Zanzibar ina mengi ya kujifunza kutoka Scotland

Kilichotokea Uingereza kwa Scotland kukubali kuendelea kuungana na UK ni kitendo kizuri cha kuigwa na Zanzibar. Katika dunia ya leo wakati mataifa yanaungana ili kupata nguvu ya kushindana kiuchumi si muda wa kufikiria kutengana hata kidogo.

Wazanzibar mnatakiwa kufahamu UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU..
 
Ni mkanganyiko mtupu pale ....waziri mkuu wa pale Scotland Alex Salomond kateuliwa na malkia lakini waziri kuu wa zenji bwana shein kachaguliwa na ccm, kwanza wale hawana kero a muungno
 
Mtumwa hajui kujituma amezoea kutumwa Jamaa wamekataa uhuru, scotland scotland scotland . . . . . . . .

huku tanganyika mmetuletea shida!!!!!
soon MSALANI na timu yake watabisha hodi kwenye uzi huu.
 
Last edited by a moderator:
Habari zilizopatikana kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa zinasema 58.5% wamekataa kujitenga na himaya ya Uingereza katika kura ya maoni.
Hapa kwetu kumekuwa na kelele nyingi kuhusu muungano huu na kufikia hatua ya kuharamiana kimaneno kama vile muungano huu ni wa kulazimishana. Jee sii vema hatua za kiungwana kama walizoonyesha wenzetu zikafanyika ili kuraya maoni ipigwe na watu wajiamulie wenyewe hatima yao?
 
Hata hapa Tanzania wanaotaka kuvunja Muungano ni wachache sana bali wengi wanataka uboreshwe
 
Scotland wamekataa kwa kishindo kujitoa kwenye muungano wao na England ingawa maamuzi na serikali hufanyika landon.Je wazanzibar wamejifunza nini?
 
Matokeo ya kura Scotland yanawafunga mdomo wale wanaohubiri Zbz kujitenga. Wananchi wawe macho na watu wanaoeneza ubaguzi kwani Tz bara na Zb ni ndugu. Viongozi kama yule aliyemwita Keissy 'mwarabu' hafai hata kuwa katibu kata. Ni ujinga kumhukumu mtu kwa rangi, dini, eneo au haiba yake. Hongera sana Scotland kumkataa Salmond ambaye ndiye alikuwa 'jusa' wa Uingereza!
 
Hivi karibuni Scotland itapiga kura ya maoni (Referendum) kuamua kwamba inataka kubaki katika United Kingdom ama laa.

Kura hii ni muhimu sana kwa mustakabali wa nchi ya Scotland ambayo kwa miaka mingi imekuwa chini ya himaya ya Uingereza baada ya kujiunga pamoja na kuunda United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland.

Umoja huu uliundwa mwaka 1801.

Kura ya maoni itafanyika tarehe 18 Septemba 2014 na kwenye karatasi ya kura kutakuwa na suala moja tu nalo ni : Je unataka Scotland iwe ni nchi huru? Na jibu liwe ima ni ‘Ndiyo’ au ‘Hapana’.

Scotland, kama Zanzibar, ilikuwa ni nchi huru ambayo kwa kuungana na Uingereza mwaka 1801 ikapoteza utaifa wake kama Zanzibar ilivyopoteza utaifa wake walipoungana na Tanganyika.

Scotland, kama Zanzibar, illiingia katika muungano huu kwa kupoteza utaifa wake na kubakia raia wake kuwa raia wa Uingereza kama walivyobaki raia wa Zanzibar kuwa ni raia wa Tanzania baada ya kuungana na Tanganyika.

Scotland, kama Zanzibar, ilipoteza sarafu yake na benki Kuu na hivi kuamuliwa chini ya UK wakitumia Pauni ya kiingereza kama ilivyo kwa Zanzibar kutumia sarafu ya Shilingi.

Scotland, kama Zanzibar, ilibakia na bunge lake dogo ambalo huchaguliwa na wapiga kura na kuwepo kwa miaka mine na Zanzibar tuna baraza la wawakilishi ambalo pia huchaguliwa kwa kura kwa muda wa miaka mitano.

Scotland, tofauti na Zanzibar, imeweza kupata uanachama wa FIFA na hivyo kuweza kushiriki katika michuano inayotambuliwa na FIFA kama ni nchi kamili licha ya kutokuwa na mamlaka (Sovereignty) wakati Zanzibar imekosa uwakilishi huu.

