Zali la Mentali

Magnesium

JF-Expert Member
Nov 9, 2014
317
250
Ni majira ya saa 10 jioni nikitoka zangu Morogoro kwenye usaili narudi zangu Dar ninapoishi.. Kutokana na ugumu wa maisha, nimebakiwa na shilingi 3000 tu mfukoni hapo nikiwaza chakula cha jioni pamoja na nauli ya daladala..tena ukizingatia Mbagala ilivyo mbali.. Nikajipa moyo siku itapita.

Tulipofika Chalinze, basi lilisimama na akapanda mrembo mmoja matata sana, umri kati ya miaka 24 hadi 26, mwenye urefu wa wastani, mweupe, mwembamba kiasi huku akiwa ametupia suruali ya jinsi pamoja na t shirt iliyomkaa vizuri na kuonesha umbo lake maridhawa la namba nane. Akaja akaketi kwenye siti iliyopo pembeni mwangu kwa kuwa kabla ya kufika chalinze, abiria aliyekuwa amekaa jirani yangu alishuka.. Basi tukasalimiana na safari ikaendelea.

Akajitambulisha anaitwa Angel.. Mimi nikamwambia naitwa Eric. Basi tukapiga stori nyingi sana.. Tulipokaribia kufika Mbezi akaniaga akasema atashuka kituo cha mbezi mwisho kwani ndipo anapoishi. Basi nikamuaga..tukabadilishana namba za simu.. Kwa kweli alikuwa mcheshi sana na nilifurahi mno kupata namba zake.. Basi baada ya kufika Ubungo wakati natoa mizigo yangu sehemu ya kuhifadhia, nikaona pochi ya kike.

Nikakumbuka angel nae aliweka mizigo yake pale..nikasema hebu nifungue niangalie ndani.. Heeeeh nikakuta pesa nyingi sana za kitanzania pamoja na Dola za marekani nyingi sana pamoja na vitambulisho vya angel.. Nikajiuliza, je nimpigie au nipotezee nisepe na mkwanja?? Wakati nawaza hayo ghafla nikaona simu inaita..Jina ni Angel... Dah..nikawazaaa huku inaita..nikaamua tu kupokea,

"Hallo, samahani Erick eti umeona pochi yangu hapo hata sijui nimeipoteza wapi"
Nikamjibu " Yah Angel ndo nimeiona sasa hivi nashuka Ubungo hapa nikawa nataka nikupigie"

"Ooooh thanks God! Yaan you can keep hizo hela but please naomba nihifadhie vitambulisho vyangu ni muhimu mno yani"
"Whaaat?? Hela zote hizi? Are you serious?"

"Yah, why not? Cha msingi naomba nitunzie tu vitambulisho ntavifuta vyote.."
"Sawa, usiku mwema Angel, ahsantee"
"Usijali.. Usiku mwema pia"

Dah, ni kama nilichanganyikiwa ghafla.. Zile pesa hazipungui kama Milioni 5 hivi... Yaani zangu zote??? Nikaona ni zali la mentali.

Nikawa nawaza, sijui nikodishe Taxi? Au nilale Blue Pearl hadi kesho? Wakati nawaza hayo, mara nasikia..

"We Eric Umejilaza tu hapo kwenye mkeka maharage hata huangalii, hivi umeongeza mkaa kweli? Na yakiungua hayo utakula ugali na chumvi..."

Dah, mama yangu kaniamsha nilikuwa ndotoni, tena usingizi wa mchana..Duuh!!!
 
Rich Pol

JF-Expert Member
Oct 11, 2013
7,836
2,000
Ukame wa hela mbaya sana. Pile sana zidisha juhudi omba na mungu utapata za kwako.
 
mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,756
2,000
ulivuta bange ya Arusha au Malawi? eeeh vipi hukuota na ndoto nyevu ya mchana hapo hapo ukapiga Goal...!!mchana kweupe...
 
Kipilipili

JF-Expert Member
May 25, 2010
2,246
2,000
Lala tena umalizie ndoto huenda Angle akifuata ID's zake akakupa "zawadi ya ushindi".
 
luckyline

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
11,241
2,000
Ni majira ya saa
10 jioni nikitoka zangu Morogoro kwenye usaili narudi zangu Dar
ninapoishi.. Kutokana na ugumu wa maisha, nimebakiwa na shilingi 3000 tu
mfukoni hapo nikiwaza chakula cha jioni pamoja na nauli ya
daladala..tena ukizingatia Mbagala ilivyo mbali.. Nikajipa moyo siku
itapita.

Tulipofika Chalinze, basi lilisimama na akapanda mrembo mmoja matata
sana, umri kati ya miaka 24 hadi 26, mwenye urefu wa wastani, mweupe,
mwembamba kiasi huku akiwa ametupia suruali ya jinsi pamoja na t shirt
iliyomkaa vizuri na kuonesha umbo lake maridhawa la namba nane. Akaja
akaketi kwenye siti iliyopo pembeni mwangu kwa kuwa kabla ya kufika
chalinze, abiria aliyekuwa amekaa jirani yangu alishuka.. Basi
tukasalimiana na safari ikaendelea.

Akajitambulisha anaitwa Angel.. Mimi nikamwambia naitwa Eric. Basi
tukapiga stori nyingi sana.. Tulipokaribia kufika Mbezi akaniaga akasema
atashuka kituo cha mbezi mwisho kwani ndipo anapoishi. Basi
nikamuaga..tukabadilishana namba za simu.. Kwa kweli alikuwa mcheshi
sana na nilifurahi mno kupata namba zake.. Basi baada ya kufika Ubungo
wakati natoa mizigo yangu sehemu ya kuhifadhia, nikaona pochi ya kike.

