Zaidi ya 4,000,000 hawakuona majina yao, nec tupe majibu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zaidi ya 4,000,000 hawakuona majina yao, nec tupe majibu.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MWANA WA UFALME, Nov 6, 2010.

 1. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja na nec kueleza kuwa iliweka mikakati ya kuwasaidia watu ambao hawakuona majina yao, bado idadi inahisiwa kuzidi million nnne ya waliokosa kupiga kura kwa kukosa kuona majina yao.

  Tusilaumu wananchi kwamba hawakujitokeza, bali tuiulize nec kwanini watu wafike vituoni kupiga kura wakiwa na kadi za kupiga kura na warudishwe!. Watu hao hao walipiga vituo hivyo hivyo mara chaguzi zilizopita lakini huu eti majina hayakuonekana.

  Inavyoonekana huu ulikuwa ni mkakati wa makusudi. Kila kituo kilikuwa na zaidi ya watu kumi waliokosa kuona majina. This is not coincidence. Nec itupe majibu ya maswali haya kabla haijaanza kujitetea eti watu hawakujitokeza.
   
 2. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,780
  Likes Received: 6,265
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kuwaomba NEC watoe maelezo leo ni sawa na kuipigia mbuzi guiter. Kwanza hawa NEC wameshamaliza kazi yao. Cha msingi ni kutafuta means za kuifutilia mbali hii NEC.

  Nina imani wabunge waliochaguliwa (CCM na Upinzani) kwa pamoja wanaweza kuanzisha motion bungeni na kuona jinsi gani NEC mpya, iliyo huru, na iliyo an wafanyakazi wasio na haja ya kulamba miguu ya mtu yeyote, inaweza kupatikana ili angalau kupunguza matatizo makubwa kabisa yaliyojitokeza kwenye uchaguzi wa mwaka huu.....japo matatizo hayo kwa 90% yalikuwa fabricated makusudi

  Tumeanza kufanya uchaguzi wa vyama vingi tangu mwaka 1995 na badala ya kusonga mbele, sisi tupo tunarudi nyuma tu. Inasikitisha na kuumiza sana. Kiravu na Makame ni vilaza tu na wasipoangalia huko mtaani, wanaweza kujikuta wanapata ''accidents''.

  Itakuwa ni upotezaji wa muda kuingia kwenye uchaguzi mwingine kwa utaratibu tulionao sasa. Kama wabunge wa upinzani watashindwa kuleta mabadiliko kwenye muundo na ufanyaji kazi wa NEC, nathubutu kusema kwamba hakutakuwa na haja ya kufanya uchaguzi mwaka 2015. Ni bora tujue moja kwamba kuna utawala wa kiimra kama ilivyo kwa Museveni au kwa Mugabe, na kwamba CCM imedhamiria kabisa kuhodhi kiti cha uRais milele dumu.
   
 3. R

  Rugemeleza Verified User

  #3
  Nov 6, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu kutegemea wabunge wa ushindani kuendesha mapambano ni kuingia katika mtego wa CCM. Mapambano lazima yawe nje na ndani ya bunge. Ni lazima tuendeshe vuguvugu kali nje kuhusu umuhimu wa katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na umuhimu wa kuwa na demokrasia ya kweli. Pale moto utakapowaka nje ndipo Kikwete na watu wake wataelewa umuhimu wa Katiba mpya. Hivyo shinikizo lazima liletwe na sisi Watanzania. Hivyo hoja ni namna gani tunaweza kuanzisha, kuendesha na kukuza vuguvugu hilo.
   
 4. w

  werawera Senior Member

  #4
  Nov 6, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  hapo kwenye RED nimekusoma tulizingatie hili mazee.
   
 5. C.K

  C.K JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Kweli tunahitaji tume huru ambayo watendaji wake hawatakuwa waajiriwa yaani watumishi wa umma bali wawakilishi wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi. Hapo hakutakuwa na mwanya wa kuchakachua kura za mtu!
   
 6. C.K

  C.K JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
   
 7. J

  JIWE2 Senior Member

  #7
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ongezea wanafunzi zaidi ya 60,000 hawakuweza kupiga kura.
   
Loading...