Wakuu heshima mbele sana,
Kumekuwa na sintofahamu nyingi sana mara baada ya Serikali kwa bahati mbaya au makusudi kugawa fedha ya change ya Rada Tanzania bara pekee na Tanzania visiwani kutokupata hata centi moja, Wabunge wengi wa Zanzibar wameonekana kutokupendezwa na swala hili, Je ni sahihi kwa mgawo wa Rada kugawanywa bara pekee na si visiwani..?
Sr. Magdalena, japo wengi wamekujibu kuwa Rada sio issue ya muungano, wamekosea!. Ukweli ni huu!.
1. Rada ni suala la muungano!. Japo rada ile ilinunuliwa kwa Watanzania kudanganywa kuwa ni rada ya kiraia!, kiukweli radar ile ni radar ya kijeshi iliyotumia "obsolate" technology na ndio maana ilisababisha kelele sana toka kwa nchi wafadhili!. Ulinzi na usalama ni suala la muungano!.
2. Jee rada hiyo ilinunuliwa na nani na inasimamiwa na nani?. Rada ilinunuliwa na Mamlaka ya Usalama wa Anga, TCAA na kusimamiwa na mamlaka hiyo hiyo!. Mamlaka ya Usalama wa Anga ni ya Muungano!. Hivyo rada ni ya muungano!.
3. Jee fedha za rada zilitoka wapi?. Fedha za rada zilichotwa toka mfuko mkuu wa hazina na zilikopwa toka benki ya Stanbic ya Uingereza hivyo fedha hizo ni sehemu ya deni la Taifa!. Mfuko mkuu wa hazina ni suala la muungano!.
4. Mgawo wa fedha hizi ni uthibitisho wa matatizo ya structure ya muungano kwani wakati zinachotwa, zimechotwa mfuko mkuu wa hazina ambao ni wa muungano na zikawa executed kupitia wizara ya mawasiliano na uchukuzi ambayo siyo ya muungano lakini Mamlaka ya Usalama wa Anga, TCAA ambayo ni taasisi ya Muungano iko chini ya wizara ambayo sio ya muungano!.
4. Wakati wa kurudishwa kwa fedha hizo, government negotioation team iliongozwa na wizara ya mambo ya nje ambayo ni ya muungano na the lobby group ni Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ambayo pia ni ya muunngano!.
5. Ilikubaliwa kuwa fedha hizo zitumike kuimarisha elimu ya msingi ambayo sio ya muungano!. This is an oversight!. Wabunge wako right kutetea haki za Zanzibar kupata mgao huo!.
6. Wizara zote ambazo sio za Muungano ikiwemo Wizara ya Uchukuzi, zinasimamia vipi taasisi za Muungano kama Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Mamlaka ya Hali ya Hewa na Shirika la Ndege la Tanzania?!.
7. Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia sio wizara ya muungano, lakini ndio inayosimamia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA ambayo ni taasisi ya Muungano?!.
8. Tukubali tukatae, muungano wetu unatatizo la imbalance kwa Zanzibar kujiona kama equal part ya muungano!, huku sisi bara tukiiona Zanzibar kama sehemu tuu ya muungano ambayo kama mkoa fulani!.
9. Tufike mahali ama Zanzibar ipatiwe haki zake zote stahili ndani ya muungano or let Zanzibar Go! ili sasa ijibebe!. Japo tumechoka kuibeba, lakini Zanzibar sasa sio tuu ni mtoto mtukutu, bali ni toto tundu!. Jee mtoto wako mwenyewe uliyembeba kwenye mbeleko, akianza utukutu na kukupiga mateke huku akieusha rusha miguu umshushe, jee utambwaga chini, au utamshusha taratibu?!.
10. Tanzania kama mama imeibeba sana Zanzibar kwenye mbeleko ya muungano kama mtoto mdogo kwa muda mrefu!. Lakini kwa vile mtoto hiyu hajiwezi kwa lolote wala chochote!, hata apige kelele vipi huku akirusha rusha miguu!. Kamwe hatutambwaga chini mtoto wetu, bali tutamtia adabu tuu!, not to let Zanzibar Go!.