Nikakumbuka angel nae aliweka mizigo yake pale..nikasema hebu nifungue
niangalie ndani.. Heeeeh nikakuta pesa nyingi sana za kitanzania pamoja
na Dola za marekani nyingi sana pamoja na vitambulisho vya angel..
Nikajiuliza, je nimpigie au nipotezee nisepe na mkwanja?? Wakati nawaza
hayo ghafla nikaona simu inaita..Jina ni Angel... Dah..nikawazaaa huku
inaita..nikaamua tu kupokea,

"Hallo, samahani Erick eti umeona pochi yangu hapo hata sijui
nimeipoteza wapi"
Nikamjibu " Yah Angel ndo nimeiona sasa hivi nashuka Ubungo hapa nikawa
nataka nikupigie"

"Ooooh thanks God! Yaan you can keep hizo hela but please naomba
nihifadhie vitambulisho vyangu ni muhimu mno yani"
"Whaaat?? Hela zote hizi? Are you serious?"

"Yah, why not? Cha msingi naomba nitunzie tu vitambulisho ntavifuta
vyote.."
"Sawa, usiku mwema Angel, ahsantee"
"Usijali.. Usiku mwema pia"

Dah, ni kama nilichanganyikiwa ghafla.. Zile pesa hazipungui kama
Milioni 5 hivi... Yaani zangu zote??? Nikaona ni zali la mentali.

Nikawa nawaza, sijui nikodishe Taxi? Au nilale Blue Pearl hadi kesho?
Wakati nawaza hayo, mara nasikia..

"We Eric Umejilaza tu hapo kwenye mkeka maharage hata huangalii, hivi
umeongeza mkaa kweli? Na yakiungua hayo utakula ugali na chumvi..."

Dah, mama yangu kaniamsha nilikuwa ndotoni, tena usingizi wa
mchana..Duuh!!!
kweli hii weekend.
 
deepsea

JF-Expert Member
Aug 10, 2013
3,292
1,500
Utaota kisengesi tu kesho utaota unamwambia ntu ntom!b!e unakuta shipa limezama tigoni full utelezi kama umemwagiwa bamia
 
love more than100

JF-Expert Member
Jan 27, 2014
2,066
1,500
Ni majira ya saa 10 jioni nikitoka zangu Morogoro kwenye usaili narudi zangu Dar ninapoishi.. Kutokana na ugumu wa maisha, nimebakiwa na shilingi 3000 tu mfukoni hapo nikiwaza chakula cha jioni pamoja na nauli ya daladala..tena ukizingatia Mbagala ilivyo mbali.. Nikajipa moyo siku itapita.

Tulipofika Chalinze, basi lilisimama na akapanda mrembo mmoja matata sana, umri kati ya miaka 24 hadi 26, mwenye urefu wa wastani, mweupe, mwembamba kiasi huku akiwa ametupia suruali ya jinsi pamoja na t shirt iliyomkaa vizuri na kuonesha umbo lake maridhawa la namba nane. Akaja akaketi kwenye siti iliyopo pembeni mwangu kwa kuwa kabla ya kufika chalinze, abiria aliyekuwa amekaa jirani yangu alishuka.. Basi tukasalimiana na safari ikaendelea.

Akajitambulisha anaitwa Angel.. Mimi nikamwambia naitwa Eric. Basi tukapiga stori nyingi sana.. Tulipokaribia kufika Mbezi akaniaga akasema atashuka kituo cha mbezi mwisho kwani ndipo anapoishi. Basi nikamuaga..tukabadilishana namba za simu.. Kwa kweli alikuwa mcheshi sana na nilifurahi mno kupata namba zake.. Basi baada ya kufika Ubungo wakati natoa mizigo yangu sehemu ya kuhifadhia, nikaona pochi ya kike.

Nikakumbuka angel nae aliweka mizigo yake pale..nikasema hebu nifungue niangalie ndani.. Heeeeh nikakuta pesa nyingi sana za kitanzania pamoja na Dola za marekani nyingi sana pamoja na vitambulisho vya angel.. Nikajiuliza, je nimpigie au nipotezee nisepe na mkwanja?? Wakati nawaza hayo ghafla nikaona simu inaita..Jina ni Angel... Dah..nikawazaaa huku inaita..nikaamua tu kupokea,

"Hallo, samahani Erick eti umeona pochi yangu hapo hata sijui nimeipoteza wapi"
Nikamjibu " Yah Angel ndo nimeiona sasa hivi nashuka Ubungo hapa nikawa nataka nikupigie"

"Ooooh thanks God! Yaan you can keep hizo hela but please naomba nihifadhie vitambulisho vyangu ni muhimu mno yani"
"Whaaat?? Hela zote hizi? Are you serious?"

"Yah, why not? Cha msingi naomba nitunzie tu vitambulisho ntavifuta vyote.."
"Sawa, usiku mwema Angel, ahsantee"
"Usijali.. Usiku mwema pia"

Dah, ni kama nilichanganyikiwa ghafla.. Zile pesa hazipungui kama Milioni 5 hivi... Yaani zangu zote??? Nikaona ni zali la mentali.

Nikawa nawaza, sijui nikodishe Taxi? Au nilale Blue Pearl hadi kesho? Wakati nawaza hayo, mara nasikia..

"We Eric Umejilaza tu hapo kwenye mkeka maharage hata huangalii, hivi umeongeza mkaa kweli? Na yakiungua hayo utakula ugali na chumvi..."

Dah, mama yangu kaniamsha nilikuwa ndotoni, tena usingizi wa mchana..Duuh!!!
Kweeeendaaa eti zali la mentali wkt ni zali la usingizi wa njaa mchana!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom