SoC02 Zama za kujiajiri ni sasa

Stories of Change - 2022 Competition

Abdi kassimu

Member
Jul 25, 2022
7
2
Ajira: Ni kazi yoyote ambayo mtu anafanya kwa malipo katika kampuni, ofisi za serikali au kwa mtu mwingine binafsi.

KUJIAJIRI: ni ile hali ya kutegemea ajira Binafsi kuliko kutegemea kupewa Ajira na mtu Binafsi,kampuni au serikali.

NI ZIPI FAIDA ZA KUJIAJIRI.

1. Ni njia bora ya kukufikisha kwenye uhuru wa fedha.

Inawezekana ukawa umechoka na kazi unayoifanya na unaoina haifai kwa namna moja au nyingine. Lakini njia bora ya kuweza kuondokana na utumwa huo ambao unakukabili ni kuanzisha biashara yako mwenyewe ambayo utaisimamia mpaka ikuletee mafanikio unayoyahitaji.

2. Ni Njia bora ya kujifunza.
Hakuna njia bora ya kujifunza kuhusu kutunza na kumiliki pesa kama biashara. Hili ndilo eneo ambalo utajifunza mengi kuhusu masoko, namna ya kukuza mtaji na jinsi ambavyo unaweza ukaufikia uhuru wa kipesa. Kwa hiyo kama una biashara yako inakusaidia kujifunza yote hayo hatua kwa hatua.

3. Ni njia bora yakujifunza kujitegemea.
Unapokuwa kwenye ajira kwa kawaida unakuwa unamtegemea mtu fulani ambaye ndiye akuamulie juu ya maisha yako. Lakini kwenye biashara mambo hayako hivyo. Wewe ndiye unakuwa mwamuzi mkubwa wa maisha yako. Na unakuwa unakikisha unafanya kila linalowezeka mpaka biashara yako ifanikiwe.

4. Inakuwa inakupa hamasa ya mafanikio zaidi.
Huo ndiyo ukweli unaotakiwa ujue kuwa, unapokuwa na biashara inakuwa inakupa hamasa ya kuweza kufanikiwa na kusonga mbele zaidi. Tofauti na ajira ni rahisi kusema kuwa ‘aaah kazi yenyewe siyo yangu kwanza’ kwa hiyo unakuwa unafanya kwa jinsi unavyojisikia. Lakini kwenye biashara mambo hayako hivyo ni lazima kujituma ili kufanikiwa.

5. Inakuongezea ujasiri.
Unapokuwa mfanyabishara ni hatua nzuri sana kwako ya kukupelekea kuwa na ujasiri wa hali ya juu. Hiyo yote ni kwa sababu unapofanikiwa katika biashara moja unakuwa ndani yako una hamasa kubwa ya kutaka kufanya biashara nyingine tena kwa mafanikio. Kwa hali hiyo unakuwa una maamuzi mengi ya kijasiri ambayo ni rahisi kukusaidia kukusonga mbele.

6. Ni njia rahisi ya kufuata mipango na malengo yako.
Mara unapoanzisha biashara yako unakuwa upo kwenye njia sahihi ya kufuata ndoto za maisha yako. Hii yote ni kwa sababu unakuwa unakifanya kile kitu ambacho unakipenda kwa dhati toka moyoni mwako. Wakati unapokuwa kwenye ajira unakuwa unafanya tu ilimradi mkono uende kinywani. Hiyo ndiyo faida kubwa mojawapo ya kuwa kwenye biashara.

7. Inakufanya unakuwa ni mtu wa vitendo.
Watu wengi mara nyingi ni waongeaji bila ya kuwa watu wa vitendo. Lakini kitendo cha kuwa na biashara yako mwenyewe inakupelekea unakuwa ni mtu wa vitendo. Utaelewa vizuri umuhimu wa kuchukua hatua katika biashara tofauti na ambavyo ungekuwa hufanyi biashara ingekupelekea wewe kuwa na maneno mengi bila utekelezaji.