Scotland, tofauti na Zanzibar, imeweza kuienzi na kuitunza historia yake na ya nchi yake wakati Zanzibar inaonesha mwelekeo wa kupoteza historia yake kwa kutoitunza kikamilifu.

Scotland, tofauti na Zanzibar, ilivienzi na kuviboresha vituo vyake vya elimu kama vyuo vikuu na kuwa kitovu cha elimu kwa vyuo vyake hasa vikuu wakati Zanzibar iliyokuwa kitovu cha elimu kabla ya Mapinduzi kupoteza umaarufu wake huo.

Moja katika hoja kuu ambazo Scortland imeamua kuzitumia katika kutafuta uhuru wao kupitia kura ya maoni ni kwamba Scotland iliyo huru itaweza kukuza uchumi kwa kasi kubwa na kuweza kufungua milango mingi ya ajira kwa vizazi vijavyo .

Waziri wa kwanza wa Scotland, bwana Alex Salmond, alitaja mambo makuu 6 ambayo kama yakiwa chini ya himaya ya Scotland iliyo huru na mamlaka kamili yana viashiria vizuri vya maendeleo

Udhibiti wa moja kwa moja wa kodi ya Biashara
Udhibiti wa mapato kwa ujumla
Udhibiti wa kodi ya usafiri wa anga
Udhibiti katika kuajiri
Udhibiti katika sera za kibiashara
Udhibiti katika uhamiaji

Mambo haya sita kwa mujibu wa Alex Salmond yakiwa chini ya Scotland iliyo huru yenye mamlaka kamili na inajitegemea , basi Scotland itakuwa ni nchi yenye kukua kwa kasi kiuchumi kwani itakuwa na uwezo kamili wa kutengeneza ajira zitakazowanufaisha waskotishi.

Mambo haya sita yanaweza kufanana kwa kiasi kikubwa na hoja za kimsingi ambazo Zanzibar, ndani ya kivuli cha muungano, imeona zinawakandamiza na kama tulivyosikia karibuni kuwepo mjadala wa kuvutana ilipokuwa ikijadiliwa sura ya 14 ya Katiba inayohusisha mapato na matumizi ndani ya muungano.

Wakati tukishuhudia na kuona kasi ya kimaendeleo upande wa pili wa muungano haiendani sambamba na kasi ya maendeleo upande wa Zanzibar ambayo haina vyanzo muhimu vya kiuchumi vya kujitegemea na kujikuta imebaki tegemezi wa muungano wakati, kama ni mshirika katika muungano,anatakiwa apate haki kwa kulingana na uhusiano wake.

Zanzibar pia inaweza kujifunza mengi kutoka Scotland hasa katika mfumo mzima na utaratibu wa kujenga hoja mpaka kufikia suala la kuamuliwa ifanyike kura ya maoni na waulizwe wananchi kama wanataka kubaki katika muungano na ama laa.

Moja katika fundisho la kuzingatia ni uwezo wa upande mmoja wa muungano kuweza kuleta hoja ya kura ya maoni ya kujiridhisha kama muungano uliopo uendelee au uvunjike. Upande mmoja wa muungano, kwa mfano Zanzibar, una uwezo kisheria na kikatiba kuileta hoja hii na kura ya maoni ikapigwa Zanzibar tu wakati Tanganyika hawatokuwa na haja ya kupiga kura hii.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwahi kunukuliwa kwamba kama wangelijua mapema hili jinamizi la muungano liko kubwa kiasi hiki wangekwenda kuwauliza wananchi kwanza ni muungano upi wanaoutaka kabla ya kufikiria masuala ya katiba mpya.

Serikali ya umoja wa kitaifa kama imeliona jambo hili kuwa ni muhimu kwao japo kwa kuweza kupata kujifunza tu vipi mfumo hii unatumika ingelifanya busara ya kuingia hasara ya leo kwa faida ya kesho kwa kutuma viongozi wake waandamizi hasa Tume ya uchaguzi, kwenda kuwa kama Watazamaji “observers” kwenye kura hii ya kihistoria ambayo kimazingira inawezekana kufanyika Zanzibar na kujifunza kivitendo vipi mfumo wa kura ya maoni unavyofanyika katika kutafuta mamlaka kamili.

Hapa wasisubiri mwaliko kutoka Scotland bali wafanye haraka kutafuta njia ya kuweza kuhudhuria kura hii hata kama ni kwa gharama ya walipa kodi kwani ninaamini kutakuwa na maslahi muhimu kwa taifa letu ambalo linapita katika kipindi kigumu katika kuwepo kwake.

