Zaidi ya 90 Wafariki Wakichota Mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zaidi ya 90 Wafariki Wakichota Mafuta

Discussion in 'International Forum' started by Babuji, Feb 1, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zaidi ya watu 90 waliokuwa wakichota mafuta kutoka kwenye lori la mafuta lilopinduka katika mji wa Molo nchini Kenya wamefariki kwa kuungua vibaya baada ya lori hilo la mafuta kulipuka.

  Watu 50 kati yao waliungua vibaya mpaka kugeuka mkaa hali iliyofanya maiti zao kushindwa kutambulika.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana zilisema kuwa moto huo ulizuka baada ya mamia ya watu kukusanyika kukusanya mafuta ya petrol yaliyomwagika baada ya lori kupinduka katika mji wa Molo na lori hilo kulipuka.

  Watu wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya na moto huo. Idadi ya vifo kutokana na moto inategemewa kuongezeka.

  Sababu ya moto huo haijajulikana ingawa baadhi ya taarifa zinasema kuwa moto huo ulisababishwa na sigara huku taarifa zingine zikisema kuwa moto huo ulianzishwa makusudi na mtu aliyezuiliwa na polisi kwenda kuchota mafuta hayo.

  "Watu walimiminika kwenda kukusanya petrol, baada ya hapo moto mkubwa ulizuka , inawezekana kuna mtu aliwasha sigara" alisema Titus Mung'ou msemaji wa Red Cross nchini Kenya.

  Source: http://www.nifahamishe.com
   
 2. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mungu awalaze pema, yaani hii habari imenikumbusha Tanzania Katika kijiji cha MNISONGOLE ilikuwa kama hivi du!
   
 3. B

  Babuji Senior Member

  #3
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana lakini yote ni kwasababu ya umaskini wetu
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii ajali ni kubwa sana, watu 90. Mola awape nguvu wafiwa na pia roho za marehemu azilaze pema.
   
 5. B

  Babuji Senior Member

  #5
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli moto wa Petroli noma! angalia mabaki ya gari

  [​IMG]

  Mmoja wa walionusurika

  [​IMG]

  Photo Source: Daily Nation Kenya
   
 6. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #6
  Feb 1, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  A Nakuru Municipal Council fireman battles with a massive from an oil tanker that had on Saturday evening burst into flames near Molo town. Inset, Red Cross personnel assisting victims of the fire which occurred near Jolly Farm on the Nakuru-Eldoret highway at about 7.30 pm.

  [​IMG]

  [​IMG]

   
 7. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #7
  Feb 1, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli umaskini unachangia kiwango f'lani katika hii mikosi maana watu
  waliona dili kupata mafuta ya bwerere kumbe kifo kinawakodolea macho.

  Poleni wafiwa na Mungu awape faraja.
  Amin.
   
 8. B

  Babuji Senior Member

  #8
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo mzee unanikumbushia wakati ule yule mtangazaji wa ITV sijui ni Pascal Mayala vile wakati akielezea tukio lile alichomekea " Wakazi wa kijiji hicho wenye madumu, ndoo, masufuria mpaka vijiko walikimbilia kujichotea mafuta ya bure
  "
  kabla hawajaungua baada ya moto kulipuka baada ya mshenzi mmoja kutaka kuiba betri la lile lori na kusababisha cheche zilizosababisha moto ule
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, idadi imeshaongezeka, sasa waliofariki wamefikia 110
   
 10. T

  Tango Member

  #10
  Feb 1, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Tunawapa pole ndugu zetu hawa. Kuna jambo la kujifunza kwenye hili, kutokimbilia kwenye ajali yeyote hata kama kuna uwezekano wa kupata dili.
   
 11. T

  Tango Member

  #11
  Feb 1, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Huyo nafikiri ni yule Mzee wa kusimulia mambo. Anaitwa Winfred MASAKO kama sijakosea
   
 12. B

  Babuji Senior Member

  #12
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yah swadakta ni Winfred MASAKO unajua tena long time
   
 13. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Huu pia ni uzembe kwa serekali ya wakenya, all these lives could have been saved. Ajali kama hizi zinapotokea kama wanausalama hawata act kuwazuia wananchi wasisogee katika eneo la tukio, majanga kama haya yataendelea kutuangamiza. Mara nyingi nimeshuhudia jinsi police wa nchi za wenzetu wenye maendeleo jinsi walivyo sharp ku cordon off maeneo ya matukio hata kama yawe madogo kiasi gani, kwanini hatujifunzi?
   
