Yusuf Manji akamatwa kutokana na malimbikizo ya kodi Tsh 300 milioni, ofisi zake zafungwa

Rostam Aziz aliona mbali. Uchwara uchwara ulipoanza kunukia kasepa. Huyu naye akianzishe tu ,vinginevyo ataanza kuokota makopo soon.Jamaa si kasema "wataishi kama shetani???!!!
Hivi Rostam kajichimbia wapi?
 
Kampuni ya Udalali ya Yono (Yono Auction Mart) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tawi la Temeke leo Oktoba 27 wamemkamata mfanyabiashara Yusuf Manji kutokana na kutolipa malimbikizo ya kodi anayodaiwa zaidi ya Tsh 300 milioni.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Yono, Scolastica Kivera alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kwamba mbali na kumkamata Manji, pia wamefunga nyumba ya kuhifadhia mali (godown) pamoja na Ofisi yake iliyopo kando ya barabara ya Nyerere ili alipe kodi anayodaiwa na Serikali.

Yono ambao ni wakala wa ukusanyaji wa madeni ya Serikali kupitia TRA, wamesema kwamba wanamshauri Manji alipe deni analodaiwa ili waweze kufungua majengo yake wanayoyashikilia kwani kinyume na hapo watapiga mnada mali zilizopo ndani ya majengo kwa idhini ya TRA ili waweze kufidia deni hilo.

Kivera ameeleza kwamba, hatua ya wao kushikilia mali hizo ni kumtaka Manji alipe deni analodaiwa.
Weziiii....
Kuna kisa kimoja kilitokea miaka ya zamani...Nyerere alimtuma Alnour Kassoum aliekuwa waziri wake wa fedha kwenda zanzibar kwa karume kumtaka lazima fedha za kigeni ziwekwe Bara BOT.
Karume alivunja protocol za kuongea..na kwa vile Alnoor alikuwa mhindi akamwambia kwa hindi...Chooor Choor....toka hapa hututakii mema ....yaan mwizi mwizi...
Sasa na hawa TRA ni wezi sasa hawamtakii mema Manji wala wafanya biashara...
Pili manji ni chairman wa bodi ya makampuni ya Quality Group.
Invidual companies zake kuna Managing Director ambao ndo waendeshaji wa hizo kampuni wao ndio wa kukamatwa kwani watakuwa na maelezo.
Ila hapa lengo ni manji.
Huyu Manji hapumziki na ngoma za chato mpaka aongee kisukuma
 
Duh ! Labda Inaweza kuwa kweli kwamba kakwepa kodi lakini napata shaka mahali huyu jamaa wamemuandama sana kesi
Za uonevu na kutafuta kiki hizi zinanitishia shaka

Mfano île kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya

●Tunapaswa kujiuliza :

♢ Je Hivi kuna mtu yeyote kati ya wale watuhumiwa wa île kesi ya madawa ya kulevya alipatikana na hatia?

♢Je Ni kweli kwâmba sikuhizi hakuna walanguzi wa madawa ya kulevya na watumiaji pia katika taifa letu ?

♢Je Ni kweli Unga pendwa "Coke" na ndugu zake kama "Hero" achilia mbali "mchicha jamaica " hawaingizwi nchini sikuhizi ?

Tukijibu haya maswali nadhani tunaweza kupata mwanga wa kinachoendelea
 
Ahadi nideni na huyu mungu Wa tz anaejibaraguza kua msema kweli nimpenzi wamungu na haliyakwamba yeye ndio muongo nambari moja aliaidi waliokua wakiishi kama malaika atahakikisha wanaishi kama mashetani yupo kazini kumalizia ahadi zake.
 
Yono tulisikia Mali zao zinauzwa, je zimeuzwa kwanza zao? Sio vimbelembele Mali za watu wakati nao niwadaiwa sugu
 
TANGU LINI TRA WAKAKADIRIA KODI YA KWELI?

WALIMKADIRIA ACACIA TR 425 KUMBE NI BN 700

SASA MANJI WAMEMKADIRIA M 300, SI AJABU HAWAMDAI HATA SENTI TANO.
 
Kampuni ya Udalali ya Yono (Yono Auction Mart) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tawi la Temeke leo Oktoba 27 wamemkamata mfanyabiashara Yusuf Manji kutokana na kutolipa malimbikizo ya kodi anayodaiwa zaidi ya Tsh 300 milioni.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Yono, Scolastica Kivera alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kwamba mbali na kumkamata Manji, pia wamefunga nyumba ya kuhifadhia mali (godown) pamoja na Ofisi yake iliyopo kando ya barabara ya Nyerere ili alipe kodi anayodaiwa na Serikali.

Yono ambao ni wakala wa ukusanyaji wa madeni ya Serikali kupitia TRA, wamesema kwamba wanamshauri Manji alipe deni analodaiwa ili waweze kufungua majengo yake wanayoyashikilia kwani kinyume na hapo watapiga mnada mali zilizopo ndani ya majengo kwa idhini ya TRA ili waweze kufidia deni hilo.

Kivera ameeleza kwamba, hatua ya wao kushikilia mali hizo ni kumtaka Manji alipe deni analodaiwa.
TRILION 400 BARICK/ACASIA VIPI ZILISHALIPWA ??
 
Back
Top Bottom