Ni kweli tayari tumeweza kufanikisha kura ya maoni kwa mara ya kwanza Zanzibar iliyopelekea kuundwa Serikali ya umoja wa kitaifa, na kama tutaitumia fursa hii ya kushuhudia kura hii ya maoni itakayofanyika Scotland mwezi ujao, ninaamini tutapata mengi yenye faida kwa mustakbali wa nchi yetu bila ya kujali kitu gani waskotishi wataamua kama ni kubaki au kujitoa katika muungano wao na Uingereza.

Chanzo:zanzinews

Scotland la Zanzibar ni vitu viwili tofauti,Scotland ilijiunga na england lakini Zanzibar iliungana na Tanganyika wakaunda Tanzania hivyo kama kuuliza waulizwe wote Watanganyika na wazanzibar.kama una uelewa nadhani utakuwa umenielewa lakini kama una akili ya kiccm sema nikufafanulie zaidi
 
Wanzanzibar wanafaidika na bara..ndio maana wanaogopa kujitenga...wauza maduka kariakoo na muuza ice-cream wataenda wapi....watanganyika ndio tupige Kura Kama tunataka muungano uvunjike....
 
Matokeo ya kura Scotland yanawafunga mdomo wale wanaohubiri Zbz kujitenga. Wananchi wawe macho na watu wanaoeneza ubaguzi kwani Tz bara na Zb ni ndugu. Viongozi kama yule aliyemwita Keissy 'mwarabu' hafai hata kuwa katibu kata. Ni ujinga kumhukumu mtu kwa rangi, dini, eneo au haiba yake. Hongera sana Scotland kumkataa Salmond ambaye ndiye alikuwa 'jusa' wa Uingereza!

Ndugu, suluhisho la kitendawili hiki cha Zanzibar ni kuiitisha kura ya maoni, sio kuchukua matokeo ya Scotland na ku-extrapolate to Zanzibar.

Suluhisho liko wazi, kwanini hatutaki kulifuata na badala yake tunaendekeza vijimaneno, au ndiyo tunataka kuwa vindicate wale wanaosema kwamba sisi Waafrika ni kizazi cha laana!
 
Hivi karibuni Scotland itapiga kura ya maoni (Referendum) kuamua kwamba inataka kubaki katika United Kingdom ama laa.

Kura hii ni muhimu sana kwa mustakabali wa nchi ya Scotland ambayo kwa miaka mingi imekuwa chini ya himaya ya Uingereza baada ya kujiunga pamoja na kuunda United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland.

Umoja huu uliundwa mwaka 1801.

Kura ya maoni itafanyika tarehe 18 Septemba 2014 na kwenye karatasi ya kura kutakuwa na suala moja tu nalo ni : Je unataka Scotland iwe ni nchi huru? Na jibu liwe ima ni ‘Ndiyo’ au ‘Hapana’.

Scotland, kama Zanzibar, ilikuwa ni nchi huru ambayo kwa kuungana na Uingereza mwaka 1801 ikapoteza utaifa wake kama Zanzibar ilivyopoteza utaifa wake walipoungana na Tanganyika.

Scotland, kama Zanzibar, illiingia katika muungano huu kwa kupoteza utaifa wake na kubakia raia wake kuwa raia wa Uingereza kama walivyobaki raia wa Zanzibar kuwa ni raia wa Tanzania baada ya kuungana na Tanganyika.

Scotland, kama Zanzibar, ilipoteza sarafu yake na benki Kuu na hivi kuamuliwa chini ya UK wakitumia Pauni ya kiingereza kama ilivyo kwa Zanzibar kutumia sarafu ya Shilingi.

Scotland, kama Zanzibar, ilibakia na bunge lake dogo ambalo huchaguliwa na wapiga kura na kuwepo kwa miaka mine na Zanzibar tuna baraza la wawakilishi ambalo pia huchaguliwa kwa kura kwa muda wa miaka mitano.

Scotland, tofauti na Zanzibar, imeweza kupata uanachama wa FIFA na hivyo kuweza kushiriki katika michuano inayotambuliwa na FIFA kama ni nchi kamili licha ya kutokuwa na mamlaka (Sovereignty) wakati Zanzibar imekosa uwakilishi huu.

Scotland, tofauti na Zanzibar, imeweza kuienzi na kuitunza historia yake na ya nchi yake wakati Zanzibar inaonesha mwelekeo wa kupoteza historia yake kwa kutoitunza kikamilifu.

