Lori la mafuta lalipuka na kusababisha vifo vya watu wanane Kusini Magharibi mwa Nigeria

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,139

Lori la mafuta lalipuka na kusababisha vifo vya watu wanane kusini magharibi mwa Nigeria​

Lori la mafuta lalipuka na kusababisha vifo vya watu wanane kusini magharibi mwa Nigeria.jpg


AFPCopyright: AFP

Takriban watu 8 wamethibitishwa kufariki kutokana na mlipuko wa lori la mafuta katika jimbo la Ondo Kusini Magharibi mwa Nigeria baada ya wakaazi kuchota mafuta kutoka kwa lori hilo lililopata ajali ya barabarani Jumapili usiku.

Kamanda wa polisi wa jimbo la Ondo amesema lori lililokuwa limepakia mafuta lilianguka kando ya barabara, na mafuta karibu yote yakimwagika kabla ya wakaazi kukimbilia eneo la tukio kuchukua mafuta.

"Lori hiyo ya mafuta ililipuka yenyewe na kuua watu 8 huku wengine wengi wakijeruhi ambao kwa sasa wanatibiwa hospitalini" msemaji wa Polisi aliambia BBC.

Wakaazi na walioshuhudia wanasema lori hilo lililipuka katika mtaa ulio karibu na kituo cha mafuta, na jengo la kanisa lakini hakuna aliyeathiriwa na moto huo.

Nigeria imerekodi ongezeko la karibu 400% la bei ya mafuta tangu Juni kufuatia kuondolewa kwa malipo ya ruzuku na Rais Bola Tinubu, hatua ambayo imezidisha gharama ya juu ya maisha na bei za bidhaa, lakini serikali inaamini inalenga kuokoa mapato na kurejesha fedha za ruzuku ya mafuta kwa sekta zingine.

Mzalishaji mkubwa zaidi wa mafuta barani Afrika huagiza zaidi ya 90% ya mahitaji yake ya mafuta kutokana na kutokuwa na uwezo wa kusafisha mafuta ghafi ndani ya nchi kwa sababu mitambo yake minne ya kusafisha mafuta haifanyi kazi.

Chanzo BBC

 
Mbona tumesikia Bwn. Dangote kafungu mtambo wa kusafisha mafuta. Kwahiyo bado wanaagiza mafuta?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom