewa ukuu wa wilaya au ujumbe wa bodi, kama wakithubutu kutumia akili na utashi wao. Wameamua kujitoa ufahamu, wakamwacha Kikwete, Kinana na Nape wafikiri badala yao.

"mkuu unakosea kidogo, kiukweli tena bila utashi wowote sisi wazanzibari tofauti yetu kubwa ipo katika vyama na si jambo jengine. sio kidini, kieneo, kikabila n.k kama ulivyoeleza.

tena hiyo kisiasa ni ile ya kupandikizwa makusudi na ccm, baada ya kuona mbinu zao zote za kututenganisha kwa njia ya kiubaguzi mwengineo hazikufua dafu.

ccm ni chama kilichoundwa na asp + tanu. na hiyo asp ni muundo wa african association + shirazi association, hawa baadhi ya african association ndio wanaotuletea bughdha hadi hii leo. nasema baadhi sio wote.

tumeunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa nia ya kuondosha tofauti zetu, ila utagundua kazi wanayoifanya hawa african association ya kutaka kutugawa. sijui kwa faida ya nani.

ni kweli wazanzibari tu wazalendo sana. japo kuwa hatuna mamlaka yetu kamili bado, lakini tumekuwa siku zote tukiuweka uzanzibari wetu kwanza kuliko utanzania.

nafurahi sasa nyinyi watanganyika mnaanza kuuona ukweli wa yale madai yetu ya siku nyingi tuliokuwa tukiyadai hadi kufika kubambikiziwa kila aina ya uoza. sijui 'wadini', 'wachoma moto makanisa', 'wamwagia watu tindikali' na kadhalika. hiyo yote ni kazi ya hao hao african association (baadhi yao) wale wasojitambua wanataka nini.

tunafahamu nchi yetu ilivamiwa 'mavamizi' na nchi kubwa jirani kwa nia ya kuitawala. jemedari akiwa nyerere (ukweli mchungu mwengine huo) lakini akijifanya kuzicheza karata zake vizuri kumtumia shk karume. ndio haya ya leo ukaona hata mkataba wa muungano haupo kumbe (upo uliotengenezwa na kusainiwa na upande mmoja tu - tanganyika).

juu ya kutosoma kwake karume hakuwa tayari kwa hilo. unafahamu kuwa wakati karume anauwawa hakuwa akiongea na nyerere kwa zaidi ya mwaka mmoja? unafahamu kuwa kesi ya mauwaji ya karume hakuingizwa hatiani hata mtuhumiwa mmoja? wazanzibari tuna mengi tunayajua kuhusu historia za nchi hizi mbili zaidi yenu watanganyika. muhimu wakati sasa mtatufahamu. na sio propaganda mlokuwa mkilishwa kwa muda mrefu.

mtaona na kusikia mengi kipindi hiki. na hii yote ni mikakati ya kurejesha heshma za nchi zetu zote mbili. zanzibar na tanganyika. kisha kwa matakwa yetu tutaamua kufata aina ya muungano tuutakao (wa ki dola nakusudia, muungano baina ya watu wa sehemu hizi mbili upo toka dahari hatuwezi kuutenganisha"
 
Tanganyika hawajielewi wapo wapo tu, kelele nyingi ata siasa wenyewe wameanza kujuwa juzi tu, mpaka Zanzibar wakokoreke ndio na wao wanajaribu
 
Wazanzibar wanajua wanachokitaka,watanganyika tupo tupo tu.Uliwahi kuona wapi mtu anakana utaifa wake!!!!!!!!!
 
Huo ni ukweli mchungu kabisa ss mitanganyika hata hio elimu tunayosema tunayo me nakataa kabisa hatuna elimu ss kabisaaaaa

Mkuu, ni kweli watanganyika wana elimu lakini ile ya darasani tu. Hatuna hekima,busara wala maono ya mbali. Vitu hivyo havihitaji elimu ya darasani japo inaweza kusaidia. Tukubali Wazanzibar wametushinda kwa hayo. Tanganyika yetu italetwa na Wazanzibar.

Siku ikija Tanganyika, nitapenda kuwaona hao wanaosema ni waumini wa serikali mbili. Sijui wataweka wapi nyuso zao. Lakini tunajua wanasiasa ni vinyonga wanaobadilika kufuatana na upepo unavyokwenda.

Sikutegemea kama Samwel Sitta angejinasibu kuwa muumini wa serikali mbili baada ya kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la katiba. Hayo angebaki nayo moyoni mwake. Ni makosa yaleyale aliyofanya Kikwete kupigia debe serikali mbili kinyume na rasimu ya katiba. Kazi yake kubwa ilikuwa kuwataka wajumbe kuweka uzalendo mbele katika maamuzi yao sio kuotoa vitisho.
 
Tanganyika ni unafiki uliopitiliza ndiyo maana hatutaki kuelewa mambo muhimu ya msingi likiwemo la Muungano na faida zake, ukweli ni kwamba huu muungano wa sasa hauna tija kwa watanganyika...kunahitajika serikali tatu au moja zaidi ya hapo ni change la macho

Muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar sasa umebakia ni kiini macho tu,Wajanja wachache wamezigeuza Kero za muungano Kuwa Mladi wa kujipatia Pesa kiulaini bila jasho, huku wakijitahidi kuongeza Kero ili Fungu la kumaliza kero za muungano liongezeke na liwe la mda mrefu ,ili kudumisha Ulaji wao wahafanya hila kukwamisha Serikali 1 au 3 Maana zitakuja na muundo mpya na kukwamisha mladi wao wa Miaka 50.
 
