Yupo wapi waziri wa maliasili na utalii? Je ameliona hili!

Mwanjigwene

Member
Mar 1, 2021
30
26
Kuna udhalimu nimeuona chini ya jua, maskini akiwa na gunia lake moja la mkaa, auze asaidie familia yake, ananyang'anywa na wafanyakazi/askari wa maliasili, sambamba na kuchukua simu na baiskeli, maana ni vya thamani!

Mtuhumiwa anaachwa guru! (huo nao ni ubatili) Mtuhumiwa Hugo anapokwenda kudai Mali zake anatozwa sh 100000. Hivi mnashindwaje kuwafikisha mahakamani, wahalifu hao, hivii hakuna njia nzuri ya kulishughulikia jambo hili?

Nimeliona hili mahali pengi! Vwawa Mkoani Songwe mmezidi Mwogopeni Mungu, mwenyezi Mungu hapendi dhuluma! soma isaya61:8 mtakuja kuwapa laana watoto wenu bila sababu za msingi, maana yeye huvika watoto makosa ya baba zao haa ta kizazi cha nne!

Kazi iendelee!
 
Back
Top Bottom