Zamaradi Kawawa ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari - Maelezo

Kansigo

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,670
2,156
kawawa.jpg

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof Elisante Gabriel amemteua Zamaradi Kawawa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari - Maelezo.

Kawawa ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo, Assah Mwambene kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya NJe Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ambapo atapangiwa kazi nyingine.

1-1-jpeg.331493
 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Assah Mwambene Ahamishiwa Wizara Ya Mambo Ya Nje
 
Attachments

  • 1-1.jpeg
    1-1.jpeg
    52 KB · Views: 567
  • 1-1.jpeg
    1-1.jpeg
    52 KB · Views: 85
aliyekua mkurugenzi wa idara ya habari maelezo ndugu assah mwambene amehamishiwa wizara ya mambo ya nje ushirikiano wa africa mashariki na kikanda ambapo atapangiwa kazi nyingne huku zamaradi kawawa akiteuliwa kushikilia nafasi yake kwa sasa source clouds tv
 
jamaa walimwambia afungie gazeti la kufichua mafisadi yeye hakufanya hivyo.mwishowe ikapelekea sefue afukuzwe kibarua
 
Tulikuwa wote Ruvu JKT 1990/91 Operation Kambarage ingawa baada ya miezi mitatu alihamishiwa nadhani Lugalo/Mgulani. Nakumnbuka siku ya kwanza alipopewa Ugali kwa maharage alimwaga. Afande akamwambia kesho utaukumbuka huo ugali.

Atakulaje Ugali kwa Maharage Mtoto wa waziri mkuu jamani???
 
jamaa walimwambia afungie gazeti la kufichua mafisadi yeye hakufanya hivyo.mwishowe ikapelekea sefue afukuzwe kibarua

Mimi nadhani gazeti liliwapunguzia kazi kwa kuuambia umma mambo ambayo wao hawakuweza kuyafanya....
 
Tulikuwa wote Ruvu JKT 1990/91 Operation Kambarage ingawa baada ya miezi mitatu alihamishiwa nadhani Lugalo/Mgulani. Nakumnbuka siku ya kwanza alipopewa Ugali kwa maharage alimwaga. Afande akamwambia kesho utaukumbuka huo ugali.

Nafikiri alihamishiwa Mgulani au Mlalakuwa .
 
Back
Top Bottom