Zaidi ya watu 700 wafa kwa joto Canada

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Joto kali limeua watu 700 magharibi mwa Canada

Karibu watu 719 wanakadiriwa kupoteza maisha kufuatia joto kali la kuvunja rekodi ambalo linaendelea kushuhudiwa magharibi mwa Canada katika msimu wa joto mwaka huu huku idadi hiyo ikitabiriwa kuongezeka.

Idara ya Uchunguzi wa Vifo katika jimbo la British Colombia inasema wiki iliyopita pekee kuliripotiwa vifo 719 hii ikiwa ni mara tatu zaidi ya wastani wa vifo wakati huu kila mwaka.

Afisa mkuu wa uchunguzi wa vifo katika eneo hilo Lisa Lapointe amesema inaaminika kuwa aghalabu ya watu hao wamepoteza maisha kutokana na joto kali katika jimbo la British Colombia.

Jumanne iliyopita, kiwango cha nyuzi joto nchini Canada kiliongezeka zaidi kwa siku ya tatu mfululizo, huku nyuzijoto 49.5 zikinakiliwa katika maeneo ya Lytton na British Columbia. Kabla ya wiki hii, kiwango cha joto cha Canada hakikuwahi kuvuka nyuzijoto 45.

Maeneo mengine duniani, hasa sehemu za kaskazini tayari zinapata hali ya kipekee ya msimu wa majira ya joto kuanzia Afrika Kaskazini, hadi Rasi ya Arabia na Ulaya ya Mashariki na pia baadhi ya maeneo ya kusini mwa Irani na kaskazini magharibi mwa bara la India. Joto la juu la kila siku linazidi nyuzi joto 45 ° C na katika maeneo kadhaa hata hufikia nyuzijoto 50° C . Magharibi mwa Russia na maeneo ya karibu na bahari ya Kaspi pia yamepata hali ya joto isiyo ya kawaida.

Hivi karibuni, Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO lilitoa tahadhari kwamba joto la kupita viwango vya wastani litarajiwe kwenye sehemu nyingi duniani katika miezi michache ijayo.
 
Joto kuanzia November hapa Dar na mikoa yenye joto mwaka huu itakuwa ni balaa.
 
Back
Top Bottom