Zanzibar: Risasi zarindima!

Status
Not open for further replies.

CHIEF MVUNGI

Member
Apr 6, 2012
99
14
Kile kikundi cha UAMSHO kinachodai zanzibar huru kikidai hakitaki muungano sasa hivi kinatawanywa na FFU kwa mabomu ya machozi na risasi baada ya risasi kadhaa kupigwa hewani.

Wapo hapa Kisonge wakitaka kuelekea kituo cha polisi cha MKUNAZINI. Fujo hizi ni baada ya viongozi wao leo kukamatwa baada ya swala ya magharibi na leo walikua na mkutano eneo la Lumumba.
 
Hicho kikundi kikajipange upya sababu mabomu ni noma lakini waendelee kudai muungano haupo mpaka magamba wachie nchi.
 
"Tunajua kuoa, hatujui kuacha, unafikiri ndoa ni lele mama, hakuna talaka hapa", mimi.
 
Jamani hebu huu muungano tuujadili upya kama kamanda Lisu alivyoongea leo,.sasa hayo mabomu ni kulazimisha watu wabaki na muungano wasioutaka?
Our leaders plz be serious otherwise damu ya raia wema itamwagika bila sababu yoyote.
 
Safi sana peleka rumande wote, tatizo si kupewa ZNZ yao hila namna ya upotoshaji wale mashee wanayoleta. Maana wale hata ZNZ ikiachwa kama wanavyodai, ujue wakitoka hapo watasema hawataki secular na uongozi uliopo ZNZ na hapo ndio mabomu ya al-khaeda yatapo ingia safi sana.
 
Kile kikundi cha UAMSHO kinachodai zanzibar huru kikidai hakitaki muungano sasa hivi kinatawanywa na FFU kwa mabomu ya machozi na risasi baada ya risasi kadhaa kupigwa hewani.

Wapo hapa Kisonge wakitaka kuelekea kituo cha polisi cha MKUNAZINI. Fujo hizi ni baada ya viongozi wao leo kukamatwa baada ya swala ya magharibi na leo walikua na mkutano eneo la Lumumba.
Usiupotoshe umma ndugu yangu, wanaokataa muungano huu feki sio kikundi cha uamsho tu, bali ni waZanzibari wengi kwa umoja wetu.

Uamsho na jumuiya za Kiislamu ni viongozi tu waliolivalia njuga suala hili ambalo kwa muda mrefu tukitegemea vyama vya siasa vitufanyie na vimeshindwa.

Kilichotokezea ni kiongozi mmoja wa Jumuiya ya Maimamu ambaye alikuwapo kwenye muhadhara pamoja na maandamano ya amani, alichukuliwa jioni hii toka msikitini na kupelekwa kituo cha polisi cha madema, polisi wakidai kwa ajili ya kumhoji.

Wafuasi akina sisi tulifika kwa wingi na umoja wetu pale kituoni, na maelfu ya watu tulokuwa pale tukitaka nasi sote waujumuishe kwenye hiyo issue, kwa maana ndio tuliofanya maandamano yake bila kusindikizwa na mtu, bali uzalendo na uchungu tu tulionao wa Zanzibar yetu. Hapo ndio polisi wakaamua kututawanya kwa mabomu ya machozi na risasi za moto hewani. Lakini hadi muda huu niandikapo hapa, bado tupo kwa umoja wetu na tunazidi kufurika hapa pahala.

Hatutasita na harakati zetu hadi Zanzibar yetu imerudi mikononi mwetu na siyo koloni la Tanganyika. Wengi wanotwita koloni letu, tumetawaliwa tunakubali kwa sasa, ila muda si mrefu tutajikombowa!!
 
Wadau tuko Mjini Zanzibar. kuna pigwa mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa Uamsho ambao wamezingira kituo cha Polisi Madema kushinikiza viongozi wao waachiwe huru.
We will be back after short break
 
Safi sana peleka rumande wote, tatizo si kupewa ZNZ yao hila namna ya upotoshaji wale mashee wanayoleta. Maana wale hata ZNZ ikiachwa kama wanavyodai, ujue wakitoka hapo watasema hawataki secular na uongozi uliopo ZNZ na hapo ndio mabomu ya al-khaeda yatapo ingia safi sana.

"naam wacha watupeleke rumande sote tupo tayari, kama baadae itakuja al qaeda au nini hiyo ni juu yetu, halikuhusu"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom