Waziri Ndaki na Katibu (Mifugo) Nzunda, Uhalisia kuhusu kuomba kusitisha mafunzo atimizi (internship) kwa Madaktari wa Mifugo

Vet Surgeon

Member
May 17, 2022
20
14
Waziri Ndaki na katibu(mifugo) Bw. Nzunda, Uhalisia kuhusu kuomba kusitisha mafunzo atimizi (internship) kwa madaktari wa mifugo.

kutoka kwa Vet Surgeon


Habari Mh. Mashimba Ndaki , pole na majukumu na hongera kwa kuwezesha sekta ya mifugo kuendelea kusonga mbele.

Kulingana na Takwimu za 2020, Tanzania inakadiriwa kua na mifugo million 33.9 na ya pili kwa wingi wa mifugo Afrika, baada ya Ethiopia. Pia kilimo na mifugo vina changia zaidi ya asilimia 28 ya uchumi wetu. Hizi zote ni juhudi zako Mheshimiwa.

Katika sekta hii ya mifugo kuna wataalamu mbalimbali walio ajiriwa ili kulinda afya ya jamii na afya za wanyama (public health, Animal health and one health etc) kama wakaguzi wa nyama (meat inspector), madaktari wa wanyama nk.

Katika wizara yako upande wa mifugo kuna shahada mama ya Udaktari wa mifugo, ambayo ina tolewa na chuo cha kilimo cha Sokoine University of Agriculture (SUA)

Kuhusu mafunzo atimizi (internship) kwa madaktari wa mifugo

Mafunzo atimizi kwa madaktari wa mifugo, ni ya mhimu sana kwetu kama madaktari wa mifugo na yana tuandaa vyema kwa vitendo kwenda kuitumikia jamii. Mafunzo haya yapo kisheria , yanapatikana katika Sheria ya Veterinari ( Veterinary Act , 2003), Sura 319 na kanuni zake(regulations) 2020 (GN. 725& 726).

Kwanini tunaomba aya mafunzo yasitishwe?

1. Kanunu zake za 2020 (regulations) bado zinaitaji marekebisho ( amendment), kwasababu zimekaa kinyonyaji. Zina mhitaji daktari aliyesoma miaka 5 au zaidi (5 solid year's) , aende kwenye mafunzo atimizi (intern) mwaka mzima bila malipo ya kujikimu 😭😭😭😭😭😭😭😭. Uyu mtu amesoma kwa shida yaani kwa mkopo wa HESLB, wengine ni yatima, wengine wanafamilia, wengine wamesomeshwa. Je hatawezaje kuishi mwaka mzima bila malipo ya kujikimu?????

2. Mafunzo atimizi (internship) , miaka yote hayakuwepo. Toka fani hii imeanzishwa , kuna madaktari, maprofesa walifanya na wanafanya vizuri tu mtaani bila kuwepo haya mafunzo, kwanini wayalazimishe kipindi hichi bila mandalizi yoyote kwa wahusika 😭😭😭😭😭😭. Nyie ndio wenye nguvu ya kimaamuzi (decision power) kuhusu sisi, kwanini msiweke mambo sawa kabla ya kutoa maamuzi ambayo hayata tuumiza sisi 😭😭😭😭😭😭😭😭.

3. Wizara ya afya ina fani mama nyingi kama madaktari wa binadamu, wakunga, wataalamu wa madawa, wataalamu wa mahabara, watalaamu wa lishe nk., na ina vyuo vingi vinavyo toa izi fani. Kwaio wanaomaliza ni wengi sana zaidi ya watu 1000, na kupitia wizara yao, hawa pia wana mafunzo atimizi (internship) ambayo wanalipwa asilimia 80 ya mshahara wa mtumishi wa serikali kulingana na fani yako, kama hela ya kujikimu. Sasa sisi madaktari wa mifugo ambao kwa mwaka atuzidi watu 60, kweli mmeshindwa kutufadhiri au hata kututaftia mfadhiri (sponsorship) kwenye Wizara yako ili na sisi tufanye internship na tuwe na hela kujikimu kama wenzetu 😭😭😭😭

4. Mwaka jana mlijaribu kuwalizimisha wahitimu wa 2020 waende kwenye mafunzo atimizi (internship), ila mlishindwa na mkawasajili kama madaktari wa mifugo. Kama mwaka jana mliona mapungufu, kwanini msitumie izo izo sababu na changamoto za mwaka jana mkatusajili na sisi au mkazitaftia ufumbuzi izo changamoto kabla ya kuturusu na sisi kuendelea na internship. Yaani tumemaliza toka mwaka jana (miaka 5) mpaka leo bado hatujasajiliwa yaani huu ni mwaka wa sita sasa 😭😭😭😭😭😭😭😭. Mnatupotezea malengo, tumekua kama watu wenye laana, tunaangaika mtaani na vitu viwili, yaani hatuna kazi na pia hatuwezi kufanya kazi hata yakujitolea kwasababu hatuja sajiliwa 😭😭😭😭😭😭😭.

4. Tumeangaika sana, tumeandika barua sana wizarani, ila hatujasidiwa mpaka sasa.


Kipi kifanyike
1. Watusajili tu, ili tupambane na swala moja la kutokua na kazi (jobless). Maana saizi imeshakua mwezi wa tano na bado hatujajua mustakabali wa maisha yetu.

2. Tufanye mafunzo atimizi (internship) kama kawaida , ila watutatulie changamoto ya pesa ya kujikimu, yaani yawepo malipo hata kama ni pungufu ya wanaolipa kwenye wizara ya afya.

3. Waongee na bodi ya mikopo (HESLB) , waongeze mda. Tuwe tunapewa mkopo kwa miaka sita ili mwaka wa mwisho tuwe tunaenda kwenye mafunzo atimizi (internship). Japo tunaongeza deni (financial burden). Ila itakua bora kuliko kuishi bila hela ya kujikimu mwaka mzima.

4. Msitutenganishe kati ya wenyenacho na watoto wa masikini. Kwasababu wapo watakao weza kujigharamikia mwaka mzima bila malipo, ila wapo sisi watoto wa wakulima, hatutaweza.

Hitimisho
1. Tunaomba mtusajili ili na sisi tuwe tunauwezo wa kuomba kazi kama wenzetu na pia msitutenganishe kulingana na hali zetu za familia, yaani watu wanaotoka kwenye familia bora na wenye uwezo wa kujihudumia mwaka mzima wa internship ndio wasajiliwe. Sisi masikini tukatupwa nje ya mfumo yaani "mwenye nacho kuongezewa na asio nacho kunyanganywa kabisa hata kidogo alicho nacho".

2. Toeni Elimu kwanza hasa kwa mwaka wa kwanza, ili mtu ajiandae kisaikolojia na kiuchumi kama hii program itakua unafanyika bila hela ya kujikimu. Na sio kumshitukiza mtu ambaye akujiandaa na ameshamaliza.

Ni hayo yangu, sita attach barua yoyote japo ninazo, ila uhalisia ndio huo.

Nawasalimu kwa jina la jamhuri.

Vet Surgeon

Nb: Haya ni maoni yangu binafsi
 
Mnajimalize wenyewe! Pambaneni. Tatizo wanataka kujilinganisha MD na vet doctor. Mnyama akizidiwa Dr wa Mifugo anasema chinja usipate hasara, lakini MD hawezi kusema hivyo. Pambaneni. Declare interest ni mtalaamu wa lishe ya mifugo
Sasa kama hatuna umuhimu, na kwel hatuwezi kua sawa na MD. Kwanini watulazimishe kwenda internship?????

Sasa si watuache tupambane wenyewe mtaani kuliko kutulinganisha na fani zingine za afya.
 
Mafunzo atimizi kwa madaktari wa mifugo, ni ya mhimu sana kwetu kama madaktari ya mifugo na yana tuandaa vyema kwa vitendo kwenda kuitumikia jamii. Mafunzo aya yapo kisheria , yanapatikana katika Sheria ya Veterinari ( Veterinary Act , 2003), Sura 319 na kanuni zake(regulations) 2020 (GN. 725& 726).

Kwanini tunaomba aya mafunzo yasitishwe?
1. Kanunu zake za 2020 (regulations) bado zinaitaji marekebisho ( amendment), kwasababu zimekaa kinyonyaji. Zina mhitaji daktari alisoma miaka 5 au zaidi (5 solid year's) , aende kwenye mafunzo atimizi (intern) mwaka mzima bila malipo ya kuijikimu 😭😭😭😭😭😭😭😭. Uyu mtu amesoma kwa shida yaani kwa mkopo wa HESLB, wengine ni yatima, wengine wanafamilia, wengine wamesomeshwa. Je ata wezaje kuishi mwaka mzima bila malipo ya kuijikimu?????
Una tatizo la H: Ulipata degree ya kudesa si bure.
 
ni Hatuna
Mimi sijasoma kiswahili, sio mwandishi wa habari, mimi ni daktari wa mifugo. Mapungufu siwezi kukosa.

