zanzibar gizani tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

zanzibar gizani tena

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kireka1980, Dec 11, 2009.

 1. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mm nipo zanzibar jana siku nzima hakukuwa na umeme kisiwa chote, ukarudi saa kumi na moja for two hours then ukakatika hadi this time haujarudi, kama kuna mwenye data zaidi. HII NI HATARI KIUSALAMA KISIWA CHOTE KUWA GIZANI!
   
 2. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa mujibu wa habari zilizopo; ni tatizo kama lile lililotokea huko nyuma ambapo umeme ulikosekana kwa mwezi mzima!!!

  Inasemekana ile marine cable(main cable itokayo bara) imeharibika tena; watu wa ZECO(Tanesco znz) bado hawajatoa tathmini yao.
   
 3. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mh magenerator yashakuwa deal sasa, thanx God langu sikuliuza ngoja nikalifufue
   
 4. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Press Conference ya Waziri Mansoor Himid imeisha muda si mrefu; ametangaza kuwa Zanzibar itakuwa gizani kwa muda wa wiki 3 hadi hapo mafundi watakaporekebisha tatizo lililojitokeza.

  Poleni sn huko visiwani, inabidi mnunue ma-generetor sasa maana habari ndio hiyo
   
 5. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,407
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  Na hapo bado kuna muungano..........!!!!!!!!!!! Tukiachana tu, tutakuwa tunaukata kwa makusudi........... Teheee tehe... hasa hasa mkichelewesha malipo ya bili
   
 6. B

  Bumbwini Member

  #6
  Dec 11, 2009
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama mambo yenyewe ndio hayo inabidi zanzibar smz itafute suluhisho la umeme la kudumu kutegemea umeme wa bara watajisumbua,huku tanganyika kwenyewe hakuna umeme wa uhakika,unategemea kuazima jamvi kwa jirani yako wakati yeye jirani yako ana msiba.wazenj amkeni tafuteni suluhisho la kudumu la tatizo la umeme nyie wenyewe kama taifa huru,
   
 7. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2009
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Poleni sana... sasa wale wataalamu waliokuja kurekebisha last time,,hawakutoa guarantee!! au hiyo marine cable imebobojoka sehemu nyengine?
   
 8. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  yaani hii nchi yaetu sijui inaongozwa na watu wa aina gani! wataalam walipendekeza system nzima ibadilishwe kwan sababu imechakaa na ni yakizamani, serikali ikasema ooh itachukua muda mrefu mno kuireplace irekebishwe ilipoharibika tuu. matokeo yake ndio hayo sasa.
   
 9. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Khatari kubwa. Pale Fumba kunani pale?

  Inaa maana mpaka mwakani kutakuwa hakuna Umeme.
   
 10. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #10
  Dec 12, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  ,,,,Hapo nilipo bold na ku italic hapo,Tatizo sio umeme wa bara haupatikani,tena kwa taarifa yako TANESCO siku zote wamekua wakiipendelea mno ZENJI,inatokea MIGAO mikalimikali huko BARA,lakini ukifika ZENJI umeme upo tena ulikua wa uhakika,Tatizo ni hiki ki kampuni kinajiita ZECO,inakuaje kampuni mama ikose spare parts muhimu ghalani???,this time around kilicho haribika sio MARINE CABLE yenyewe,ni kitu ambacho spare yake haipo katika STORE mfu za vijaa vya ZECO,na yote hii imetokana na ongezeko kubwa la matumizi wakati ma TRANSFORMER yanayotumika ni yaleyale ya miaka ileee,,,hii mijitu tusipoibadili,hakiamama vile tutaendelea kuishi kwa KUBAHATISHA kwa miaka mia ijayo,,watu kama hamuwezi si MTOKEEE!!!
   
 11. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,054
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  wazanzibar banaah kazi kila siku ooh muungano ufe !!!kumbe hawayawezi ona sasa wanavyovurunda hako sijui ka ZECO???mmmmh muungano na ufe tuu uone kama uko Zenji kutakalika hawatakawia kusema sijui wanyamwezi/wazaramo/wanyasa ili tu warejee bara.Watakula jeuri yaooooo.NA BADO !!!!
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Yale majenereta ya Saateni vipi? Yameingia kutu nini?
   
 13. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hatimaye Umeme umerudi tena jioni hii; nimeongea na mtu wangu wa karibu huko visiwani amenithibitishia hilo.

  Lakini kutakuwa na muendelezo wa matengenezo kuelekea katika ufmbuzi wa kudumu wa tatizo la main cable kutoka bara. Juzi niliskia Kaimu Manager wa ZECO akisema wanatarajia kubadilisha waya wote na kazi hiyo inatarajiwa kukamilika kabla ya mwishoni mwa mwezi January.
   
 14. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #14
  Dec 22, 2009
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  ,,,Nani kakudanganya muzee,hiyo source yako KIMEO,giza na joto limetawala haka ka NCHI,na nasikia balaa lishakua kubwa,waziri wa Nishati anapaswa kuachia ngazi sasa,maneno meeengi kuhusu MAFUTA,ilhali hata nishati hii tuliyonayo ya kuazima tu inatushinda kuitia majumbani mwetu,,Mheshimiwa acha maneno meengi,fanya kazi,na ka huwezi achia ngazi,tushachoka kukaa na giza na mikelele ya jenerators fake hizi.
   
 15. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tatizo sio umeme ...tatizi sisi wenyewe wabongo,watanganyika,wa zenji ,wapemba au kila m tz...
  ccm imeshindwa kuiongoza tanzania, inataka muungano wa kulazimisha...kwahiyo inatumia muda mwingi kuwatia watanzania upumbavu na woga...wale waliosema watanzania tumelala fofo ni kweli...kamakuna mtu atanuna poa tu...sisi sio nchi ni kundi tu la wapumbavu tunaoishi tanzania...na hao wanaotuongoza ,pia wapumbavu ambao baadhia yao washahada za upumbavu. tanzania sia nchi yakuwa na tatizo la maji wala umeme....lakini hii ccm badala ya kufanya maendele inawakandamiza raia wake na kuwatia woga na upumbavu...boro kuzaliwa mbwa ulaya kuliko kuzaliwa binaadam tanzania...bull shit
   
Loading...