Zanzibar: Maalim Seif, Shein kuteta Leo

Zanzibar: Maalim Seif, Shein kuteta Leo

Pistol

Senior Member
Joined
Oct 13, 2015
Posts
194
Reaction score
86
Mazungumzo ya kutafuta muafaka wa mgogoro wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, yataendelea kufanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.

Mazungumzo ya kikao hicho ambacho ni cha tatu, kitaongozwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.Wajumbe wa kikao hicho ni Marais wastaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, Amani Abeid Karume, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Mazungumzo hayo yanasubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), kufuta matokeoi ya Uchaguzi Mkuu visiwani humu Oktoba 28, mwaka huuu na kuibua mgogoro mkubwa wa Kikatiba.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazrui, alisema kuwa hadi sasa mazungumzo hayo bado siri kubwa hata viongozi wa ndani ya chama chake, hawafahamu kinachoendelea tangu viongozi hao wa kitaifa kuanza kukutana.

"Hadi sasa usiri umetawala, sielewi chochote kinachoendelea kama kurejewa kwa uchaguzi au Zec kuendelea kutangaza matokeo, lakini ninachofahamu kuwa kesho (leo), viongozi wakuu watakutana tena kwa mara ya nne Ikulu," alisema Mazrui ambaye pia ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani humu.

Alisema inasikitisha mno vikao vyote vitatu vilivyofanyika pamoja na hicho kinachotarajiwa kufanyika leo, upande mmoja unawakilishwa na watu watano wakati upande mwingine ukiwa na uwakilishi wa Maalim Seif peke yake.

Alisema mashariti yaliyowekwa katika muongozo wa mazungumzo, ni magumu kwa kuwa hakuna mtu mwingine anayeruhusiwa kushiriki katika mazungumzo ya kutafuta muafaka wa uchaguzi wa Zanzibar zaidi ya Maalim Seif pekee.

Hali kadhalika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud, alithibitisha kufanyika kwa kikao hicho, lakini alisema hafahamu kinachoendelea pamoja na bosi wake kuwa mshiriki wa mazungumzo hayo.

"Yawezekana wewe ndugu mwandishi unafahamu zaidi, lakini na mimi pia nimesikia kuwa viongozi wetu watakutana, bahati mbaya sifahamu kinachoendelea,? alisema Waziri Aboud.

Maamuzi ya kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar, yamesababisha Baraza la Wawakilishi kukosa uwakilishi wa wananchi kinyume na Kifungu cha 90(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Kwa mujibu wa kifungu hicho, Baraza la Wawakilishi linatakiwa kuitishwa mkutano wake wa kwanza tangu kuvunjwa Agosti 13, mwaka huu ndani ya siku 90.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, alisema ataendelea kushika wadhifa huo pamoja na Naibu wake bila ya kuwa na wajumbe katika chombo hicho cha kutunga sheria Zanzibar.
Mjadala mkubwa umekuwa ukiendelea katika Manispaa ya Mji wa Zanzibar kuhusu tarehe ya kurudiwa kwa uchaguzi huku CUF wakiendelea kupinga lakini CCM wanaunga mkono uamuzi wa Zec.

CHANZO:Nipashe
 
Nani kuwa mshenga wa kikao...maana naona wajumbe tu.
Kikao kinasimamiwa na UN, EU na Comonwealth

Kuna tetesi zinasema, umoja wa mataifa umetoa kauli kwamba, kuna mambo matatu yamatolewa.
Kurudiwa uchaguzi na kusimamiwa na wao.
Kutangazwa mshindi alie shinda or
Kufutwa kwa vyama vingi

Kesho jibu linatakiwa
 
Mchambuzi wa Kimataifa Ahmed Rajab alisema:
Kuna Siasa za Kistaarabu
Kuna Ustaarabu wa Kisiasa
Kuna Siasa za Kipumbavu
Kuana Upumbavu wa Kisiasa
Kilichotokea Zanzibar ni Upumbavu wa Kisiasa.
Mwaka huu CCM wataisoma siasa ni nini?
 