 14. B

  Babuji Senior Member

  #14
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uzembe mwingine unaotukabili ni kuchelewa eneo la tukio, hauwezi ukauacha moto wa petroli uwake masaa kadhaa halafu utegemee kuokoa mtu!
   
 15. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  siku zote, faida ya wizi ni matatizo. mshahara wa dhambi ni mauti. kama wewe unaona mafuta sio yako, kwanini unataka kuyachukua? kwanini unapenda kudhulumu kitu cha mtu? nani aliwaruhusu wachote hayo mafuta badala ya kumwonea huruma mfanyabiashara mwenzao anayepoteza mafuta wenyewe wanataka kuchota kama kisima bweleleee, walitegemea nini? hilo ni fundisho si kwa mafuta tu, bali katika kila kitu katika maisha. duniani kuna njia mbili, ya usima na ya kifo. ukitaka kutafuta njia ya uzima, jitahidi kutenda mema na kuepuka dhuluma, ukitaka kufa mapema we uwe mwizimwizi,fisadi,na mtenda maovu. utakufa siku si zako na hauna wa kumlaumu, ni moja ya maisha. wamekufa, wametangulia, sisis tuliobaki ndo iwe fundisho, na si kwa mafuta tu, bali katika kila jambo katika maisha.
   
 16. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Ubungoubungo,
  Mafuta waliyokuwa wakichota hawa wakenya yalikuwa yamemwagika na mengine yalikuwa yanaendelea kumwagika, sidhani kama huu ni wizi.Haya mafuta yalikuwa yanaishia aridhini na mwenye mzigo hakuwa na cha kufanya.
  Sijui kama sheria za kwenye meli zina apply kwenye magari pia lakini ninachojua ni kwamba (kwa meli) kama ajali imetokea ie mali imezama au kupinduka na mizigo kuelea ni rukhsa mtu yeyote kuchukua ili mradi tu atoe details zake ili iwapo mwenyewe ataamua ku claim mzigo wake ajue pa kuupata.
  Naona umegusia dini tena hapo lakini bado nashangaa kama unajaribu kusema kuwa watenda mema huwa hawafi! Na nawajua wezi wa kupindukia ambao wameishi zaidi ya miaka 90. Hitler na maovu yake yote naskia aligonga aka 100!
   
 17. B

  Babuji Senior Member

  #17
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :mad: Idadi ya waliofariki kwa moto wa lori la mafuta yafikia 111

  Idadi ya watu waliofariki kwa moto wakichota mafuta ya petroli yaliyomwagika kutoka kwenye lori lililopinduka katika mji wa Molo, nchini Kenya na baadae kulipuka wamefikia 111 huku zaidi ya watu wengine 200 wamejeruhiwa vibaya kutokana na moto huo.

  "Kila mtu alikuwa akikimbia huku akipiga kelele, wengi wao wakiwa wanakimbia huku wanaendelea kuungua, walikuwa wakikimbilia kuelekea kwenye vichaka" alisema Charles Kamau, 22, aliyekuwa akiendesha gari lake kupitia mji wa Molo na kukuta barabara ikiwa haipitiki baada ya mamia ya watu waliokuwa wakipigania kuchota mafuta ya petroli yaliyomwagika toka kwenye lori hilo kuzuia barabara.

  source: Nifahamishe.com
   
 18. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu babuj nafikiri ni Winfred Masako
   
 19. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #19
  Feb 1, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Be warned that some of the pictures are graphic:

  [media]http://news.yahoo.com/nphotos/Deadly-Kenya-Oil-Fire/ss/events/wl/020109kenyaoilfire#photoViewer=/090201/ids_photos_wl/r3048558511.jpg[/media]
   
 20. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #20
  Feb 1, 2009
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Man started fire after arguing with police


  [​IMG]

  Updated 1 hr(s) 4 min(s) ago

  By Amos Kareithi and Steve Mkawale

  When a drunken man threatened to light a fire, nobody took him seriously as police officers manning the scene charged those scooping free oil.

