Mabasi aina ya Scania na Mercedes Benz vs Yutong na Zongtong: Mchina ameuza ramani ya vita kwa adui

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,782
Chasis ya Scania Bus engine nyuma

Miaka ya nyuma Scania ndio alikuwa mfalme wa kusafirisha abiria na mizigo hapa nchini. Wamiliki wa mabasi waliziamini sana Scania kwa uimara wake na mwendo barabarani.

Miaka ya katikati Mchina akaleta mabasi ya YUTONG na Zongtong. Matajiri wengi wakazimbilia basi hizi kwasababu ya ulaji mdogo wa mafuta, bodi nzuri, interior design, na unafuu wa vipuri.

Njia nyingi Scania zikaanza kuadimika, na watu wakasahau makali ya muziki wa Scania Njia ya Mbeya Kuna mabasi yanaitwa Sauli, ni Scania na Mercedes Benz. Yutong na zongtong zinaonekana kama Leyland CD, zinapitwa kama zimesimama, iwe ni mlimani, tambarare au mteremkoni, Mchina anapigwa home and away.

Pia nimeshawahi kusafiri sana na Volvo za Zainabs, mwendo wake haukuwa wa kitoto Wala wa kimama, ngoma ni mbio, nguvu, balance na stability ya uhakika.

Sasa naona kama mchina anaanza kupoteza imani kwa namna mabasi ya Sauli yanavyomfanya huko Mbeya.
 
Mchina yule yule wa tecno, itel na infinix ndiye yule yule wa zhongtong, higher, youtong hajawahi kuwa serious kwenye kazi.

Basi kama lake linauzwa mil 900,yeye anaunda lake anauza ml 250, halafu mtu anakuja kubeza scania/ benz/ volvo si lolote si chochote, basi unamuangalia halafu unafanya ihiiiiiiiiiiiiiiiiiiii (kwa sauti ya Magu).
 
Unataka kusema nn. Mabasi yote yamefungwa speed limit, barabarani Kuna touch, huo mwendo Ni upi? Issue kubwa hapo Ni unafuu wa manunuzi na uendeshaji wa mabasi ya kichina basi
Sawa kuna speed limit , mfano kwanin mara nyingi sauli ambayo ni scania inawahi kufika mbeya..

1) madereva wazuri
2)ubora wa gari,, milima sio mchezo kwa mchina
3)scania za sauli zimefungwa booster kwa hiyo kwenye humps inapita na zote na watu ndani ya gari wanakua comfortable tu,, sasa pitisha mchina mtagongesha kwenye roof ya gari mpaka mvunjike shingo
 
Unataka kusema nn. Mabasi yote yamefungwa speed limit, barabarani Kuna touch, huo mwendo Ni upi? Issue kubwa hapo Ni unafuu wa manunuzi na uendeshaji wa mabasi ya kichina basi
Either hujui au haupo makini, gari kukimbia ni kitu kimoja na gari kuhimili kukimbia ni kitu kingine kabisa , mabasi yana speed limit ya 85km/h, lakini wastani wa mwendo hutofautiana kadiri engine inavyokuwa dhaifu milimani.

Mchina basi karibu zote anatumia technology ya euro 1, mechanical injector pump na nozzle , scania za f95 ni euro 5, common rail fuel injection , variable geometry turbocharger etc Ni very efficient, kiasi kwamba waliamua kupunguza cylinder moja , kwa option za mabasi,
F95 Ina uwezo wa kumaintain speed ya 85 kwa kipande kirefu, ndo maana sauli inakuwa ya kwanza kila siku

Sent
 
Either hujui au haupo makini, gari kukimbia ni kitu kimoja na gari kuhimili kukimbia ni kitu kingine kabisa , mabasi yana speed limit ya 85km/h, lakini wastani wa mwendo hutofautiana kadiri engine inavyokuwa dhaifu milimani. Mchina basi karibu zote anatumia technology ya euro 1, mechanical injector pump na nozzle , scania za f95 ni euro 5, common rail fuel injection , variable geometry turbocharger etc Ni very efficient, kiasi kwamba waliamua kupunguza cylinder moja , kwa option za mabasi,
F95 Ina uwezo wa kumaintain speed ya 85 kwa kipande kirefu, ndo maana sauli inakuwa ya kwanza kila siku

Sent
Very logical reply
 
Gari ya kichina Ni gari ya mapito Sana kwa watu wenye quick cash, kwa watu wenye kuijua hii biashara hawezi kuhangaika na gari ya kichina kwa sababu service life zake no kidogo sana, na mind you gari za kichina sio rahisi kivile .

Kwenye industry ya transportation chombo kuhudumu kwa muda mrefu Ni moja ya faida, majinja hajanunua basi mpya lakini anakwrnda Mbeya kiuhakika zaidi na kwa miaka mingi zaidi, kwa kutumia mtaji kidogo na inawezekana akawa na base kubwa ya wateja , kuliko basi nyingi za kichina kwa huko mbeya na sumbawanga,

Kukipambazuka watu watajua ni kiasi gani cha pesa na muda walipoteza kumiliki magari ya kichina


Sent
 
Miaka ya nyuma Scania ndio alikuwa mfalme wa kusafirisha abiria na mizigo hapa nchini. Wamiliki wa mabasi waliziamini sana Scania kwa uimara wake na mwendo barabarani.

Miaka ya katikati Mchina akaleta mabasi ya YUTONG na Zongtong. Matajiri wengi wakazimbilia basi hizi kwasababu ya ulaji mdogo wa mafuta, bodi nzuri, interior design, na unafuu wa vipuri...
Sasa huo ndio uchawi.....
 
Gari ya kichina Ni gari ya mapito Sana kwa watu wenye quick cash, kwa watu wenye kuijua hii biashara hawezi kuhangaika na gari ya kichina kwa sababu service life zake no kidogo sana, na mind you gari za kichina sio rahisi kivile...
Kuna siku nilipanda Majinja pale Simike sàa nne asubuhi, saa tano usiku tuko UB mwisho wa safari
 
Mercedes Mzee ni shida nyingine hiyo kwanza inatembea tuu swala la matengenezo sio leo wala kesho sasa ukute kaweka Engine ya Actros humo si balaa hilo maana Actros inataka kubeba mzigo mkubwa harafu inabeba abiria hao wachache atabaki kusifiwa tuu...maana bodi ni ya Kenya ile sio merc au ya Scania kama nilivyosikia..
 
Back
Top Bottom