Zanzibar: CUF hawaepukiki

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Pamoja na CCM kutangazwa washindi katika ngazi ya Urais,Uwakilishi na Udiwani,CUF hawaepukiki katika ustawi wa Zanzibar. Katika uchaguzi wa jana,CUF iligomea uchaguzi huo ingawa wagombea wao hawakuondolewa kwenye karatasi za kupigia kura.

Hali halisi hapa Zanzibar inaonesha kuwa CUF wanahitajika,kuliko wakati wowote ule,katika kutanzua mkwamo mpya wa kikatiba pamoja na kufanyika uchaguzi unaosifiwa kipropaganda. Hapa Zanzibar,kwa hali ilivyo kulingana na matokeo,hakutapatikana Makamu wa kwanza wa Rais.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar,makamu wa kwanza wa Rais anapaswa kuwa mgombea aliyeshika nafasi ya pili ambaye lazima awe amepata asilimia kumi ya kura zote halali. Kwa asilimia tisini na moja za Dr. Shein,hakuna mgombea aliyepata asilimia kumi. Ndiyo kusema,hata Hamad Rashid,ingawa ndiye aliyetangazwa wa pili,hawezi kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar. ADC ya Hamad Rashid haina hata Mwakilishi mmoja pia.

Katika kuliona hilo,leo hii hii,Rais mteule Dr. Shein na hata Hamad Rashid wamekiri uwepo wa mgogoro wa kisiasa. Kwakuwa CUF hawakushiriki katika uchaguzi wa jana waliouita batili,watashiriki kutafuta suluhisho? Hapa,wananchi karibu wote wako puzzled!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Zanzibar)
 
Mkuu VUTA NIKUVUTE waambie vijana wako wa Lumumba wasionyeshe ujinga wao. Katiba ni katiba inapokuwepo itakuwa ni uhalifu kuivunja.

Umemsikia Magufuli kuhusu uchaguzi wa Meya Dar? Huu ni ujumbe tosha kwa uchaguzi wa Zanzibar.

Lumumba mjipange Magufuli yuko njiani kuitumbua CCM tena kwa kushtukiza

Aione TataMadiba na wajinga wengine wa Lumumba
 
Wanacheza na Mwenyezi Mungu , amewalaani tena ,Jecha na kundule ke lazima wafahamu kuwa ALLAH yupo anawaangalia ,haya tusubiri wabadilishe matokeo wampe SHeni asilimia 81, na hata hilo haliwashughulishi CUF ,wao hawakushiriki na mpira ni hivyo vyama vitimbakwiri vilivyoshiriki ,wakubali mmoja wao alipwe umakamo kama bahshishi ya kushiriki,
Hongera CUF ALLAH yu pamoja nawe.
 
Kuna mtanziko mkubwa.....pia wakati waabadili katiba yao, walivunja katiba ya jamhuri ya muungano
 
Pamoja na CCM kutangazwa washindi katika ngazi ya Urais,Uwakilishi na Udiwani,CUF hawaepukiki katika ustawi wa Zanzibar. Katika uchaguzi wa jana,CUF iligomea uchaguzi huo ingawa wagombea wao hawakuondolewa kwenye karatasi za kupigia kura.

Hali halisi hapa Zanzibar inaonesha kuwa CUF wanahitajika,kuliko wakati wowote ule,katika kutanzua mkwamo mpya wa kikatiba pamoja na kufanyika uchaguzi unaosifiwa kipropaganda. Hapa Zanzibar,kwa hali ilivyo kulingana na matokeo,hakutapatikana Makamu wa kwanza wa Rais.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar,makamu wa kwanza wa Rais anapaswa kuwa mgombea aliyeshika nafasi ya pili ambaye lazima awe amepata asilimia kumi ya kura zote halali. Kwa asilimia tisini na moja za Dr. Shein,hakuna mgombea aliyepata asilimia kumi. Ndiyo kusema,hata Hamad Rashid,ingawa ndiye aliyetangazwa wa pili,hawezi kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar. ADC ya Hamad Rashid haina hata Mwakilishi mmoja pia.

