Huu uzi haujaandikwa leo wala jana. Tazama tarehe yake kwenye post namba moja.Kufa ni jambo la lazima haina hata haja ya utabiri...
Vipi baada ya kufa mmepata hilo eneo lenu?
Baada ya kumsomea albadili na kumshitakia kwa mungu wenu mmepata hilo eneo?
AmenNa Mwenyeezi Mungu ndiye ajuwae zaidi.
Nimekuibia idea siyo!!Nilijua tu nitakutana na comment kama hii ndio Maana sikutaka kua na kiherehere cha kuicomment!
😂😂
Hapana, kasome tena. maudhui ilikuwa ya kumtakia mema sana Manji.Ndiyo tunajuwa ni thread ya zamani 2017, lakini maudhui yake yalikuwa yanataka Yusuf Manji apatwe na mabaya. Na kweli yamempata kwa dua zako FaizaFoxy
Haujaiba ila mawazo yetu yamegongana mkuu ulichowaza nimewaza kabla sijaona comment!Nimekuibia idea siyo!!
Yussuf Manji, ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu utakufikia popote ulipo.
Binafsi kama Muislam mwenzako nnachukuwa fursa hii kukukumbusha kuwa hakuna kitu bora kama kukiri na kukubali makosa yako na kuomba toba.
Toba nnayokushauri kuiomba hapa, si kwa serikali wala kwa watawala. Toba nnayokukumbusha mimi kuiomba ni kwa Mola wako Muumba mbingu na ardhi.
Manji uliwakosea sana Waislam kipindi cha nyuma kiasi, kwa kutumia fedha zako kununulia viwanja vya wakf vya Waislam, na kuwa mkaidi kila uliposemeshwa kuhusu hilo.
Viwanja hivyo ambavyo historia inaonyesha kuwa vilikuwa vijengwe chuo kikuu cha kwanza Tanganyika (hilo halikufanyika lakini hilo ni simulizi jingine kabisa ambalo Alama Mohamed Said anaweza kulisimulia vizuri zaidi).
Ulifatwa na Waislam wakikuomba kuwa mkataba ulioingia na BAKWATA ni wa kidhalimu na haufai lakini kwa ukaidi wako hukuwasikiliza na uliwatoa njiani na kuendelea na mkataba wako.
Sakata la viwanja hivyo lilipelekea Waislam kufungwa, kupigwa na kujeruhiwa mpaka walipoona kuwa hawakuwezi kwa ajili ya kutumia fedha zako na nguvu ya baadhi ya waliokuwa BAKWATA, Waislam wakafikia maamuzi makali ya kuwa sasa wanakushtaki kwa Mwenyeezi Mungu.
Miaka imepita ukidhani kuwa shtaka hilo halina meno kwako, lakini leo tunashuhudia ukigeukwa kila upande.
Aibu ya kushikwa na kuwekwa ndani pekee si ndogo kwa mtu wa "caliber" yako. Licha ya kupimwa na kukutwa kuwa u mlevi wa madawa, tumeona sakata la Oysterbay likikutia hasara kubwa sana, tumeona wafanyakazi wako wakifungiwa kuingia kwenye ofisi zao, tunasikia akaunti zako zinafungiwa kila kukicha.
Kama hiyo haitoshi, tunasikia umepatwa na matatizo ya moyo. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an tukufu:
Qur'an 2:10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. Maelezo
Kwa yote hayo bado tu hujashtuka ni kwanini yakukute yote hayo? Nakusihi, zingine zote ni sababu lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, Waislam wameitikiwa dua zao dhidi yako.
Yussuf Manji tunakutaka usiwe katika wale ambao:
Qur'an 2:7. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. Maelezo
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na hachoki kusamehe, tunakutaka uombe toba kwa mola wako, umtake radhi, uwatake radhi na Waislam na uwarudishie viwanja vyao na mali zao, tena usithubutu kuvirudisha kwa wale wale waliokuuzia, itakuwa haina maana kabisa. Virudishe kwenye taasisi za Kiislam zenye kumuogopa Mwenyezi Mungu au tumia viwanja hivyo hivyo kuanzisha Manji Islamic Trust Fund na uiendeshe mwenyewe kwa manufaa ya Waislam.
Fata nasaha hizo uone mambo yatavyokunyookea.
Jikumbushe:
Maimamu kumsomea Manji Ahla-badri
Mjue Sheikh Ponda Issa Ponda na Kundecha
Waislamu wataka jengo lao toka Quality Group | Bongo5.com
MKATAMBUGA: WAISLAMU WAMELOGWA NA NANI?
Manji hakuna wakukuokoa katika haya na hayatokwisha ukifanya dharau isipokuwa wewe mwenyewe, anza kwa kumrudia Allah na kumuomba toba.
Na Mwenyeezi Mungu ndiye ajuwae zaidi.
Je waislamu wanaoiba mali za wanyonge wapo sahihi? tuanze na hao kwanzaSamehe saba Mara sabini elfu. Badala ya kumsamehe wao wanamsomea albadir. I guess Manji siyo muislam ila ni hinduism
wangapi wamekufa kwenye hiyo miaka 7? kifo ni kifo tu kila nafsi itaonja mauti2017~2024
7 yrs jamaa kakata moto dah
RIP.
Yussuf Manji, ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu utakufikia popote ulipo.
Binafsi kama Muislam mwenzako nnachukuwa fursa hii kukukumbusha kuwa hakuna kitu bora kama kukiri na kukubali makosa yako na kuomba toba.
Toba nnayokushauri kuiomba hapa, si kwa serikali wala kwa watawala. Toba nnayokukumbusha mimi kuiomba ni kwa Mola wako Muumba mbingu na ardhi.
Manji uliwakosea sana Waislam kipindi cha nyuma kiasi, kwa kutumia fedha zako kununulia viwanja vya wakf vya Waislam, na kuwa mkaidi kila uliposemeshwa kuhusu hilo.
Viwanja hivyo ambavyo historia inaonyesha kuwa vilikuwa vijengwe chuo kikuu cha kwanza Tanganyika (hilo halikufanyika lakini hilo ni simulizi jingine kabisa ambalo Alama Mohamed Said anaweza kulisimulia vizuri zaidi).
Ulifatwa na Waislam wakikuomba kuwa mkataba ulioingia na BAKWATA ni wa kidhalimu na haufai lakini kwa ukaidi wako hukuwasikiliza na uliwatoa njiani na kuendelea na mkataba wako.
Sakata la viwanja hivyo lilipelekea Waislam kufungwa, kupigwa na kujeruhiwa mpaka walipoona kuwa hawakuwezi kwa ajili ya kutumia fedha zako na nguvu ya baadhi ya waliokuwa BAKWATA, Waislam wakafikia maamuzi makali ya kuwa sasa wanakushtaki kwa Mwenyeezi Mungu.
Miaka imepita ukidhani kuwa shtaka hilo halina meno kwako, lakini leo tunashuhudia ukigeukwa kila upande.
Aibu ya kushikwa na kuwekwa ndani pekee si ndogo kwa mtu wa "caliber" yako. Licha ya kupimwa na kukutwa kuwa u mlevi wa madawa, tumeona sakata la Oysterbay likikutia hasara kubwa sana, tumeona wafanyakazi wako wakifungiwa kuingia kwenye ofisi zao, tunasikia akaunti zako zinafungiwa kila kukicha.
Kama hiyo haitoshi, tunasikia umepatwa na matatizo ya moyo. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an tukufu:
Qur'an 2:10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. Maelezo
Kwa yote hayo bado tu hujashtuka ni kwanini yakukute yote hayo? Nakusihi, zingine zote ni sababu lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, Waislam wameitikiwa dua zao dhidi yako.
Yussuf Manji tunakutaka usiwe katika wale ambao:
Qur'an 2:7. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. Maelezo
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe na hachoki kusamehe, tunakutaka uombe toba kwa mola wako, umtake radhi, uwatake radhi na Waislam na uwarudishie viwanja vyao na mali zao, tena usithubutu kuvirudisha kwa wale wale waliokuuzia, itakuwa haina maana kabisa. Virudishe kwenye taasisi za Kiislam zenye kumuogopa Mwenyezi Mungu au tumia viwanja hivyo hivyo kuanzisha Manji Islamic Trust Fund na uiendeshe mwenyewe kwa manufaa ya Waislam.
Fata nasaha hizo uone mambo yatavyokunyookea.
Jikumbushe:
Maimamu kumsomea Manji Ahla-badri
Mjue Sheikh Ponda Issa Ponda na Kundecha
Waislamu wataka jengo lao toka Quality Group | Bongo5.com
MKATAMBUGA: WAISLAMU WAMELOGWA NA NANI?
Manji hakuna wakukuokoa katika haya na hayatokwisha ukifanya dharau isipokuwa wewe mwenyewe, anza kwa kumrudia Allah na kumuomba toba.
Na Mwenyeezi Mungu ndiye ajuwae zaidi.
Yeah dunia tunapita.wangapi wamekufa kwenye hiyo miaka 7? kifo ni kifo tu kila nafsi itaonja mauti
Hakuna jipya kwenye kifo, leo wamekufa mapadre watatu huko kusini nao wameiba mali za waislamu?Yeah dunia tunapita.