Zanzibar na ufisadi wa kutisha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar na ufisadi wa kutisha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NasDaz, May 11, 2012.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Vihelehele wanaofurahia kuona serikaliinafanya vibaya kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa bila shaka walifunguathread hii huku wakiwa na shauku kubwa ya kuona kimenuka nini huko ZNZ!! Wenyemapenzi ya kweli na nchi yetu katu hatuwezi kufurahia kuona serikali ikifanyavibaya ili tu nasi tupate nafasi ya kutawala! Wenye mapenzi na nchi yetuhatujali ni nani anashika hatamu za uongozi wa nchi hii bali bali yeyote yuleatatoa mustakabali bora wa taifa na watu wake! Iwe inaongozwa na CCM, CHADEMA,CUF, NCCR, TLP or chama chochote; hatujali. Na hata kama pangekuwa na uwezekanowa kuwepo kwa Management and Governance Contract kiasi kwambatukaongozwa/kutawaliwa na uongozi kutoka nje; we don't care provided uongozi huoutatufikisha kule ambako kila Mtanzania angependa tuwe! Ya nini basi kuendeleakuongozwa na Mtanzania ikiwa amesha-prove failure tangu uwepo wa dunia?!Hatujashindwa tangu baada ya uhuru bali tulishashindwa tangu mwanadamualipoanza kuwepo duniani! Industrial Revolution iliyokuwa imetokea Europe karneya 17, ni status ambayo hadi leo hii Afrika hatujaifikia! Revolution hiyo ilitokea kwa wenzetu wakati Afrikatukiwa bado tunavaa magome ya miti…..na ndio maana nasema tulishindwa tanguhapo!!

  Sasa turudi kwenye mada "Zanzibarna Ufisadi wa Kutisha!" Hapa ninachojaribu kufanya ni kuulizia STATUS yaufisadi Zanzibar. Lazima tu nikiri kwamba bado sijapata kusikia ufisadi wakutisha kutoka kisiwani humo. Je, ni kwamba ufisadi haujaota mizizi kwa kiasikikubwa kama ilivyo bara au tu tunashindwa kupata taarifa sahii?! Sijapatakusikia hata wakati CCM na CUF walipokuwa na uhasama mkubwa wa kisiasa. Kilauchao kashfa kubwa za ufisadi zinatokea Bara!!! Kama tunaweza kudhihirishiwakwamba angalau Zanzibar ni waadilifu katika suala zima la ufisadi, je, panaubaya wowote wa kuwaachia wizara nyeti waziongoze?! Kama nilivyotangulia kusemahapo awali, mtu kama mimi sijali nani anaongoza ili mradi tu awe na uwezo wakulisongesha mbele taifa hili.
  NAWAKILISHA!
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,768
  Likes Received: 6,098
  Trophy Points: 280
  Hivi bajeti ya mwaka ya taifa la Zanzibar ni dola ngapi vile? Cha kufisidi kiko wapi? Magunia mawili matatu ya karafuu ambayo ndio uchumi wa Zanzibar au? Hicho cha kufanyia "ufisadi wa kutisha" hakipo and thats the reason.
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  NasDaz,
  Nakubaliana na wewe kabisa kwenye hoja ya Taifa kwanza halafu mambo mengine baadae. Pia naunga mkono hoja ya kuwapa watu wenye uwezo wa kutusogeza mbele wakati huo huo wakawa na roho ya kuridhika bila kujiingiza katika wizi na ufisadi unaotisha.
  Isipokuwa mtu atokee upande gani wa muungano sioni kama ni tatizo zaidi ya siasa zilizopo maana wapo wazanzibar pia ndani ya serikali ya jamuhuri.
  la muhimu pengine ni kufanyia kazi utaratibu wa adhabu na kwa staili gani, watu wenye kuchezea mali za umma wapewe ili kudhibiti tabia hizo kutoka kwenye chama chochote kile kitakachotawala.
  Pengine katiba inayokuja iingize vipengele kama hivyo ili kuongoza nchi isiwe kigezo cha wachache kuiibia nchi
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 4,014
  Trophy Points: 280
  vile vyakula vibovu vinavyoingizwa zanzibar kila mwezi si ufisadi huo ama?
   
 5. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,182
  Likes Received: 10,531
  Trophy Points: 280
  Hivi Wazanzibar mmefikia wapi na ile ishu yenu ya kujitenge naona mmepooza kweli.
   
 6. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sio kwamba Zanzibar hakuna ufisadi, hapana nakataa. Ufisadi upo, ila kilichopo Zanzibar saiv ni utawala ambao hauruhusu uhuru wa vyombo vya habari, ni kama alivyokuwa Mkapa madarakani. Je, kipindi cha mkapa ulikuwa unasikia habari za ufisadi? Jibu ni hapana, lakjini je, ni kweli ufisadi haukuwepo? hapana, zaidi ya nusu ya ufisadi ulioibuliwa kipindi cha JK ulifanyika kipindi cha mkapa, so sio kweli kwama ZNZ hakuna ufisadi, vuta muda utayasikia tu pale mfumo wake wa utawala utakavyokuwa wa wazi kama wa JK.
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Hata mi sijawahi kusikia ufisadi visiwani. Waibe wapeleke wapi? Wanaridhika tu na kilichopo
   
 8. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Nilitaka nishangae, we wachamungu wanakuwaga wezi?
   