Scotland, tofauti na Zanzibar, ilivienzi na kuviboresha vituo vyake vya elimu kama vyuo vikuu na kuwa kitovu cha elimu kwa vyuo vyake hasa vikuu wakati Zanzibar iliyokuwa kitovu cha elimu kabla ya Mapinduzi kupoteza umaarufu wake huo.

Moja katika hoja kuu ambazo Scortland imeamua kuzitumia katika kutafuta uhuru wao kupitia kura ya maoni ni kwamba Scotland iliyo huru itaweza kukuza uchumi kwa kasi kubwa na kuweza kufungua milango mingi ya ajira kwa vizazi vijavyo .

Waziri wa kwanza wa Scotland, bwana Alex Salmond, alitaja mambo makuu 6 ambayo kama yakiwa chini ya himaya ya Scotland iliyo huru na mamlaka kamili yana viashiria vizuri vya maendeleo

Udhibiti wa moja kwa moja wa kodi ya Biashara
Udhibiti wa mapato kwa ujumla
Udhibiti wa kodi ya usafiri wa anga
Udhibiti katika kuajiri
Udhibiti katika sera za kibiashara
Udhibiti katika uhamiaji

Mambo haya sita kwa mujibu wa Alex Salmond yakiwa chini ya Scotland iliyo huru yenye mamlaka kamili na inajitegemea , basi Scotland itakuwa ni nchi yenye kukua kwa kasi kiuchumi kwani itakuwa na uwezo kamili wa kutengeneza ajira zitakazowanufaisha waskotishi.

Mambo haya sita yanaweza kufanana kwa kiasi kikubwa na hoja za kimsingi ambazo Zanzibar, ndani ya kivuli cha muungano, imeona zinawakandamiza na kama tulivyosikia karibuni kuwepo mjadala wa kuvutana ilipokuwa ikijadiliwa sura ya 14 ya Katiba inayohusisha mapato na matumizi ndani ya muungano.

Wakati tukishuhudia na kuona kasi ya kimaendeleo upande wa pili wa muungano haiendani sambamba na kasi ya maendeleo upande wa Zanzibar ambayo haina vyanzo muhimu vya kiuchumi vya kujitegemea na kujikuta imebaki tegemezi wa muungano wakati, kama ni mshirika katika muungano,anatakiwa apate haki kwa kulingana na uhusiano wake.

Zanzibar pia inaweza kujifunza mengi kutoka Scotland hasa katika mfumo mzima na utaratibu wa kujenga hoja mpaka kufikia suala la kuamuliwa ifanyike kura ya maoni na waulizwe wananchi kama wanataka kubaki katika muungano na ama laa.

Moja katika fundisho la kuzingatia ni uwezo wa upande mmoja wa muungano kuweza kuleta hoja ya kura ya maoni ya kujiridhisha kama muungano uliopo uendelee au uvunjike. Upande mmoja wa muungano, kwa mfano Zanzibar, una uwezo kisheria na kikatiba kuileta hoja hii na kura ya maoni ikapigwa Zanzibar tu wakati Tanganyika hawatokuwa na haja ya kupiga kura hii.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwahi kunukuliwa kwamba kama wangelijua mapema hili jinamizi la muungano liko kubwa kiasi hiki wangekwenda kuwauliza wananchi kwanza ni muungano upi wanaoutaka kabla ya kufikiria masuala ya katiba mpya.

Serikali ya umoja wa kitaifa kama imeliona jambo hili kuwa ni muhimu kwao japo kwa kuweza kupata kujifunza tu vipi mfumo hii unatumika ingelifanya busara ya kuingia hasara ya leo kwa faida ya kesho kwa kutuma viongozi wake waandamizi hasa Tume ya uchaguzi, kwenda kuwa kama Watazamaji “observers” kwenye kura hii ya kihistoria ambayo kimazingira inawezekana kufanyika Zanzibar na kujifunza kivitendo vipi mfumo wa kura ya maoni unavyofanyika katika kutafuta mamlaka kamili.

Hapa wasisubiri mwaliko kutoka Scotland bali wafanye haraka kutafuta njia ya kuweza kuhudhuria kura hii hata kama ni kwa gharama ya walipa kodi kwani ninaamini kutakuwa na maslahi muhimu kwa taifa letu ambalo linapita katika kipindi kigumu katika kuwepo kwake.

Ni kweli tayari tumeweza kufanikisha kura ya maoni kwa mara ya kwanza Zanzibar iliyopelekea kuundwa Serikali ya umoja wa kitaifa, na kama tutaitumia fursa hii ya kushuhudia kura hii ya maoni itakayofanyika Scotland mwezi ujao, ninaamini tutapata mengi yenye faida kwa mustakbali wa nchi yetu bila ya kujali kitu gani waskotishi wataamua kama ni kubaki au kujitoa katika muungano wao na Uingereza.

