Zanzibar: Kwa nini tunasaili kipengele cha Katiba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar: Kwa nini tunasaili kipengele cha Katiba?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Aug 22, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Magazeti wiki hii yamekuwa yakiandika kuwa mabadiliko ya 10 yaliyofanyika Zanzibar ya kuonyesha kuwa hiyo ni nchi iliyo na uhuru kamili na mipaka yanataka kuanzisha mgogoro wa kikatiba nchini.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Sioni kama kuna mgogoro wa kikatiba, ila waandishi wa habari wanataka kuyafanya tu mabadiliko haya kuwa ndiyo chanzo cha mgogoro wa kikatiba, badala ya kuiona Katiba ya Jamhuri ya Muungano yenyewe kama ndiyo tatizo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Mimi sioni kama kuna tatizo katika maamuzi hayo ya Katiba kama ni tatizo, bali ni kuwa waandishi wa habari wameshindwa kuyajadili mabadiliko haya katika muktadha wake halisi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wiki mbili zilizopita Wanzanzibari walipiga kura kuamua kama waunde serikali ya umoja wa kitaifa au hapana; hatukuona kuwa ule ni uamuzi wenye athari kikatiba; lakini Katiba ya Zanzibar imekuwepo hapo miaka yote hiyo, zaidi ya miongo miwili.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Waandishi hatukujiuliza iweje kama Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano iwe na Katiba yake. Iwe na Rais wake, iwe na wizara zake na bajeti zake. Nadhani waandishi wangejiuliza haya yote wasingeona mabadiliko haya kama ni tishio katika Muungano, bali kuwa mchakato mzima wa kuunda Muungano ndio wenye matatizo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Binafsi ninataka kuwakumbusha waandishi wenzangu kuwa, kabla ya kuundwa kwa Muungano, Zanzibar ilikuwa nchi kamili yenye hadhi ya Jamhuri na ilikuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa tangu Desemba 15, 1963. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Iliingizwa siku moja na Kenya. Kumekuwa na dhana, pengine, kuwa kwa vile uhuru ule wa awali ulikuwa chini ya Waarabu basi haikuifanya Zanzibar kuwa nchi kamili. Sio Kweli, na mapinduzi ya Januari 1964 hayakuiondolea Zanzibar hadhi ya Jamhuri.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]

