Yutong/zongtong/Higer and scania buses

Kwa hiyo kuna wabongo wamewekeza kwenye biashara ya mabasi Zambia na SA!
hayo Shalom ni ya Mtanzania na wengine Zimbabwe wanatoa Harare/Johannesburg na Harare/Messina hizo Nchi ni rahisi kuwekeza mkuu abiria wengi wenye kipato na pia mizigo ni mingi inayokwenda mfano Zambia na kodi yao reasonable na mkimalizana boarder basi hakuna Longo Longo tena ndio maana Lusaka na kitwe wafanyabiashara wakubwa wengi ni Watanzania wana Maroli yao ya kupakia mzigo Jozi mpaka Lusaka..,
 
Kila mtu/mfanyabiashara tunaangalia faida hayo mambo ya sijui scania sijui yutong mara zonghton sijui nini mnasema nyie msio na shekeli.

Wewe ukitaka bus zenye ubora kakope bank na ununue hizo sijui ndiyo irizal v 7i na hiyo tela yake alafu zilete hapa ubungo!!.
 
Kila mtu/mfanyabiashara tunaangalia faida hayo mambo ya sijui scania sijui yutong mara zonghton sijui nini mnasema nyie msio na shekeli.

Wewe ukitaka bus zenye ubora kakope bank na ununue hizo sijui ndiyo irizal v 7i na hiyo tela yake alafu zilete hapa ubungo!!.
Kweli kabisa mkuu.
Wabongo tumeanza kuwa na porojo nyingi kama Wakenya. Mimi kuna siku nilimsikia mkenya anasifia zile Gari zao zimechorwa chorwa uchafu. Nikamwambia upuuzi Tanzania aupo
Biashara ya magari ni biashara ngumu sana kuwamudu madereva. Unanunua Scania ya 500 milioni unampa dereva ambaye anakula mirungi, bangi na kila aina ya Madawa ya Kulevya. Ni bora kununua magari ya kichina ambayo ni bei nzuri kuliko kuja kupata hasara
 
Tuwe wa kweli scania wapo vizuri. Lakini mchina anasoma upepo wa soko na uhitaji. Nina uhakika Mchina anaweza akatengeneza magari kama hayo ya Scania lakini shida itakuwa wakuwauzia. Pia ukumbuke hizi fashion mpya za mabasi zinatoka kila siku. Sasa ukikomaa kununua za zamani ndio unajimaliza. Pia mwendo wa mabasi hayo una athari kibiashara. Mchina nae yupo vizuri katika hilo.
 
R̤̈ö̤ö̤ẗ̤ ÿ̤ä̤ d̤̈ä̤r̤̈-m̤̈b̤̈ë̤ÿ̤ä̤ ï̤n̤̈ä̤ẗ̤ë̤g̤̈ë̤m̤̈ë̤ä̤ n̤̈ä̤ ẗ̤ï̤m̤̈ï̤n̤̈g̤̈ s̤̈ö̤m̤̈ë̤ẗ̤ï̤m̤̈ë̤ f̤̈ö̤r̤̈c̤̈ë̤ ẅ̤ä̤ k̤̈ẅ̤ä̤n̤̈z̤̈ä̤ m̤̈ṳ̈d̤̈ä̤ m̤̈ẅ̤ï̤n̤̈g̤̈n̤̈ë̤ ï̤l̤̈ä̤s̤̈ï̤ l̤̈ä̤b̤̈d̤̈ä̤ m̤̈ṳ̈ö̤n̤̈g̤̈ë̤l̤̈ë̤ë̤ r̤̈ö̤ö̤ẗ̤ z̤̈ï̤n̤̈g̤̈n̤̈ë̤
 
Kisbo ni mabasi ambayo ni Scania, Yale magari yako imara sana na yanamudu mwendo kasi na urefu wa safari. Yutong safari ndefu lazima ufungue pale mbele upepo upige la cvyo yanalipuka.
Yaani kuna posts nkizisoma nabaki kucheka tu.

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha!
 
kama swala la luxury ndugu yangu umeshapanda zile gari za modern cost ni scania ila ndani ni zaidi ya fast jet kuna zile za nairobi mombasa ni single siti kuna jamaa anaitwa air bus pale nairobi anachonga body wacha kabisa youtong zinasubiri
Tuma picha Mkuu
 
Mkuu nakuomba ingia Wikipedia, usiingie Google, utakuta option nyingi, ukiingia huko directly tafuta hizo Higer uone. Hao wachina ni kiboko. Tena wameingia ubia wa kitengo cha R&D,kimsingi walishirikiana kutoa Engine na hao Scania. So naamini Wachina wakiamua kutoa kitu kwa matumizi ya Wazungu kinakua cha ukweli mno
Ila nahisi bei haiwezi kubaki ile ile.
 
Dar express anazo Scania Marcopolo Viaggio 1050 gharama ya bus moja nikama milioni 900 bado ushuru na Kilimanjaro Express anazao pia macropolo za kawaidia katika historia ya mabus Tanzania ni Dar express tu ajawai nunua mchina na kwenye historia yake ameshawai kuwa na bus za scania na mercedez benzi zenye body ya Marcopol,Irzar na Dar Coach Body.Katika biashara kuna na ghari ya gharama nyingi unakaa nayo miaka 10 bila usumbufu na inakupa faida na kurudisha gharama zote ndio biashara nzuri,mabus mengi ya kichina baada ya mda wamiliki ubadili Injini na kuweka ya Scania,Gear Box na Deaf ndio siri watu wasio ijua,chines bus azidumu miaka miwili au mitatu mara nyingi wanabadilisha na kuvika injini ya scania,deaf na gear box hiyo ndio siri wengi awaijui.Nimepita kenya na uganda haya mabus ya kichina sio mengi huko kama huku.Pia kitu cha bei rahisi kina faida na hasara zake.Mfano mzuri mabus mengi ya Higer viti vyake sio rafiki kwa watu warefu,yutong na Zhongtong au Kinglion kidogo viti ni vizuri na pia hizi gari zinachoka sana mapema miaka miwili au mitatu ni mingi.Na mara nyingi mabus ya china yanayotengenezwa kwa soko la ulaya ni tofauti kabisa kiviwango wenzetu wana viwango walivyoweka vya bus liweje la safari fupi au safari ndefu,na ghararama ya hilo bus kwa viwango vya ulaya japo limetengenezwa china gharama zinakuwa kubwa sana karibu na kununua scania,man,volvo,mercedes,nissan,issuzu n.k.
Asante Mkuu
 
Back
Top Bottom