Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,934
Ni wakati wa kutafakari faida za Muungano. Na kama zipo, ni muhimu kuwa na Muungano imara ambao tunakubaliana uwe ni Muungano wa namna gani.
Fikiria kuwa mikopo yote inatafutwa kwa jina la Tanzania, ambayo kimsingi ni Tanganyika. Na siku zote anayekopa ndiye anayedaiwa. Lakini pesa hiyo ya mkopo inapelekwa kuijenga Zanzibar, kuna wakati Zanzibar imepewa mpaka 20% ya mkopo.
Wakati Tanzania inahangaika kutafuta mikopo na misaada, inahangaika kuvutia wawekezaji, inahangaika na kufanya jitihada kubwa kuvutia watalii, Zanzibar inadidimiza sekta ya utalii kwa kufanya matendo ambayo kwa vyovyote, yatafifisha utalii.
Huko Zanzibar, watalii wamezuiwa kula hadharani. Ikumbukwe hawa watalii, hawakwenda Zanzibar wakashinde vyumbani, kutalii ni kuzunguka na kutembelea maeneo mbalimbali, na wanapotembea, wengine huwa na lunch boxes zao au snacks kama biscuits, n.k. Wamelipa gharama zote, hawakuambiwa kuwa wakifika Zanzibar wote watalazimishwa kufunga au kwenda kulia snacks zao vyooni/mafichoni. Wanaenda kukutana na karaha hii wakiwa wamefika Zanzibar.
Dini ni suala binafsi halitakiwi kulazimishwa kwa mtu mwingine. Anayekula hadharani, kwani amekuwekea wewe chakula mdomoni hata uumizwe na kula kwake? Wewe umeamua kuacha kula mchana kwa kipindi fulani, na kuamua kula wakati wa usiku, kwa nini uwalazimishe na wengine kufanya hivyo hivyo?
Nilitarajia kufunga kungeendana na matendo mema, lakini inaonekana ni kinyume chake kwa upande wa Zanzibar. Je, wanaoendekeza hayo, wamefunga au ni wanafiki wanaotaka kuharibu Taifa kwa mgongo wa dini?
Serikali ya Zanzibar ijitafakari. Haiwezekani Zanzibar wafanye matendo yanayofifisha uchumi wa nchi, halafu wakiwa katika uduni wa uchumi, mzigo unaangukia kwa nchi nzima kuwaokoa.
Tusiwe wanafiki, tukemee kwa nguvu zote unafiki unaoendelea Zanzibar. Kama Zanzibar, haitaki wageni, wanataka kila mmoja akifika Zanzibar awe muislam, waitangazie Dunia, na siyo kuwakerehesha watu wakati tayari wakiwa wamefika Zanzibar.
Sheria za nchi zifuatwe. Nchi yetu inatoa uhuru wa kila mtu kufuata imani yake na yale anayotaamini kwa kadiri ya mafundisho ya dini anayoiamini, bila ya kuingilia uhuru wa mtu mwingine, alimradi uhuru huo usikiuke sheria za nchi.