Zama za Haji Manara zipo ukingoni na asipokuwa makini zitalazimishwa kutamatika

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,067
6,193
Wakati mwingine ujuaji usio na kiasi huweza kumsababishia mhusika matatizo yasiyo ya lazima mbele ya safari ambayo pengine angefika salama.

Haji Manara kwa mfano. Bwana yule hujifanya anayo mengi ayatambuayo. Na kutokuwa kwake makini na ayasemayo, hatimaye yanaelekea kumfitinisha hata na waliopo kwenye mfumo ( serikalini).

Kwa msiofahamu, mapema jana, bwana Haji kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, alidai haoni mantiki ya timu za Taifa kuchangiwa na Wananchi ilhali gharama zote zihusuzo ushiriki wake kwenye mashindano mbalimbali yaliyo chini ya chama cha soka barani Afrika, hugharamikiwa na wao (CAF).

Huenda bwana Haji alikuwa sawa kutoa malalamishi yale, pengine.

Lakini unajiuliza, je, bwana yule hakugundua halibio lile lingewaathiri hata maswahibaye walio ndani ya mpango ule wa upigaji!? Kwamba, Haji hatambui tawi pekee (Serikali) linalomfanya aweze japo kubaki akining'inia asidondoke ndilo hilo ameanza kulitusi eti linamuumiza?

Hakika, naanza kuuona mwisho wa zama za Haji! Na akiendelea kufanya mchezo, hata hizo zama zilizopo ukingoni-zitawahishwa na ujuaji wake usio na kiasi.

Acha muda/mda uwe Mwalimu.
 
Ana hoja asikilizwe,,,ni aibu kubwa kwa timu ya taifa kupitisha bakuli kwa wanainchi..

Serikali imejaza watu wengi kwenye msafara wa timu ya taifa ambao hawana faida zozote,,
Halafu mnawabebesha wanainchi mzigo wa gharama.
Sijawahi kuona dunia kote kwenye msafara wa timu imejaza wanasiasa na wacheza comedy balada ya kujaza football veterans.

Manara ana hoja asipuuzwe .
 
Wakati mwingine ujuaji usio na kiasi huweza kumsababishia mhusika matatizo yasiyo ya lazima mbele ya safari ambayo pengine angefika salama.

Haji Manara kwa mfano. Bwana yule hujifanya anayo mengi ayatambuayo. Na kutokuwa kwake makini na akisemacho, hatimaye yanaelekea kumfitinisha hata na waliopo kwenye mfumo ( serikalini).

Kwa msiofahamu, mapema jana, bwana Haji kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, alidai haoni mantiki ya timu za Taifa kuchangiwa na Wananchi ilhali gharama zote zihusuzo ushiriki wake kwenye mashindano mbalimbali yaliyo chini ya chama cha soka barani Afrika, hugharamikiwa na wao (CAF).

Huenda bwana Haji alikuwa sawa kutoa malalamishi yale, pengine. Lakini unajiuliza, je, bwana yule hakugundua halibio lile lingewaathili hata maswahibaye walio ndani ya mpango ule wa upigaji!? Kwamba, Haji hatambui tawi pekee ( Serikali ) linalo mfanya aweze japo kubaki akining'inia asidondoke ndilo hilo ameanza kulitusi eti linamuumiza!?

Hakika, naanza kuuona mwisho wa zama za Haji! Na akiendelea kufanya mchezo, hata hizo zama zilizopo ukingoni-zitawahishwa na ujuaji wake usio na kiasi.

Acha muda/mda uwe Mwalimu.
Hua nipo against Haji ila kwa hilo nipo nae
 
Ana hoja asikilizwe,,,ni aibu kubwa kwa timu ya taifa kupitisha bakuli kwa wanainchi..

Serikali imejaza watu wengi kwenye msafara wa timu ya taifa ambao hawana faida zozote,,
Halafu mnawabebesha wanainchi mzigo wa gharama.
Sijawahi kuona dunia kote kwenye msafara wa timu imejaza wanasiasa na wacheza comedy balada ya kujaza football veterans.

Manara ana hoja asipuuzwe .
Naunga mkono hoja ana hoja asikilizwe,
 
Tatizo la haji anazeeka vibaya kwanza kwa umri wake anatakiwa busara zake ziongee zaidi kuliko sifa zake zakijinga, haji anadharau, anakiburi na jeuri, hana nidhamu....ndio maana simba walimtimua na ndio maana kila mwanamke anaemuoa anamkimbia....haji anashida
 
Tz ukisema ukweli unakuwa adui wa chawa wa watawala?, Ungekuja na hoja ya kupinga hoja ya manara ungeeleweka ila umekuja na chuki binafsi dhidi ya Manara!!. Je Kama anayajua asiseme?.... Njooni mjibu hoja acheni kutafuta huruma ya watu kwa Jambo hili. Nchi mpaka inaanda mashindano bado mnategemea kuomba michango ya raia?.
 
Back
Top Bottom