Wajinga sn ccm kuanzia bara wanaruhusu vyama vingi lkn hawataki kurndesha uchaguzi ulio huru??????
 
Siyapendi mazungumzo ya huyu Maalim Seif, anaitwa na anakwenda kuongea mambo ya msingi yanayohusu wananchi kama vile anaongea na babaake mdogo.

Amekosa Protocol ya kichama wakimaliza kuongea wanamgeuka, anafanya siasa za kizamani washauri wake dhaifu au ni mbishi?

Anafanya vikao na viongozi zaidi ya 4 wa ulibzani wake yeye yuko pekeyake anamaslahi gani kwa kura za waliomchagua?

Nina wacwac na uongozi wa huyu Maalim?
 
Kikao kinasimamiwa na UN, EU na Comonwealth

Kuna tetesi zinasema, umoja wa mataifa umetoa kauli kwamba, kuna mambo matatu yamatolewa.
Kurudiwa uchaguzi na kusimamiwa na wao.
Kutangazwa mshindi alie shinda or
Kufutwa kwa vyama vingi

Kesho jibu linatakiwa

Hujui mikataba ya UN wewe, UN ni sawa na mpiga picha analitegesha kamera akisubiri mtoto aliwe na ndege ili yeye apate picha ilhali alikuwa na uwezo wa kumfukuza yule ndege na kuuokoa maisha ya mtoto.
 
Hata mimi naliona hilo... Utasikia tu.
 
Hii inaitwa MTAKA FITINA HAKOSI SABABU; nyie nipashe hamjui kuwa Zanzibar ina katiba Mpya? Au mmefukunyua hiyo ya mwaka 1984 ili kuhalalisha fitina.
 
Kikao kinasimamiwa na UN, EU na Comonwealth

Kuna tetesi zinasema, umoja wa mataifa umetoa kauli kwamba, kuna mambo matatu yamatolewa.
Kurudiwa uchaguzi na kusimamiwa na wao.
Kutangazwa mshindi alie shinda or
Kufutwa kwa vyama vingi

Kesho jibu linatakiwa

Aisee zote ngumu kumesa kwa waroho wa madaraka maccm.
 
Hujui mikataba ya UN wewe, UN ni sawa na mpiga picha analitegesha kamera akisubiri mtoto aliwe na ndege ili yeye apate picha ilhali alikuwa na uwezo wa kumfukuza yule ndege na kuuokoa maisha ya mtoto.

Baba subiri dawa ikuingie,
Kwani nani walochangia hiyo Bajeti ya Uchaguzi? UNDP?
Nani walisaidia kufunga hiyo mitambo ya kukusanya Matokeo?
UNDP
Leo wamekuwa watoto? Mutaisoma namba na Upumbavu wenu wa Kisiasa, kila mukijizonga ndio munaraksisha kuipatia zanzibar kujitangazia Uhuru
 
Hicho kikao tajwa umesikia kuna mjumbe yeyote kutoka bara..! Zanzibar ni nchi huru na inauwezo kwa kujiamlia mambo yake. Bara ni ndugu anayeweza kushauri kama mwanafamilia ila siyo mwenyefamilia.
 
Iweje CUF iwakilishwe na mtu mmoja t????

Kama ni hivi kwa nini kikao hiki wasingekaa Shein na Maalim Seif peke yao ili kuwe na usawa wa pande zote???

Hapo kuna hofu ya haki kutendeka.

CUF kazeni buti msimamo uleule, "TUNATAKA ATANGAZWE RAIS NA SIYO KURUDIA UCHAGUZI, KWASABABU TUMESHAPIGA KURA"

Hilo la alieshinda atangazwe hata msiliombee,ndo mtakuja kuaminishwa "Umdhaniaye ndiye kumbe siye.:-O:-O:-O
 
Back
Top Bottom