 9. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Rais wa Jamhuri ya muungano awamu ya pili si alitoka Zanzibar?Je uadilifu wake katika suala la ufisadi ulikuwaje,au alikuwa hana doa...???
   
 10. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  Wazanzibar ni vipofu,hawajui kuhoji maendeleo!kusamehewa 50bn na tanesco sio ufisadi?zec haikukusanya bili?
   
 11. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Sizani kama hiyo ni hoja, huku bara hata kwenye serikali za vitongoji, kuna ufisadi!
   
 12. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Hiyo peke yake hatuwezi kuita ufisadi !! Kwani leo hii nikikupa huduma kwa maana kesho unilipe lakini ukashindwa kulipa nami nikaamua kukusamehe ni ufisadi?!
   
 13. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unakubali JK ni RAIS NAMBARI WANI wa TZ. bila yeye kuruhusu yote hay na hata haya ya report ya CAG juzi tungejua? pongezi zake Rais JK.
   
 14. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Ndahani,
  Nakubaliana na wewe kwa 100% na ndio maana hata mimi kwenye maandiko yangu mara kwa mara nimekuwa nikizungumzia suala hilo. Binafsi, naamini maadili TZ yamemomonyoka kwa kiasi cha kutisha na na ndio maana mara zote nimekuwa nikipendekeza pawepo na Approved Dictatorship Governance ambayo itakuwa ni matokeo ya Dictactorship Constitution ambayo italenga kuwarudisha Watanzania kwenye mstari wa maadili. Sio uongozi wa kidikteta bali katiba ya kidikteta.
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  How will we develop the nation if we entertain the the bad habit of people not footing their bills?
   
 16. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  uandishi huu wa heading hizi unafaa kuuzia magazeti ya aina fulani fulani..

  Lakini kwenye kadamnasi ya watu tunaoheshimiana na kujali muda sidhani kama ni fair kumfanya mtu asome paragraph mbili kumbe kile ulichokiahidi hakipo.., nadhani ungeweza kufikisha ujumbe kwa uwazi na ufupi pia...
   
 17. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Mie sijasema Zanzibarhakuna ufisadi, nimeuliza, hivi ZNZ hamna ufisadi? Nimeuliza kwavile bado sijapata kusikia kashfa nyingi za ufisadi serikalini kama ilivyo huku bara. Madai kwamba hakuna uhuru wa vyombo habari sikubaliani na wewe. Kwani haya magazeti ya bara hayawezi kuandika taarifa za znz?! Gazeti gani bara liliandika kuhusu ufisadi (narudia, UFISADI kwa maana ya corruption) wa znz halafu likafungiwa?!

  Nakubaliana na wewe kwamba zaidi ya nusu ya ufisadi ulioibuliwa wakati wa JK ulitokea wakati wa Mkapa. Hata hivyo, watu tunafahamu hata wakati huo ulikuwa unazungumzwa ingawaje sio kwa uhuru kama ilivyo sasa! Tofauti kubwa iliyopo ni kwamba Mkapa alikuwa anakuja juu kama moto wa kifuu pale taarifa za ufisadi dhidi ya serikali yake zinapoandikwa lakini JK anawaacha waaandishi waandike wanavyojisikia. Sasa inakuwaje magazeti ya bara yashindwe kuandika kuhusu ufisadi wa znz na tusikie kwamba yamefungiwa?! Nakubali Dr. Salmin alikuwa mtemi na angeweza kufanya chochote dhidi ya magazeti...na alishawahi kulipiga marufuku Mtanzania kutotia mguu znz! Sasa tujiulize, hivi kweli Karume alikuwa dikteta kiasi hicho?! Hivi kweli Dr. Shein ni dikteta kiasi hicho?! Hivi kweli jembe kama Juma Duni Haji (yule wa CUF b4 muafakana sio huyu wa sasa ambae ni waziri wa afya) aone ufisadi ataacha kusema kisa anamuogopa rais?! Let's be honesty at least for this.
   
 18. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu,
  usitake kuniambia kwamba na wewe ulitarajia kukuta taarifa za kutokea ufisadi wa kutisha huko znz!!! Kwani zinakufurahisha taarifa za kushamiri kwa ufisadi?! Na kama ulitarajia ni taarifa za ufisadi na kukuta kumbe sivhyo, uungwana si ingekuwa kushukuru na kusema "thanx god, kumbe si kwamba kumetokea ufusadi!"
   
 19. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  We can not, we can not at all!
   
 20. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Kwavile ufisadi una maana pana sana, nakiri kushindwa kukusanya bili nako ni ufisadi especially kama zec ipo commercial oriented! Hata hivyo, let's try to sticky in political/grand corruption
   
Loading...