Yote inatokana na kushobokea kila la Nyerere, kubalini kuwa Nyerere alifanya makosa na muanze kukataa kudumisha fikra zisizokuwa na maana.

Tanzania itapiga hatua kubwa sana ya maendeleo siku tukiamuwa kabisa kuwachana na fikra za ki Nyerere.
 
Elimu yetu yenye majanga, siumeona Prof. Anafundisha vingine anatoa maoni tofauti !!! Umoja hapo kabisa
 
Tanganyika inapaswa iwadai Zanzibar pesa zake , Maana wamezitumia kinyume na matarajio,Pesa ya Tanganyika hupelekwa Zenji kwa makusudio ya kuimarisha huduma za jamii na mishahara ya watumishi tu, lakini Zenji kazitumia hizo pesa kuvunja Katiba kufanya atakavyo na pesa zingine kumezwa na wajanja bila maelezo ya kiina. Ni wakati Watanganyika wazidai Pesa zao zinazotumika kuubembeleza muungano zirejeshwe zije kuinua Uchumi wa Tanganyika Maana Pesa imetumika nyingi sana na Kero hazimaliziki na Hakuna dalili ya kero kuyeyuka hadi ije Serikali Moja au 3.
 
Mara nyingi katika mijadala mbalimbali, Watanganyika wamekuwa wakiwabeza Wazanzibari. Lakini kwa mtazamo sahihi Wazanzibari wameonesha wana ukomavu na uzalendo kuliko sisi Watanganyika.

Uzalendo kwanza hupimwa katika umoja wa kuetetea utaifa na kujivunia utaifa wako. Wazanzibari katika hilo, kwa kiwango kikubwa wameweza kulionesha. Tunajua utofauti wa kiitikadi, kimaeneo na kiasilia uliopo Zanzibar. Wazanzibari kiitikadi wamegawanyika hasa kwa misingi ya vyama viwili, CUF na CCM. Kimaneneo wamegawanyika kwa kufuata kisiwa cha Unguja na Pemba, na kiasilia ni kati ya wale waafrika wa asili ya bara na asili ya kiarabu.

Wazanzibari wanatakiwa waushukuru sana Muungano ndio unaowaweka pamoja! Nje ya Muungano utakuwa kuna Wapemba, Waunguja, Wazanzibara, Waarabu, nk! Hayo yatakuwa ndio matunda machungu ya ubaguzi!!
 
Yote inatokana na kushobokea kila la Nyerere, kubalini kuwa Nyerere alifanya makosa na muanze kukataa kudumisha fikra zisizokuwa na maana.

Tanzania itapiga hatua kubwa sana ya maendeleo siku tukiamuwa kabisa kuwachana na fikra za ki Nyerere.
Tambua Nyerere alikuwa akifanya mambo kipindi cha Mfumo wa Chama kimoja,na Hakuna Sehemu Nyerere alikataza watu kwenda na wakati, ya Enzi za Nyerere yatabakia yalivyo na sasa inakuja Lugha ya kurekebisha kasoro za zamani ili tuweze Kuwa Digtal , Hakuna haja ya kumlalamikia Nyerere Maana alikuwa akifanya yake kwa wakati huo ambao Nadhani ilifaa Kuwa hivyo , sasa mambo yamebadilika tunaenda na wakati tusifanye mambo kwa kukariri historia tu.
 
Tatizo lako wee Kibibi Kungwi, Nyerere alikataa kukuvulia Pichu............. Ohhhh, hata Warioba aligoma.
Yote inatokana na kushobokea kila la Nyerere, kubalini kuwa Nyerere alifanya makosa na muanze kukataa kudumisha fikra zisizokuwa na maana.

Tanzania itapiga hatua kubwa sana ya maendeleo siku tukiamuwa kabisa kuwachana na fikra za ki Nyerere.
 
Tanganyika inapaswa iwadai Zanzibar pesa zake , Maana wamezitumia kinyume na matarajio,Pesa ya Tanganyika hupelekwa Zenji kwa makusudio ya kuimarisha huduma za jamii na mishahara ya watumishi tu, lakini Zenji kazitumia hizo pesa kuvunja Katiba kufanya atakavyo na pesa zingine kumezwa na wajanja bila maelezo ya kiina. Ni wakati Watanganyika wazidai Pesa zao zinazotumika kuubembeleza muungano zirejeshwe zije kuinua Uchumi wa Tanganyika Maana Pesa imetumika nyingi sana na Kero hazimaliziki na Hakuna dalili ya kero kuyeyuka hadi ije Serikali Moja au 3.

Tanganyika ipi hiyo unayoizungumzia? Tanganyika haipo ipo Tanzania(Jamuhuri ya muungano) na Zanzibar, muungano wa ajabu kabisa. Kabla ya yote ile Tanganyika irudi kwanza kisha mengine yafuate. Hii sisiem kwa upande wangu ni kama mkoloni mwingine katika vazi la uzalendo
 
Back
Top Bottom