Katika kuliona hilo,leo hii hii,Rais mteule Dr. Shein na hata Hamad Rashid wamekiri uwepo wa mgogoro wa kisiasa. Kwakuwa CUF hawakushiriki katika uchaguzi wa jana waliouita batili,watashiriki kutafuta suluhisho? Hapa,wananchi karibu wote wako puzzled!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Zanzibar)

Kwa mara ya kwanza napingana na wewe. Waliotunga hiyo katiba walijua hilo linaweza kutokea na wakaweka maelekezo ikitokea hivyo nini kifanyike (take as an asignment) CUF wanachosubiria ni busara za Shein na nafasi mbili za wapinzani (kwa mujibu wa katiba) katika nafasi 10 za upendeleo kwa Rais.
 
Kwanza nikupe hongera kwa kujifunza kwa vitendo. Usiusahau usemi asiyefunzwa na mama yake hufunzwa na dunia; ni matumaini yangu kuna somo tumejifunza wote. Tunasubiri kwa hamu mwelekeo baada ya matokeo haya.
 
Kwa mara ya kwanza napingana na wewe. Waliotunga hiyo katiba walijua hilo linaweza kutokea na wakaweka maelekezo ikitokea hivyo nini kifanyike (take as an asignment) CUF wanachosubiria ni busara za Shein na nafasi mbili za wapinzani (kwa mujibu wa katiba) katika nafasi 10 za upendeleo kwa Rais.
Usitoe porojo. Nipinge au nikosoe kikatiba. Karibu mkuu!

Mzee Tupatupa
 
Kwa mara ya kwanza napingana na wewe. Waliotunga hiyo katiba walijua hilo linaweza kutokea na wakaweka maelekezo ikitokea hivyo nini kifanyike (take as an asignment) CUF wanachosubiria ni busara za Shein na nafasi mbili za wapinzani (kwa mujibu wa katiba) katika nafasi 10 za upendeleo kwa Rais.
Mkuu CUF wamesusia kila kitu kwa sababu ni haramu. Shein atafanya ya Jecha matokeo yatakuwa ya ki Jecha Jecha mgogoro hadi bara unakuja.
 
Pamoja na CCM kutangazwa washindi katika ngazi ya Urais,Uwakilishi na Udiwani,CUF hawaepukiki katika ustawi wa Zanzibar. Katika uchaguzi wa jana,CUF iligomea uchaguzi huo ingawa wagombea wao hawakuondolewa kwenye karatasi za kupigia kura.

Hali halisi hapa Zanzibar inaonesha kuwa CUF wanahitajika,kuliko wakati wowote ule,katika kutanzua mkwamo mpya wa kikatiba pamoja na kufanyika uchaguzi unaosifiwa kipropaganda. Hapa Zanzibar,kwa hali ilivyo kulingana na matokeo,hakutapatikana Makamu wa kwanza wa Rais.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar,makamu wa kwanza wa Rais anapaswa kuwa mgombea aliyeshika nafasi ya pili ambaye lazima awe amepata asilimia kumi ya kura zote halali. Kwa asilimia tisini na moja za Dr. Shein,hakuna mgombea aliyepata asilimia kumi. Ndiyo kusema,hata Hamad Rashid,ingawa ndiye aliyetangazwa wa pili,hawezi kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar. ADC ya Hamad Rashid haina hata Mwakilishi mmoja pia.

Katika kuliona hilo,leo hii hii,Rais mteule Dr. Shein na hata Hamad Rashid wamekiri uwepo wa mgogoro wa kisiasa. Kwakuwa CUF hawakushiriki katika uchaguzi wa jana waliouita batili,watashiriki kutafuta suluhisho? Hapa,wananchi karibu wote wako puzzled!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Zanzibar)
mkuu,next time ukienda uko visiwani unipitie namimi!
Mkuu VUTA NIKUVUTE waambie vijana wako wa Lumumba wasionyeshe ujinga wao. Katiba ni katiba inapokuwepo itakuwa ni uhalifu kuivunja.

Umemsikia Magufuli kuhusu uchaguzi wa Meya Dar? Huu ni ujumbe tosha kwa uchaguzi wa Zanzibar.

Lumumba mjipange Magufuli yuko njiani kuitumbua CCM tena kwa kushtukiza

Aione TataMadiba na wajinga wengine wa Lumumba
mkuu,naona usha danganyika na porojo za magufuli!usivuke daraja kabla ya kulifikia!
 
Back
Top Bottom