Cha mhimu angalia hoja zangu, na lete mchango wako. Yaani muda wote ulikua unangalia makosa tu. Tena kwenye reply
 
Enzi za kuchaguliwa na TCU niliomba hii kitu kama passion yangu kuwa daktari mifugo as my first priority lakini TCU walijua walichonichagulia wao na PCB yangu ,though nashkuru Mungu hiko ndo kinanifanya napata nguvu ya kutype hapa na mengineyo japo nakumbuka nliumiaga sana.

Tuyaache hayo.........
naona wizara iangalie namna ya kufanya hapo......kufanya intern mwaka mzima bila chochote sio kitu rahisi. naelewa sababu nimebahatika kujitolea walau miezi mitatu kwenye mji wa watu .....nilishindwa aisee....πŸ™Œ

Serikali iliangalie hili Ione namna ya kuwasaidia ......
 
Mimi sijasoma kiswahili, sio mwandishi wa habari, mimi ni daktari wa mifugo. Ayo mapungufu siwezi kukosa.

Cha mhimu angalia hoja zangu, na lete mchango wako. Yaani muda wote ulikua unangalia makosa tu. Tena kwenye reply
Acha huo utoto! Kuwa msomi - ambaye anakubali challenges
 
Mimi sijasoma kiswahili, sio mwandishi wa habari, mimi ni daktari wa mifugo. Ayo mapungufu siwezi kukosa.

Cha mhimu angalia hoja zangu, na lete mchango wako. Yaani muda wote ulikua unangalia makosa tu. Tena kwenye reply
Acha weak defensive mechanisms..wewe ni msomi umesoma kiswahili primary to secondary.

Halafu unaandika upotolo unajificha kwenye usomi uchwara.

Kili umekosea na kwanini ukosee wakati ni mtanzania tena mswahili.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enzi za kuchaguliwa na TCU niliomba hii kitu kama passion yangu kuwa daktari mifugo as my first priority lakini TCU walijua walichonichagulia wao na PCB yangu ,though nashkuru Mungu hiko ndo kinanifanya napata nguvu ya kutype hapa na mengineyo japo nakumbuka nliumiaga sana.

Tuyaache hayo.........
naona wizara iangalie namna ya kufanya hapo......kufanya intern mwaka mzima bila chochote sio kitu rahisi. naelewa sababu nimebahatika kujitolea walau miezi mitatu kwenye mji wa watu .....nilishindwa aisee....πŸ™Œ

Serikali iliangalie hili Ione namna ya kuwasaidia ......
Pole ndugu kwa kuto kuchagiliwa, na hongera sana kwa sehemu uliopo sasa.

Kufanya intern mwaka mzima bila malipo, sio kazi rahisi. Wizara lazima ione namna ya kutusaidia
 
Acha weak defensive mechanisms..wewe ni msomi umesoma kiswahili primary to secondary.

Halafu unaandika upotolo unajificha kwenye usomi uchwara.

Kili umekosea na kwanini ukosee wakati ni mtanzania tena mswahili.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ndugu unanikosoa, wakati haujui matumizi ya nukta tu. Kajifunze kiswahili kwanza
 
Sasa kama hatuna umuhimu, na kwel hatuwezi kua sawa na MD. Kwanini watulazimishe kwenda internship?????

Sasa si watuache tupambane wenyewe mtaani kuliko kutulinganisha na fani zingine za afya.
Tuliwaambaia wakatupuuza wakati wa kuandaa hiyo Sheria, lakini wajitia ujanja. Pambaneni na Hali yenu! Vet doctors wanajisikia sana
 
Tuliwaambaia wakatupuuza wakati wa kuandaa hiyo Sheria, lakini wajitia ujanja. Pambaneni na Hali yenu! Vet doctors wanajisikia sana
Wala hatujisikii sana ndugu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.

Sema hayo mambo omba yasikutokee yana umiza sana (more than pain). Nahisi labda wahusika uko wizarani ndio wanajisikia sana.
Ila huku mtaani ( on the ground) hali ni tofauti kabisa. Tuna maisha magumu sana, mwaka mzima upo nyumbani na ujasajiliwa.

Na wanataka twende intern mwaka mzima bila hela ya kujikimu. Sasa tukienda intern wanataka tuishi kama majambazi, wezi au tukajifunze kuishi mwaka mzima bila kua na kitu.
 
Back
Top Bottom