CHANGAMOTO ZINAZOTOKANA NA KUJIAJIRI.
Zipo sababu kadhaa za changamoto zinazotokana au zinazochangia watu wengii haswa vijana kutokujiajirii na sababu hizoo ni kama zifuatazoo.

1. Changamoto ya kukosa MTAJI.
Mtaji ni kianzio chochote Cha biashara kama vile fedha,sehemu ya kufanyia biashara na mashine au vitendea kazi vya kufanyia biashara. Swala hili ni changamoto kubwa kwa watu haswa wanaohitaji kuanzisha biashara.

2.Changamoto ya udhubutu.
Watu wengii wamekuwa si wa kudhubutu katika kuanzisha wa biashara wenye tija ya kujiajirii

3. Ukosefu wa elimu ya kibiashara.
Hili kimekuwa ni tatizo kubwaa saana haswa kwa vijana kukosa elimu ya namna ya kujiajirii na changamoto zinazoikumba sekta ya kujiajirii hiii inapelekeaa hata kama mtu Unakuwa na mtaji unaweza kuanzisha biashara na ikafa kwasababu tuu hauna elimu ya namna ya kujiajirii.

4. Vikwazo vya kiserikali.
Ni kweli serikali inasisitiza vijana kujiajirii lakini yenyewee inaweka vikwazo mbali mbali ambavyo vinapelekea kama mtu ana mtaji mdogo kushindwa kuwekezaa zaidi mfano changamoto ya upatikanaji wa leseni ya biashara ambayoo inawezesha kuendesha biashara.

NI KIPI KIFANYIKEE ILI KUHIMIZA VIJANA WENGI WATEGEMEE KUJIAJIRI KULIKO KUAJIRIWA.

1. Serikali kuweka Sheria ndogo ndogo za kutofautisha mfanyabiashara anayeanza na Yulee ambayee ni endelevu yaani wa muda mrefuu. Hiii ina maana ya kwamba serikali lazima iweke vikwazo vidogo vidogo kwa wafanyabishara walio endelevu kutofautiana na walee wanaoanza kwenye biashara hii itasaidiaa haswa watu wengii kujiajirii.

2. Serikali kutoa mikopo kwa wajasiriamali . Kiukweli hakuna mkopo unaotoka bila ya masharti ila lazima serikali iangaliee na iweke msharti nafuu kwa walee watu ambao ni wagenii yaani ndio kwaanza wanaingia kwenye biashara masharti nafuu kama kutumiaa vitambulisho haswa vya TAIFA katika kuombea mikopo.

3. Kutoa Elimu ya namna ya uendeshaji wa Biashara na changamoto zakee. Haswa mashuleni kuwepo na SoMo la ujasiriamali hili litawawezesha wanafunzi na raia wa kawaida katika kuanzisha biashara na kuwa wajasiriamali wenye MANUFAA MAKUBWA kwa nchi na TAIFA kwa ujumla.

USHAURI
Katika suala Zima la Elimu ya ujasiriamali Elimu zaidi inahitaji mfano kuwepo kwa SoMo la ujasiriamali ambalo litasaidiaa wanafunzi na watu wa kawaida kujua namna Gani ya kuwa wajasiriamali wazurii... Mfano kuwapa vipindi wajasiriamali waliofanikiwa kufundiaha SoMo la ujasiriamali vyuoni na mashuleni kwa lengo la kujua umuhimu wa ujasiriamali moja kwa mojaa tofauti na kusoma kwenye vitabuu Tuu.... Hiii italeta matokeo chanya kwenye kujiajiri .

MWISHO
" PAMBAZUKA SASA KUJIAJIRI NDIO HABARI YA LEO KWA MALENGO YA KESHO NA MANUFAA YA NCHI"
BY ABDI KASSIMU 0718733106
 
Back
Top Bottom