ZANZIBAR: Mabalozi, Dkt. Wilbroad Slaa na Muhidin Mboweto wafika Ikulu kujitambulisha na kumuaga Rais Dk. Shein

Slaa: Nikiwa rais namuweka Magufuli ndani kwa kuuza nyumba za serikali.

Slaa: Nchi haitatawalika

"Nakushukuru sana mheshimiwa rais kwa kuniamini na kuniteua kuwa miongoni mwa wasaidizi wako katika kuendeleza Tanzania ya viwanda. Naahidi kuwa nitafanya kazi kwa maarifa yangu yote na uwezo wangu wote" Slaa
Kama mlitaka amfunge Magufuli mngemteua agombee ila kwa vile mlipenda pesa kuliko maono, mwacheni naye afaidi matunda ya vita ya ufisadi aliyopigana kwa zaidi ya miaka 20!
 
24f357ffac77fe51ea746af97b751d58.jpg
f26db85dd52d9b90ec16a6080f03d741.jpg
3088cfd78e77c919ce0879832c77db06.jpg
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kwa Mabalozi wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Sweden na Nigeria kutilia mkazo Sera ya Diplomasia ya Uchumi ili Tanzania iweze kutekeleza malengo iliyojiwekea katika kuimarisha uchumi wake.

Dk. Shein aliyasema hayo Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipofanya mazungumzo na Mabalozi wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi hizo, waliofika Ikulu kumuaga Rais pamoja kujitambulisha na hatimaye kufanya mazungumzo.

Mabalozi hao ni balozi Wilbroad Peter Slaa, balozi wa Tanzania nchini Sweden na balozi Muhidin Ally Mboweto, balozi wa Tanzania nchini Nigeria.

Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa shabaha kuu ya serikali zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuimarisha sekta za kiuchumi na huduma za jamii ikiwemo sekta ya viwanda, utalii, uvuvi pamoja na elimu na utamaduni.

Dk. Shein alieleza kuwa Serikali zote mbili zimedhamiria kutekeleza Diplomasia ya uchumi katika kuhamasisha uwekezaji hasa katika sekta ya viwanda kwani ndio kiu ya uchumi wa Tanzania hivi sasa.

Akizungumza kwa upande wa Zanzibar, Dk Shein alisema kuwa licha ya Zanzibar kuwa ni visiwa ambavyo vimezungukwa na bahari sambamba na kuwa na azma ya kutekeleza uchumi wa bahari lakini bado hakuna viwanda vya samaki au viwanda vyenye kutumia rasilimali za bahari.

Hivyo, Dk Shein alitumia fursa hiyo kuwaeleza mabalozi hao kuwa Zanzibar inawakaribisha wawakezaji kutoka Sweden na Nigeria kuja kuwekeza katika viwanda vya samaki.

Sambamba na hayo Dk Shein aliwatakia heri na fanaka mabalozi hao katika utendaji wao wa kazi kwenye balozi hizo na kuwaahidi kuwa ataendelea kutoa ushirikano wake kwa mabalozi hao kwa lengo kutekeleza dhamira zao hizo.

Na Mabalozi hao walimthibitishia Dk Shein kuwa wamepokea maelekezo na miongozo yote aliyowapa na kumuahidi kuyafanyia kazi hasa kwa maeneo maalum ya Zanzibar na yale ya Tanzania Bara sambamba na kuimarisha uhusiano na ushirikano kati ya Tanzania na nchi hizo wanazoenda kufanya kazi.
Ni hbr njema nawatakia mabalozi kila kheri katika utekelezaji wa majukumu yao
 
Dr. Slaa ni opportunist flani hivi. Well, kila mtu by nature ana tendency ya umimi. Kila la kheri kwake.
 
haya maajabu kwakweli tangu lini mabalozi wanaenda kuaga Zanzibar naanza kuamini huu uteuzi wa Dr slaa there something behind,halafu huyu Dr slaa hv katoa hata pole au comment yeyote kuhusiana na kifo cha mwanafunz alipigwa risasi na police kweli? sijui kwann mtu akienda ccm anakua katili sana
weee utabishana na kula a.k.a njaa?
24f357ffac77fe51ea746af97b751d58.jpg
f26db85dd52d9b90ec16a6080f03d741.jpg
3088cfd78e77c919ce0879832c77db06.jpg
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kwa Mabalozi wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Sweden na Nigeria kutilia mkazo Sera ya Diplomasia ya Uchumi ili Tanzania iweze kutekeleza malengo iliyojiwekea katika kuimarisha uchumi wake.

Dk. Shein aliyasema hayo Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipofanya mazungumzo na Mabalozi wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi hizo, waliofika Ikulu kumuaga Rais pamoja kujitambulisha na hatimaye kufanya mazungumzo.

Mabalozi hao ni balozi Wilbroad Peter Slaa, balozi wa Tanzania nchini Sweden na balozi Muhidin Ally Mboweto, balozi wa Tanzania nchini Nigeria.

Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa shabaha kuu ya serikali zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuimarisha sekta za kiuchumi na huduma za jamii ikiwemo sekta ya viwanda, utalii, uvuvi pamoja na elimu na utamaduni.

Dk. Shein alieleza kuwa Serikali zote mbili zimedhamiria kutekeleza Diplomasia ya uchumi katika kuhamasisha uwekezaji hasa katika sekta ya viwanda kwani ndio kiu ya uchumi wa Tanzania hivi sasa.

Akizungumza kwa upande wa Zanzibar, Dk Shein alisema kuwa licha ya Zanzibar kuwa ni visiwa ambavyo vimezungukwa na bahari sambamba na kuwa na azma ya kutekeleza uchumi wa bahari lakini bado hakuna viwanda vya samaki au viwanda vyenye kutumia rasilimali za bahari.

Hivyo, Dk Shein alitumia fursa hiyo kuwaeleza mabalozi hao kuwa Zanzibar inawakaribisha wawakezaji kutoka Sweden na Nigeria kuja kuwekeza katika viwanda vya samaki.

Sambamba na hayo Dk Shein aliwatakia heri na fanaka mabalozi hao katika utendaji wao wa kazi kwenye balozi hizo na kuwaahidi kuwa ataendelea kutoa ushirikano wake kwa mabalozi hao kwa lengo kutekeleza dhamira zao hizo.

Na Mabalozi hao walimthibitishia Dk Shein kuwa wamepokea maelekezo na miongozo yote aliyowapa na kumuahidi kuyafanyia kazi hasa kwa maeneo maalum ya Zanzibar na yale ya Tanzania Bara sambamba na kuimarisha uhusiano na ushirikano kati ya Tanzania na nchi hizo wanazoenda kufanya kazi.
 
Siasa bwana eti huyu padri ndio alikuwa anasema wakati wa JK kuwa nchi haitatawalika na akasema akishinda atamweka ndani Magufuli kwa kuuza nyumba za serikali. Kapewa ubalozi sasa ananyenyekea kama mtoto mdogo.
Ndio siasa hizo. Hata Chadema walisema Lowasa ni fisadi na anyemuunga mkono inabidi akapimwe akili, baadaye wakamfanya awe mgombea wao wa urais.
 
natabiri slaa kugombea kupitia ccm baada ya rais magu. au anaweza kuja kuwa makamu wa raisi au waziri mkuu. tunza kumbukumbu hii
 
Back
Top Bottom