  Shortly after, the man walked a few steps and struck the match that set off a fire that burnt 110 people dead in Sachang’wan, Molo District.

  "The GSU officers were selling petrol. They allowed those who could part with Sh100 fetch petrol from the overturned ranker. Those who refused to pay were violently chased away," Mr Simon Korir recalls.

  Korir, who is nursing burns at Molo Sub District Hospital, narrates how he watched the scramble for fuel from a distance, as he had no money.

  "The police dared him to do as he pleased, while they pocketed money from those siphoning petrol. Immediately the stick flared, the man and everybody else were engulfed in a mighty flame. I tried to run but I could not outrun the fire," he says.


  Issued threat

  Another witness alleged that a resident, who differed with GSU officers, started the fire.

  "The man was angry at the GSU officers who were stopping people from siphoning the fuel. I overheard him tell the GSU: "Mtaona ikiwa munanikataza kuchota mafuta (I will teach you a lesson if you deny me permission to tap the fuel)," said Mr John Kamau, a motorcycle taxi operator.

  Most bodies at the scene were those of women and children who were drawing the spilled fuel from a roadside trench where the tanker had landed.

  Mr Kamau, who had just arrived at the scene, told The Standard that the fire broke out soon after the man issued the threat.

  "Even the person who issued the threats must have died in the ensuing fireball," he said.

  Kamau said he was called at the scene by a friend but only escaped the tragedy because he had no container to siphon the fuel.

  Police, accompanied by Rift Valley PC Hassan Noor Hassan and Kenya Red Cross Society officials had by yesterday morning counted 91 charred bodies at the scene.

  Another 20 were said to have succumbed to injuries at the Rift Valley Provincial General Hospital and other facilities where volunteers took them for treatment.

  More bodies

  "There are more bodies in the forest. Those were people who tried to flee as they carried siphoned petrol," said a traffic policeman who was among the first to arrive at the scene.

  The officer said those who died were soaked in petrol.

  "Their clothes were soaked in petrol so they could not escape when the fire broke out," he said.

  Two vehicles, whose owners had stopped at the accident scene to witness the incident, were also burnt. In one of the vehicles was the body of a man in handcuffs.

  The Standard team witnessed the counting at the scene on Saturday night after firefighters from the Nakuru Municipal Council put out the blaze.

  The fire that started as the victims scrambled for petrol has devastated Molo residents. And they were stunned to learn the inferno was allegedly started deliberately.

  Mr Michael Siele, said his brother, Peter Malakwen Kibenei may have died in the fire.

  "We arrived together and since I had nothing to carry the fuel, I rushed to the centre to look for one only to hear a loud explosion," he said.

  Siele was among hundreds of the fire victims’ relatives who kept vigil at the scene waiting for police to collect the mutilated bodies.

  "I cannot reach my brother on the phone and his wife keeps on calling me," he sobbed.

  Hanging from matatu

  Ms Rose Koech, 47, said she last saw her son, Robert Cheruiyot, hanging from a matatu and a jerrican in hand. "I hope he is among the survivors," she said.

  Another survivor, Rashid Baraka, 19, recounts how he went to the accident scene only to discover that he had left his wallet at home and had to watch as his colleagues’ fetch petrol.

  After realising he had only seconds to live, Baraka like hundreds of other villagers took to the forest and rolled on the ground. He got burnt on the feet and hands.

  Some of the people who were carrying jerricans full of looted petrol died in a forest by the roadside as they attempted to flee from the fire.

  A group of children from a local school were said to be among the dead. Their driver had stopped their car to witness the accident.

  At least 92 people, among them 10 officers from a nearby GSU camp were admitted to various hospitals.

  "More than 90 people have been taken to hospitals in Molo, Rongai and Nakuru. We have made arrangements for some to be transferred to Nairobi for specialised treatment," said Mr Hassan.

  The Standard | Online Edition :: Man started fire after arguing with police
   
Loading...