  Kwa hiyo basi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa ni kati ya nchi mbili zenye hadhi ya kimataifa, na kwa hiyo Muungano huu ni wa Kimataifa. Zanzibar haikuwa mkoa wala haijawahi kuwa mkoa, hata baada ya Muungano.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kilichotokea ni kuwa kwa vile hatukuwa na Katiba ya Jamhuri ya Tanganyika, Katiba ya Tanganyika ikarekebishwa ili kuwa Katiba ya muda kwa matarajio kuwa kwama 1965, Katiba ya Muungano ingetungwa na baraza la wabunge.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Hilo halikufanyika hadi mwaka 1977, miaka mitano baada ya kufariki Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume. Waandishi hatujiulizi, kwa nini Katiba ya Tanganyika ikatoholewa kuwa Katiba ya Muungano? Na Kwa nini Katiba ya Jamhuri haikurudishwa kama wenzetu wa Zanzibar walivyofanya mwaka 1984, kurudisha Katiba yao? Kwa nini Katiba ya Tanganyika iwe ndio hiyo hiyo Katiba ya Muungano? [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Kuna tafsiri nyingi lakini moja la kukumbuka kuwa, katika mambo ya umoja wa kitaifa na muungano wa nchi kumekuwa na tabia ya wanasiasa kudhani kuwa “Umoja”, “Muungano”, na mikondo kama hiyo ya kikanda inaweza kutokomeza hisia za kitaifa na kikabila bila hata kukaa chini na kuongea na wahusika juu ya namna gani utaifa uwe mbele na hisia za ukabila na utaifa ziwekwe kando.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Hili lilijitokeza katika nchi za Kisovieti na kilichotokea baada ya perestroika ni kuwa watu walirudi tena kule kwenye ukabila, umajimbo. Na sisi tulifanya kosa hilohilo. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Muungano haukuanza na mjadala wa namna gani tutaachana na siasa za kimajimbo na kikabila na kidini. Wanasiasa walidhani mifumo hii ya kijamii itakufa yenyewe au ingekufa kwa vile watu wangetambua kuwa Jamhuri ya Muungano ni muhimo kuliko umajimbo. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Na kwa sababu hiyo, wanasiasa wa wakati ule wa kuunga Muungano hawakutaka kuwashirikisha wananchi kuhusu uamuzi huu adhimu. Ndiyo maana Abdul Jumbe alitaka kuliweka hili suala sawa mwaka ule wa kuchafuka kwa hali ya hewa ya kisiasa. Lakini Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na wenzake hawakulichukulia maanani na badala yake wale waliotaka kuujadili Muungano na kuufanyia marekebisho walifanyiwa kebehi au kufukuzwa madarakani.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Haikuwa sahihi. Tulifanya kosa la kutowashirikisha wananchi ambao, kupitia kura ya maoni, mijadala ya kitaifa, na kadhalika, tungeweza kusema aina gani ya Muungano tungeutaka.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa maoni yangu ni kuwa hata uamuzi wa kuutengeneza Muungao nao ulikuwa wa haraka sana. Nchi nyingi za kiafrika wakati ule ndiyo kwanza zilikuwa zinapata uhuru. Wananchi wengi walikuwa hawana ufahamu wa kutosha juu ya serikali katika mfumo wa kimagharibi, tofauti na sasa; na wengi hawakuwa na elimu ya juu kama tulivyo sasa; [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Kilichofanyika ni kuwaburuza tu. Hapo ndipo palikuwa mwanzo wa mgogoro wa kikatiba, kwa sababu wanasiasa wale hawakutafakari kuwa hapo baadaye kizazi kipya kitauangalia muungano huu na mchakato wa kuunda kwa jicho pevu zaidi na kuuliza maswali. Hicho ndicho kinachotokea zaidi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wanasheria watanisaidia hapa! Muungano ulianza na mkataba kati viongozi wawili wa kisiasa- Marais- Karume na Nyerere. Na kwa vile Muungano huu ulikuwa ni kati ya viongozi wa nchi, basi serikali ziliwakilishwa na serikali, sio vyama, ndizo zenye uwezo wa kuamua kuuza uhuru- sovereignty- na kuifanya nchi ikaingia kwenye Muungano. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Angalizo; Kumbukeni tulichokifanya kabla ya kuingia kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki. Maraisi walikubali, lakini walitaka watu wajadili, tukajadili. Baadaye bunge likaidhinisha kwa sheria, na ndipo tukajiunga.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Haiwezekani chama chochote kikajadiliana na chama cha nchi jirani na kuunda Muungano wa nchi bila rais, au bunge na wananchi kuupitisha. Hatukufanya hivyo wakati ule na kila tunapotaka kuwe na mjadala kuna watu wanaweka mguu.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Na kwa sababu mkataba ndio uliotumika kuongoza uundwaji wa Katiba ya Muungano, basi lazima tutambue kuwa sheria mama sio Katiba ya Muungano, tunaozungumzia Muungano. Sheria mama inakuwa Mkataba wa Muungano ambao unaweka bayana nini Tanganyika haki yake; na nini Zanzibar haki yake; na vipengele vile ndivyo tunavyokubali kuvitumia kutengenezea Katiba.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Sasa kama Zanzibar wamekubaliana kufanya serikali ya Umoja wa Kitaifa; na kuianisha Zanzibar vizuri zaidi kiutawala na kijiografia, mgogoro unatoka wapi kwa sababu mkataba wa Muungano, haujaikataza Tanganyika au Zanzibar, kuwa na Katiba zake na kuainisha mipaka ya mamlaka yake kiutawala.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mgogoro ungetokea katika mambo yale ambayo mkataba wa Muungano uliorodhesha kuwa yashughulikiwe na serikali ya Muungano, na ndiyo yakaingizwa katika Katiba ya Muungano, na Zanzibar wakaamua kuyaweka katika katiba yao binafsi kama vile hayakutajwa kuwa mambo ya Muungano. Hakuna Katiba iliyovunjwa kwa maamuzi yaliyofanyika Zanzibar.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Ninahimiza kuwa ili haya mashaka yote yatoweke mambo kadhaa yafanyike. La kwanza ni kuanzisha mjadala wa kitaifa wa marekebisho ya katiba. Kwanza tutajadili kama tuwe na Katiba ya Tanganyika na ya Muungano na ya Zanzibar.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]
  Pili tutairekebisha Katiba ya Muungano ili iondokane na viraka viraka, kama tunataka, baada ya majadiliano, kuendelea kuwa na Muungano. Tatu tutajadili kama tunaihitaji Muungano, na kama ndivyo uwe wa namna gani.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Na mwisho tungeirekebisha katiba kwa kuangalia kama tuna mambo ya kijamii, yangejadiiliwa wakati huo ili kuona kama yangefaa kuwa katika katiba au hapana.[/FONT]
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Aaah! Kumbe katiba ya Tanganyika ndio katiba ya Muungano!. Watanganyika wajanja kweli, lakini Wazenj wamesha washtukia.
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  hakuna nchi inayoitwa Tanganyika, na hakuna watanganyika, Kuna Jamhuri ya Muungano Ya Tanzania na kuna Watanzania, Jamhuri ya Muungano ina serikali mbili, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano, Hiyo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambuliwa na Serikali ya Muungano pekee katika hii dunia, wanachotaka kukifanya Wanzanibar ni kuitangaza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar dunia nzima, na kwa kufanya hivyo ina maana Muungano hakuna tena
   
 4. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wewe kweli ni kituko na naishangaa IQ yako ni ngapi ndugu . Serikali ya Jamhuri ya Muungano imetokea wapi? Na hapo awali kabla hawajaungana zanzibar na tanganyika zilikuwa nini? Na unaposema serikali mbili ya muungano na zanzibar inamaana nchi inaendeshwa na serikali mbili? Binafsi sijawahi kuona muungano wa ajabu kama huu kwasababu meli ikiwa na manahodha wawili itafika kweli katika safari yake?
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2010
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kwanini watanganyika mnakataa Utaifa wenu? Kulikoni?
   
Loading...