Chanzo:zanzinews

hapa kwetu sio suala la kuulizwa wazanzibar, hapa kwetu watanganyika wanataka nchi yao kutoka Tanzania na wanzanzibari wanataka nchi yao kutoka Tanznia
 
Mleta mada nafikiri tunachopashwa kujifunza hapa sio nani kashinda au nani kashindwa, nani kakubali kuendelea kuwa mtumwa na nani kakataa minyororo ya utumwa wa uingereza. Tunachopashwa kujifunza kwa maoni yangu ni watu kupewa uhuru kwa kuamua wanachokitaka. Wenzetu wa Zanzibar kama ilivyofanyika Scotland nao wapewe nafasi ya kupiga kura ya maoni waseme kama Muungano huu wa Waasisi uendelee au ukome? Tanganyika hali kadhalika tuulizwe kama tunaitaka Tanganyika yetu au tunataka kuendelea kumezwa ndani ya tumbo la mnyama aitwaye Tanzania.

Tupewe uhuru wa kuamua kama wascotish walivyopewa uhuru.

Tiba
 
Kwani mejiuliza wanaotaka huo utengano Zenji ni wananchi? Walevi tu wa madaraka na wenye ulafi majina yao yawe kwenye historia na huku wakitaka kumrudisha mwarabu kisingizo wataendelea.
Nani atakuletea maendeleo kama hujishughulishi??

Pamoj na ungese wa baadhi ya viongoz wa zanzibar,Muungano na tanganyika bado sio efficient enough.malalamiko yafanyiwe kazi lakni sio kutengana.
 
Jana Wascotish wamepiga Kura ya kuamua kama wanataka kujitenga na Uingereza au LA. Matokeo yaliyotangazwa leo asubuhi yameonyesha kuwa KURA ya HAPANA imeshinda, Wascotish wamekataa kujitenga na Uingereza maana yake muungano wa visiwa hivyo (sijui ni vingapi, ni 3 au 4) uliodumu kwa zaidi ya karne 3 utaendelea.

Wakati kampeini za kura hizo zikiendelea, Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron aliwaahidi Wascotland kuwa kama watakataa kujitenga na Uingereza na kubaki ndani ya Muungano basi Uingereza itaipa mamlaka zaidi Scotland.

Hapa Kwetu, Sura zinazozungumuzia muundo wa Muungano katika katiba mpya (sura ya 2 na Sura ya 6) inayoandikwa sasa imekuwa ni gumzo kubwa kwa nchi yetu na hata kupelekea kuhitilafiana kati ya wajumbe wa bunge maalum la Katiba. Je tunacho cha kujifunza kutoka Scotland? Muundo wa muungano wa Uingereza Ukoje? Scotland ina seat UN? Je Scotland ni Mwanachama wa mashirikisho ya Kimataifa kama ya FIFA? Ni mambo gani yanayoratibiwa na serikali ya Muungano na yepi wascotland wanaamua wenyewe? Michango ya kuendesha serikali ya Muungano ikoje? gharama za kuendesha serikali za washirika zikoje??

Zanzibar kwa miaka mingi sana haijaridhishwa na uendeshaji wa muungano, imekuwa ikitaka madaraka zaidi, ikitaka kuwa na uwezo wa kujiamulia mambo yake zaidi, Zanzibar inataka kuwa na seat katika Umoja wa Mataifa, Zanzibar inataka iwe na uwezo wa kujiunga na mashirika ya Kimataifa kama OIC? Je umefika wakati sasa wa Rais wa JMT kumuiga David Cameron na kuwapa wazanzibari Madaraka zaidi?? Au umefika wakati wa kuwa na referendum hata hapa kwetu kuamua kama Tanzania bara inataka kubaki ndani ya Muungano au itoke?? Matokeo ya Kura za maoni Scotland zitaawathiri vipi wale wanaotaka muundo wa serikali 2 na wale wanaotaka muundo wa serikali 3??

Daaa!! Scotland Bwana
 
Wanzanzibar wanafaidika na bara..ndio maana wanaogopa kujitenga...wauza maduka kariakoo na muuza ice-cream wataenda wapi....watanganyika ndio tupige Kura Kama tunataka muungano uvunjike....

Kwa hiyo una maana yule mbunge wa CCM aliyesema wanainyonya Tanganyika alikuwa sahihi?
 
Back
Top Bottom