Zamani ilikuwa raha

Vijana mpooo....tupoooo ...tupo kabisa

jeuri ya chama...chini ya umoja wa vijana

yebaaa .....waaaa

………………………………


mwenge huooo..mwenge...mbio...mbio

mwenge tunaukimbiza mbio..mbio

mpaka makao makuu mbio...mbio

ZAMANI KULIKUWA NA KAUZALENDO TOFAUTI NA SASA,

TULIKUWA TUNAJIPANGA BARABARANI KUMSUBIRI RAIS AKIPITA.

ILA SIKU HIZI WATU HAWANA UJINGA HUO.
 
Moshi Tech walikuwa wanaitwa mafundi.
wengi walikuwa wanakuja wasukuma sasa kutongoza hawajui utaskia dhadha nimekudohndohkea (sukuma accent) ilikuwa ni shida.
vifua chuma walikuwa Ilboru manake walikuwa watanashati ila ukija Umbwe mweeeh wanywa mbege hao. walikuwa wanagionga mbege af wanaoshea na bia basi wanajiona vidumeee................
 

Ha ha ha.........yaani umegonga kwenyewe........longtime sana, unawakuta hao jamaa wa MoshiTech na zile raba za DH.....yaani unapomwona jibaba linakuja kukuomba mcheze unatamani uyeyuke....
 
wanawake walikalikiti nywele kwa kuchoma bati na kupitisha juu ya kichwa
 
Nakumbuka nyerere alipokuja huku tanangozi 1976 enzi za vijiji vya ujamaa kuna kiongozi alijilinda kwa wananchi kuhusu kunywa pombe akasema
UGIMBI MNYWESAGE ILA POMBE MSINYWE

AKASHANGILIWA KWELI NA WANANCHI.
 
siku za sikukuu kulikuwa na tamaduni za kupeana chakula hasa pilau, kama mimi ni mkristo na ni krismass lazima pilau ipikwe na niwagawie jirani zangu hasa ambao sio wakristo, na wao vileviile ikifika sikukuu yao wanafanya hivyo hivyo....
​umenikumbusha mbali sana, we used to do this..................aaahh those days;-)
 
Nakumbuka nyerere alipokuja huku tanangozi 1976 enzi za vijiji vya ujamaa kuna kiongozi alijilinda kwa wananchi kuhusu kunywa pombe akasema
UGIMBI MNYWESAGE ILA POMBE MSINYWE

AKASHANGILIWA KWELI NA WANANCHI.
nakumbuka kuna wazee walitoa kilita wakataka kumpatia ilikuwa iiishu..............me ni wa tanangozi pale barabarani kaka
 
Mnaikumbuka pool side kilimanjaro hotel
 
Tulikua tunaudhulia mashindano ya disco lan'gata social hall na harbour's club walikuepo mabingwa wa kucheza style mbalimbali. Mabingwa wetu kama akina savy pops akiwa kijana mdogo kabisa kuchukua ubingwa akitokea mitaa ya keko. Akina Black Moses kinondo, Ngedere Morogoro. Du!! Ilikua hatari natamani siku zingerudi nyuma.
 

Enzi za DJ Kalikali R.I.P na baadae akina Young millionnaire.....
 
Reactions: BAK

hizi hadithi zilikuwa zina mafunzo makubwa

nimewakumbuka Mr & Mrs Daudi, Baraka na Neema na Neema atakuwa ameolewa sasa
 
Kumbe zamani hamkuwa na raha yeyote...., uzuri ni kwamba, baada ya miaka 20 leo pia itaitwa zamani.

Siku hizi ndo hamna raha wakati huo kila kitu kilikuwa kinasisimua kwani havikuwa vinapatikana kila mahali kama leo. Wali wa maharage ulikuwa mtamu kuliko chipis mayai/kuku leo, hata uji usio na chochote ulikuwa mtamu kuliko uji wa asali leo
 
Tulicheza mpira wa makaratasi na shule nzima ilitushangilia kwa nguvu ikiwa pamoja na waalimu wetu.

Halafu asubuhi kabla ya masomo tulikimbia mchakamchaka huku tukiimba nyimbo nyingi kama vile:

Idd Amini akifa,
mimi siwezi kulia,
Nitamtupa Kagera,
awe chakula cha mamba.
 
Hapo nimekukubali mkuu, kuigiza miondoko ya akina Michael Jackson kama hutaki kukanyaga chini vile!! Miondoko ya kufokafoka ya akina Shaba Ranks utafikri wewe ndo unaimba!!
 
HIZO ZOTE NI HEKIMA NA BUSARA ZA BABA WA TAIFA,ati leo tuna madini,gesi na utalii..tunalipia Matibabu na elimu na maisha yamekua Kero kama sio nyoka mwenye makengeza basi utaomba ardhi ipasuke uingie!ndio maana nikasema tunatakiwa kama nchi si kusherehekea bali KUSIKITIKIA MIAKA 50 YA UHURU,tumuenzi Baba Nyerere!!
 
Hivi UKWATA bado upo kweli? Zamani ilikuwa raha sana shuleni. Nakumbuka nilipiga safari ya Kigoma kwa Tren, kule tulipokelewa na afisa elimu, huku una Orange Squash ya kunywa, na inapatikana RTC pekee. Tumetoka mbali.
 
Enzi hizo vitabu vilikuwa na chapa ya Prof Mtabaji, siku hizi ni Nyambari Nyangwine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…