Yuwapi Komredi Benard Membe?

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,849
67,285
Ni muda mrefu sasa umepita sijamsikia jasusi mbobezi na mwanadiplomasia mahiri ndugu Benard Membe ambaye siku za awali za utawala wa JPM alijitahidi kutoa matamko mbalimbali kadri anavyojisikia. Kwenye sakata kama hili la sukari nimjuavyo angeshatoa tamko tena zito haswa.

Lakini sasa shushushu huyu hasikiki wala kuonekana kwenye media kama hapo awali, nini kimemsibu? Anayejua aje atujuze alipo mbunge huyu mstaafu wa pale Mtama.
 
Unaonekana unamchukia, jiepushe na hilo
 
Magufuli kawapoteza wengi.
Hata kina Mama Tanzania,Six ,Wenje nk.
Wote hawapo kwenye ramani.
Edo kidogo naye anajitutumua!!
 
Teheeteeh, Membe alisema 2016 maadui zake watakimbia nchi, imekuwa kinyume yeye ndio kakimbia maadui zake. Siasa bana eti nae alikuwa aishi magogoni?! mtama tu ilimshinda nchi nzima ingekuwaje?
hahaha...eti maadui zake wangekimbia nchi? hao maadui zake ni akina nani? tujuze mkuu
 
Adui yake mkuu kwenye ile ligi ya kuingia magogoni alikuwa LOWASA, sasa badala ya Lowasa kukimbia nchi, Membe amekimbizwa na kivuli tu cha Lowasa maana Lowasa alisha muacha ndani akatoka nje ila kivuli kikafanya yake now membe ni historia.
 
ahsante!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom