Zali la Mentali

Zali la Mentali

Utaota kisengesi tu kesho utaota unamwambia ntu ntom!b!e unakuta shipa limezama tigoni full utelezi kama umemwagiwa bamia

Ndugu yangu naona umepanik...jinsi unavyoandika ni kama shabiki wa yanga unakimbia uwanja wa taifa baada ya kipigo.. Tuliaaa acha wenge..Btw kama una huo mchezo mchafu pole sana ndugu.. Tutakupeleka India ukapigwe bomba ..
 
ulivuta bange ya Arusha au Malawi? eeeh vipi hukuota na ndoto nyevu ya mchana hapo hapo ukapiga Goal...!!mchana kweupe...

Ndugu yangu bangi uniuzie mwenyewe halafu usahau tena ni ya wapi? Anyways ni ya Arusha..
 
Ni majira ya saa 10 jioni nikitoka zangu Morogoro kwenye usaili narudi zangu Dar ninapoishi.. Kutokana na ugumu wa maisha, nimebakiwa na shilingi 3000 tu mfukoni hapo nikiwaza chakula cha jioni pamoja na nauli ya daladala..tena ukizingatia Mbagala ilivyo mbali.. Nikajipa moyo siku itapita.

Tulipofika Chalinze, basi lilisimama na akapanda mrembo mmoja matata sana, umri kati ya miaka 24 hadi 26, mwenye urefu wa wastani, mweupe, mwembamba kiasi huku akiwa ametupia suruali ya jinsi pamoja na t shirt iliyomkaa vizuri na kuonesha umbo lake maridhawa la namba nane. Akaja akaketi kwenye siti iliyopo pembeni mwangu kwa kuwa kabla ya kufika chalinze, abiria aliyekuwa amekaa jirani yangu alishuka.. Basi tukasalimiana na safari ikaendelea.

Akajitambulisha anaitwa Angel.. Mimi nikamwambia naitwa Eric. Basi tukapiga stori nyingi sana.. Tulipokaribia kufika Mbezi akaniaga akasema atashuka kituo cha mbezi mwisho kwani ndipo anapoishi. Basi nikamuaga..tukabadilishana namba za simu.. Kwa kweli alikuwa mcheshi sana na nilifurahi mno kupata namba zake.. Basi baada ya kufika Ubungo wakati natoa mizigo yangu sehemu ya kuhifadhia, nikaona pochi ya kike.

Nikakumbuka angel nae aliweka mizigo yake pale..nikasema hebu nifungue niangalie ndani.. Heeeeh nikakuta pesa nyingi sana za kitanzania pamoja na Dola za marekani nyingi sana pamoja na vitambulisho vya angel.. Nikajiuliza, je nimpigie au nipotezee nisepe na mkwanja?? Wakati nawaza hayo ghafla nikaona simu inaita..Jina ni Angel... Dah..nikawazaaa huku inaita..nikaamua tu kupokea,

"Hallo, samahani Erick eti umeona pochi yangu hapo hata sijui nimeipoteza wapi"
Nikamjibu " Yah Angel ndo nimeiona sasa hivi nashuka Ubungo hapa nikawa nataka nikupigie"

"Ooooh thanks God! Yaan you can keep hizo hela but please naomba nihifadhie vitambulisho vyangu ni muhimu mno yani"
"Whaaat?? Hela zote hizi? Are you serious?"

"Yah, why not? Cha msingi naomba nitunzie tu vitambulisho ntavifuta vyote.."
"Sawa, usiku mwema Angel, ahsantee"
"Usijali.. Usiku mwema pia"

Dah, ni kama nilichanganyikiwa ghafla.. Zile pesa hazipungui kama Milioni 5 hivi... Yaani zangu zote??? Nikaona ni zali la mentali.

Nikawa nawaza, sijui nikodishe Taxi? Au nilale Blue Pearl hadi kesho? Wakati nawaza hayo, mara nasikia..

"We Eric Umejilaza tu hapo kwenye mkeka maharage hata huangalii, hivi umeongeza mkaa kweli? Na yakiungua hayo utakula ugali na chumvi..."

Dah, mama yangu kaniamsha nilikuwa ndotoni, tena usingizi wa mchana..Duuh!!!

Ha ha ha haaaa nimecheka sana Mkuu.
 
ulivuta bange ya Arusha au Malawi? eeeh vipi hukuota na ndoto nyevu ya mchana hapo hapo ukapiga Goal...!!mchana kweupe...

Huyu alichanganya goto na mavi ya kuku...

Akapiga pafu kadhaa kabla ya kuangusha...
 
Mkuu una kipaji kilichojificha! nimecheka sana na kuifanya siku yangu kuanza vizuri,Tunga kama hizi kadhaa tengeneza kijitabu chenye finishing na cover page nzuri utauza na utakuwa milionea amini nakuambia!
 
siku nyingine ukilala mchana tafuta sehemu nzuri ya kujificha ili wasikatishe ndoto zako, ona sasa wala hujafaidi mapesa yako, alafu ndoto ingeendelea walahi mtoto ungemgegeda kilaiini, by the way namba yake si uliisevu? sasa kwa nini usiku ulivyo lala hukumpigia tena ili uendelezee ulipoishia. siku nyingine ukiota ndoto za mikwanja, kimbiza kwanza bank ili uwe unainjoi kwenye ndoto na mifweza yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom